Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
Mkuu Dada yangu , kwanza pole, maana mimi ni mzoefu humu hivyo najua jinsi waabudu wanavyoumia kila waabudiwa wanapokosolewa humu jf, haswa kwa kuzingatia baadhi ya waabudiwa wanahesabiwa kuwa wao ni malaika!, hivyo ukiyaleta tuu madudu yao humu, waumini wao huumia sana!.Wewe ni kati ya watu ninaowaheshimu kwa michango yao hapa JF, Hivyo ninatarajia mtu kama wewe kusoma na kuelewa ni kitu gani mtu alichokiandika na anamaanisha nini..Tujifunze kuangalia mambo kwa mapana si kwa maono finyu, tusifungwe na mfn wa Dr.Slaa tukaacha mfn wa Shibuda na kwa mtu kama wewe nategemea kuangalia pande zote mbili na kuja na hoja mhafaka.
By the way kadi mbili au tatu si hoja,kadi haiyashirii mapenzi yako kwa chama, kadi ni karatasi tu, kinachoashiria mapenzi yako kwa chama ni matendo yako, kufuata itikadi za chama chako na nk.
Sasa nikuulize swali kwa matendo na mienendo ya Dr. Slaa je ni CCM au ni Chadema? na kwa matendo na mienendo ya Shibuda (kabla hajaama) alikuwa ni CCM au ni Chadema?
Niliisha wahi sema humu, Shibuda was just a barking dog, seldom bite!, hizo kelele zake ni harmless kwa Chadema kuliko silent killers walio inside Chadema, nyinyi mkiwadhania ndio wazalendo wa kweli!. Ingekuwa system wanatoa majina ya walio katika payroll yao, kuna watu humu wasingelikuwa na mahali pa kuzificha sura zao.
Kwa taarifa yako, huu uchaguzi wa 2015, wengi mnauzungumzia leo, mimi nimeuzungumzia tangu 2010!, na mwaka 2011, nilikutana na Dr. Slaa mahali just by chance tuu, akiwa na 'would be 1st lady!', na tulizungumzia kwa kina ugombea wake 2015, ila kwa vile ni informal talk, siwezi kuweka hapa contents za mazungumzo hayo, ila najua mengi kuhusu viongozi wenu kuliko hata baadhi yenu mnavyojua!.
Uzalendo wa kweli haupimwi kwa maneno wala matendo bali dhamira!.
Pasco