Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Hivi majuzi wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti Bungeni Waziri wa Fedha alitaja Mikoa mitano inayoongoza kwa Umaskini, ambayo wananchi wake ni Maskini kiasi wanashindwa hata mlo wa siku. Aliitaja Mikoa hiyo na akatoa na asilimia kuwa ni; Kigoma (48.9), Geita (43.7), Kagera (39.3), Singida (38.2), na Mwanza (35.3)
Swali langu la msingi hapa ni njia gani ya kitakwimu iliyotumika kufanya research hii mpaka kutupa majibu kama haya? Je ni kweli Mwanza ni maskini kiasi cha kuwa chini ya mstari wa Dodoma na Katavi? Utafiti huu umefanyika maeneo gani ya Mikoa hii?
Mara kwa mara tunaona taarifa zikiripotiwa wananchi wa Dodoma wanakufa njaa na wengine kujinusuru kwa kula Mizizi na udongo, au hii Dodoma tunayoisikia ni ya Sudan Kusini?! Au la takwimu hizi ni za mwaka gani?
Msaada wa ufafanuzi tafadhali, ni njia gani za kitafiti zilizotupa takwimu hizi?
(Nimechukua Dodoma na Katavi kama mfano tu)