Swali Chokonozi: Hivi ni kweli Mwanza ni Maskini kuliko hata Dodoma na Katavi?

Nimevumilia sana; NIMESHINDWA-- nioneni tu mbeya lakini tuhuma mzito kama hizi, sina budi kumuita Kaka Pasco! Kaka Pasco, inasemekana huna lolote wewe Msukuma fake mtoto wa Kizaramo:
Kwanza Wasukuma hawana makabila madogo madogo...huo ni uongo wako tu kwanza utakua msukuma wa Dar wewe...!
Kwahiyo ni kwamba hapo juu aache kujiita Chapa Ng'ombe sio wakati hata akitaka kunywa mtindi sharti aujaze sukari, au!
Wazinza wako Uzinza na si wasukuma na wakerewe wako Ukerewe na si Wasukuma na hawaongei kisukuma ila wamemezwa tu na kabila kubwa.Hakuna kinyantunzu usukumani ila kuna kisukuma cha lafudhi ya watu wanaotoka Bariadi (na Kinyantuzu inatokana na tarafa ya Tunzu)
Duh! Hilo darsa hapo juu ni tosha kabisa kumfanya mtu ajitathmini na kutafakari ikiwa kweli nae ni Chapa Ng'ombe au ni Chapa Kiepe Yai tu kama sie wengine!!
Wasukuma wa Mwanza ni sawa na Wanyamwezi tu
Basi tutakuwa tunatandika nao urojo huku Uswahilini!
Wasukuma halisi wanatoka bariadi na sehemu za Busega ukijumuisha na Bunda yaani wale amabo wako karibu na Mbuga...Lakini hawa wengine kazi yako ni kuvaa shanga tu
What did you just say? SHANGA?! This's serious ACCUSATION against... oh shit! How dare you?! Watch your fingers while typing young man! You mean Pasco possibly nae ni mvaa... (shit! Got no gut to complete the sentence)! Lakini acha kutisha watu bhana, hata Wamasai nao wanavaa shanga... au nao ni Wamasai wa Chalinze na Bagamoyo... nyama sharti kwa nazi!!
 
Acha uongo wewe Toka lini uliona kwenye TV Bariadi inagawiwa chakula? Bariadi ndo wanakotoka wanyantuzu wakulima wa pamba na wafuga ng'ombe wanaokula ugali mgumu na wanapenda wanawake weupe.Au unasemea Wanyantuzu wa wapi? Kwanza Wasukuma hawana makabila madogo madogo...huo ni uongo wako tu kwanza utakua msukuma wa Dar wewe...Wazinza wako Uzinza na si wasukuma na wakerewe wako Ukerewe na si Wasukuma na hawaongei kisukuma ila wamemezwa tu na kabila kubwa.Hakuna kinyantunzu usukumani ila kuna kisukuma cha lafudhi ya watu wanaotoka Bariadi (na Kinyantuzu inatokana na tarafa ya Tunzu) japo wanaoitwa wanyantuzu hawakai Ntuzu yenyewe wanakaa Kanadi,Itilima,Dutwa na baadhi ya maeneo ya Meatu .Pia wanyantuzu si Masikni maana wao wanatoka mkoa wa Simiyu na si Mwanza
Umasikini kwa Mwanza na Geita ni sababu moja kijijini kuna watu wanaoa wanawake wengi sana tofauti na uwezo wao halafu kulima ni wazembe,Wasukuma wa Mwanza ni sawa na Wanyamwezi tu,hawana nshu za maana....
Wasukuma halisi wanatoka bariadi na sehemu za Busega ukijumuisha na Bunda yaani wale amabo wako karibu na Mbuga ya serengati,hao ndo walikua wanapambana na wamasai kwa miaka nenda Rudi,ni jasiri na mashujaa....Lakini hawa wengine kazi yako ni kuvaa shanga tu
Wanaovaa shanga si wasukuma, fuatilia historia
 
Sipendi kukataa au kukubali kwamba Mwanza kuna maskini wengi kwa kuwa mtoa taarifa hajatoa takwimu kuonyesha namna alivyofanya calculation zake ila .....

Mmimi naishi jijini Mwanza ambap naona kiukweli maisha ni mazuri kwa walio wengi (mijini). Ukitoka tu pembeni mwa mji let say 1 km .. unaweza kushangaa ...

Kuna siku niliamua kutembea kwa mguu kutafuta maeneo ya mashamba nje ya mji, (naishi Igoma). Niliingilia mnada wa ng'ombe nyuma ya kiwanda cha Coca ... kama nusu kilometa toka kwenye lami ... dah! niliyoyaona huko ni ya kushangaza... nilikutana na familia zenye hali ngumu hadi nilishangaa .. ilikuwa mwaka 2008....

Mwaka huu nimepita tena maeneo hayohayo .. mambo ni tofauti kabisa ... kumebadilika sana ...sikutegemea ...

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba huenda mtoa taarifa alifanya utafiti wake miaka ya nyuma kidogo ... Mwanza kama mwanza ni mkoa unaobadilika sana kimaendeleo ... na seerikali ikiwekeza kwenye mazao yanayopatikana kwenye mkoa huu; basi Mwanza ndo itakuwa tajiri zaidi ya mikoa mingine yote hapa Tanzania.
 
Sana mie sio mtu wa kanda ya kaskazini lakin nimepita Arusha na kilimanjaro mpaka vijijini. kuko vizuri sana
Haya mambo yana sababu nyingi sana na wala hatuwezi kurely katika jambo moja fulani. Juzi ulisikia unatajiwa na mikoa iliyo na viwanda vingi, huo ukanda una mikoa yote yenye viwanda vingi, na bado kuna bandari Tanga, kuna mlima Kilimanjaro, kuna madini Tanzanite. Hivi ni vitu vichochezi vya kiuchumi tayari (factors for economy). Kwa vyovyote vile uwepo wa mambo haya una athari za moja kwa moja katika uchumi. Uangalie hiyo mikoa kuna vyuo vikuu na taasisi za serikali kiasi gani pia. Na mwisho ulinganishe na maeneo mengine, je kuna ulinganifu? Ishu ni hapana. Tulienda shule kusoma na kupata ufahamu wa mambo na si kutembea. Hapa hatuongei tu mtizamo was sehemu fulani ama kajisababu kamoja fulani hivi, maendeleo ni suala pana sana na linahusisha ujumla wa mambo mengi pia. Jiulize kama leo si gesi pale Mtwara na Lundi ile mikoa unaionaje ilivyokuwa? bado huoni maana ya visababishi vya uchumi? unaweza ukatoa picha ya Dodoma miaka 10 iliyopita, unaijua? hebu iangalie sahivi, ni Dodoma ile ile? je unadhani ni kwa bahati mbaya vimeibuka tu ghafla? kwa vyovyote vile ni muhimu tukaiangalie nchi kwa ujumla wake na kureason kama golden people badala ya kuwaza kama ma irony wapiga kelele na washangiliaji.
 
Wasukuma hao, hawakuhesabiwa Mwanza, utajiri wao wa mifugo, umeneemesha maeneo waliokuwepo wakati wa sensa kwani walihesabu waliokuepo eneo husika tuu. Ila hata ombaomba wa Dodoma, waliotapakaa Tanzania nzima hawakuhesabiwa Dodoma hivyo kupunguza hesabu za umasikini wa Dodoma na kuiongeza hesabu ya umasikini kule walikokuwepo. Idadi kubwa ya masikini wa kutupwa Mwanza, sio Wasukuma bali makabila madogo madogo na watu wa kuja. Wasukuma wenyewe ni matajiri wakubwa wa roho, hata wakilala njaa ni kusmile na kuimba usiku kucha. Kama ilivyo kwa wenyeji wa Darisalama ni Wazaramo, ni masikini kutupwa, ila utajiri wa Darisalama unachangiwa na watu wa kuja, hivyo kuufuta umasikini wa Wazaramo, hivyo kuna sehemu watu wa kuja ndio wanaoboost profile ya mkoa na kuinyanyua na kuna maeneo hao wakuja ndio wanaodidimiza profile ya mkoa
Pasco
Ninavyofahamu mimi wakuja mara nyingi kama ulivyodokeza ndio wanaoboost eneo waliloloea lakini wewe unasema kwa baadhi ya maeneo wakuja wanadidimiza maendeleo,hivi hizi allegations zako zina ithibati?waweza thibitisha hayo? mimi nadhani wageni ndio huleta maendeleo ya eneo,mengine huwa ni chuki tu za wenyeji kuona inakuwaje huyu wakuja anapata maendeleo hapa kwetu ilihali yeye ni wakuja tu,hapo sasa ndio huanza lawama za kuzua na uongo mwingine ili wageni waonekane wabaya.Chunguza utabaini.
 
Serikali ili kuzuia mijadala kama hii ili muda tutumie kwa mambo mengine; basi isiwe inahangaika kutafuta takwimu... iende tu Bungeni na Waziri husika amwage nondo:

"Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa unaotisha kwa umaskini nchi hii ni Lindi! Yaani kule Mheshimiwa Spika, watu kushinda njaa cku mbili au tatu ni jambo la kawaida! Maji wanakunywa ya kwenye madimbwi-- Wakilima Korosho wanaishia kukaanga na kuzitafuna wenyewe! Wanalima ufuta wanaishia kuutengeneza mafuta ya kupakaa! Minazi inaishia kuporomosha madafu! Wakivua samaki wanaishia kuwachemsha supu na ndio maana hata Dar es salaam nazi na samaki adimu sana siku hizi!

Baada ya Lindi Mheshimiwa Spika mkoa unaofuatia kwa karibu kunuka umaskini ni Mtwara! Hawa Wamachinga sijui wana akili gani cjui! Yaani hawa wakiuza korosho na ufuta pesa wanaenda kununua mitego ya panya! Wakivua samaki; wanaenda kutegea panya matokeo yake Mkoa wa Mtwara ni umaskini wa kutisha kila mahali!

Ukitoka Mtwara nenda mkoa wa Pwani! Hali inasikitisha Mheshimiwa Spika! Yaani watu wa mkoa wa Pwani wameshindwa kabisa kutumia fursa za kuwa karibu na Jiji la Dar es salaam... wao ni kupiga msuli kwenda kupiga soga kwenye vijiwe vya Kahama!

Tanga nako Mheshimiwa Spika, cjui Mungu awape nini! Hawa nao wenzao wanajisifia kufanya kazi hawa wanajisifia kuyajua mapenzi! Matokeo yake hakuna lolote la maana zaidi ya kuvaa misuli na vibarakashia na kwenda kwenye vijiwe vya kahawa! Inasikitisha sana Mheshimiwa Spika!

Nafasi ya tano Mheshimiwa Spika ktk kuzama kwenye lindi refu la umaskini inachukuliwa na Dodoma! Sijui tuwafanyie nini hawa watu! Tumewaletea Makao Makuu ya Nchi! Tumewaletea Makao Makuu ya Chama na pia tumewaletea chuo kikubwa kabisa kupita chochote kile nchini lakini haisaidii... wao na kuomba omba kuomba omba na wao!

Hiyo ndo mikoa 5 Mheshimiwa Spika inayonuka kwa umaskini nchi hii na bila shaka Afrika Mashariki yote! Mikoa mingine yote iliyobaki; wao mambo dole!

Natoa hoja!"

Hizo ndo habari tunazotaka kuzisikia Dr. Mpango... we jamaa wa wapi wewe?! Ungetoa hotuba kama hiyo hapo juu huu mjadala wala usingekuwapo na kama ungekuwapo basi ungekuwa ni wa kukashifu vibarakashia!
 
Hivi majuzi wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti Bungeni Waziri wa Fedha alitaja Mikoa mitano inayoongoza kwa Umaskini, ambayo wananchi wake ni Maskini kiasi wanashindwa hata mlo wa siku. Aliitaja Mikoa hiyo na akatoa na asilimia kuwa ni; Kigoma (48.9), Geita (43.7), Kagera (39.3), Singida (38.2), na Mwanza (35.3)

Swali langu la msingi hapa ni njia gani ya kitakwimu iliyotumika kufanya research hii mpaka kutupa majibu kama haya? Je ni kweli Mwanza ni maskini kiasi cha kuwa chini ya mstari wa Dodoma na Katavi? Utafiti huu umefanyika maeneo gani ya Mikoa hii?

Mara kwa mara tunaona taarifa zikiripotiwa wananchi wa Dodoma wanakufa njaa na wengine kujinusuru kwa kula Mizizi na udongo, au hii Dodoma tunayoisikia ni ya Sudan Kusini?! Au la takwimu hizi ni za mwaka gani?

Msaada wa ufafanuzi tafadhali, ni njia gani za kitafiti zilizotupa takwimu hizi?
(Nimechukua Dodoma na Katavi kama mfano tu)
Kumbe wewe hujui? Tukishaweka takwimu za aina hiyo, sasa tumepata kisingizio cha kuwapa umuhimu wananchi wa mikoa hiyo ktk bajeti ili kupunguza 'umaskini'.

Sasa usiulize kwa nini tunapeleka miradi mingi ktk mikoa hiyo.
 
Mwanza imeshikiliwa na wachaga wachache waliovamia,serikali iangalie wazawa tupewe fursa!
Kila kiwanja kizuri,jumba na eneo la niashara utaskia Kessy,Mushi,Massawe,Manka,Munisi,Ndewawio ,Assenga ndo wamiliki
Hao Wachaga hivyo viwanja vizuri wanapewa bure na serikali; au?! Ikiwa mnaviona vizuri ni kwanini msivinunue na nyinyi?! Acha hizo habari bhana!
 
Serikali ili kuzuia mijadala kama hii ili muda tutumie kwa mambo mengine; basi isiwe inahangaika kutafuta takwimu... iende tu Bungeni na Waziri husika amwage nondo:

"Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa unaotisha kwa umaskini nchi hii ni Lindi! Yaani kule Mheshimiwa Spika, watu kushinda njaa cku mbili au tatu ni jambo la kawaida! Maji wanakunywa ya kwenye madimbwi-- Wakilima Korosho wanaishia kukaanga na kuzitafuna wenyewe! Wanalima ufuta wanaishia kuutengeneza mafuta ya kupakaa! Minazi inaishia kuporomosha madafu! Wakivua samaki wanaishia kuwachemsha supu na ndio maana hata Dar es salaam nazi na samaki adimu sana siku hizi!

Baada ya Lindi Mheshimiwa Spika mkoa unaofuatia kwa karibu kunuka umaskini ni Mtwara! Hawa Wamachinga sijui wana akili gani cjui! Yaani hawa wakiuza korosho na ufuta pesa wanaenda kununua mitego ya panya! Wakivua samaki; wanaenda kutegea panya matokeo yake Mkoa wa Mtwara ni umaskini wa kutisha kila mahali!

Ukitoka Mtwara nenda mkoa wa Pwani! Hali inasikitisha Mheshimiwa Spika! Yaani watu wa mkoa wa Pwani wameshindwa kabisa kutumia fursa za kuwa karibu na Jiji la Dar es salaam... wao ni kupiga msuli kwenda kupiga soga kwenye vijiwe vya Kahama!

Tanga nako Mheshimiwa Spika, cjui Mungu awape nini! Hawa nao wenzao wanajisifia kufanya kazi hawa wanajisifia kuyajua mapenzi! Matokeo yake hakuna lolote la maana zaidi ya kuvaa misuli na vibarakashia na kwenda kwenye vijiwe vya kahawa! Inasikitisha sana Mheshimiwa Spika!

Nafasi ya tano Mheshimiwa Spika ktk kuzama kwenye lindi refu la umaskini inachukuliwa na Dodoma! Sijui tuwafanyie nini hawa watu! Tumewaletea Makao Makuu ya Nchi! Tumewaletea Makao Makuu ya Chama na pia tumewaletea chuo kikubwa kabisa kupita chochote kile nchini lakini haisaidii... wao na kuomba omba kuomba omba na wao!

Hiyo ndo mikoa 5 Mheshimiwa Spika inayonuka kwa umaskini nchi hii na bila shaka Afrika Mashariki yote! Mikoa mingine yote iliyobaki; wao mambo dole!

Natoa hoja!"

Hizo ndo habari tunazotaka kuzisikia Dr. Mpango... we jamaa wa wapi wewe?! Ungetoa hotuba kama hiyo hapo juu huu mjadala wala usingekuwapo na kama ungekuwapo basi ungekuwa ni wa kukashifu vibarakashia!
Ha hahahah hahahahahah
 
Hizo ni takwimu za kiuchumi,wamefanya household economic survey,lakini pia wametumia GDP ya mwanza divide by population size,etc.Hata kwa macho huo ni ukweli angalia idadi ya watu wenye makazi bora lakini ukiacha jiji la mwanza,wilaya zake zote ziko hoi hakuna shughuli yeyote ya maana inawapa watu vipato vya maana
 
ni halali kabisa mwanza kuwa maskini. ilivyogawanywa imekuwa na eneo la ardhi 9000km skweya. imeizidi dar tu. katika hako kaardhi kuna wakulima laki sita!? watazalisha nini kama siyo uganga njaa.wasukuma njoeni Ruvuma tulime mbaazi. acheni kubanana hapo.
 
Kwanza naomba ku declare interest, mimi ni chapa ng'ombe!.

Hili ni swali la msingi sana!. Mwanza ndio mkoa unaoongoza kwa utajiri Tanzania ila pia ni mmoja ya mikoa yenye watu wengi sana Tanzania!. Wasukuma ndilo kabila kuu Tanzania linaloongoza kwa idadi ya watu, ambao wamesambaa katika mikoo 5 ya Mwanza, Shinyanga, Shimiyu, Katavi, na Geita.

Miongoni wa wakazi wa Mwanza, pia ndani yake kuna makabila masikini wa kutupwa kama Wanzinza, Wakerewe, Wakara, Wanyamtunzu, hivyo kitakwimu kutoka na wingi wa idadi ya masikini wote wa Mwanza ni wengi kuliko masikini wote wa Singida na Dodoma put together!. Tofauti ya masikini wa Mwanza ni baadhi tuu, lakini Singida na Dodoma wote ni masikini!.

Pasco
 
Kama wachumi wametumia wastani wa kipato inaweza kuwa.kweli ! Mfano mkoa wa Mwanza kwa sasa wakulima uchumi umedidimia sana,hakuna maxao ya uhakika ta biashara,mimi majuzi nilikywa Kwimba na Misungwi,vijijini hali si nzuri,hata hao ng"ombe wanaisemwa ni wachache sana,ardhi ya kilimo haipo/mbaya! I

Labda wachumi watuambie he njia hii ya kuangalia kipato cha wastsni inasaidia kweli kubainisha hali ya mtu mmoja 1?!, Lakini kwa nyanja Zingine kama afya mkoa wa Mwanza upo byuma sanaaaa! Kuna zahanati haxina vyoo toka uhuru!Nitarudi kujadili Kagera na Singida
hizo sababu zipo nchi nzima, so kwanini mpike data kwa ajili ya mwanza?
 
Wasiwasi uko wapi. Sidhani kama wizara inaweza kuwasingizia watu Umasikini. Hata hivyo takwimu hubadilika kila mwaka baada ya utafiti kufanywa na Wizara ya Fedha na Uchumi. Kwa mfano Singida imebaki kwenye top 3 ya mikoa masikini kwa miaka 10 mfululizo. Mwanza imeingia kwenye top 5 kwa mara ya kwanza mwaka huu kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Dodoma haijawahi kuingia kwenye top 5 kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Takwimu hizi hutolewa kila mwaka na Wizara ya Fedha na Uchumi. Vigezo vinavyotumiwa ni pamoja na Wastani wa pato Kimkoa, Uwezo wa kujikimu kwa chakula, Uwezo wa wananchi kugharamia huduma za jamii nk.
 
Hamna kitu hapa ni upuuzi wa siasa. Nani hajui hiyo mikoa ilivyojaa Neema? Pelekeni hela wakazichukue wajanja.
 
Back
Top Bottom