Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?


JEMBE NA NYUNDO,
KILIMO KWANZA...MAPINDUZI YA KIJANI
UHUISHAJI WA VIWANDA VILIVYOBINAFSISHWA...itafatia

Loh!
 
tatizo lako huan akili.............umeshachakachua maaada na kutuchfulia hali ya hewa lione kwanza wanazungumzia CCM umeleta habari zingiiine
 

Mkuu usiende nje ya mada,
Kilichopo sio vyama bali naitafiti neno 'mapinduzi' kutumiwa na chama tawala kwa zaidi ya miongo 3, siongelei ubora/uzuri/ubaya wa vyama vya siasa...LA HASHA!
 
Swali lina fanana nini maana ya Chadema je kuna demokrasia?

Mlengo wa kati swali halijibiwi kwa swali maana naona kiswahili si kigumu hivyo. Jibu ya ccm halafu kama una swali la chadem uliza but dont mix things
 

Nilitarajia ujibu swali kwanza kabla ya ku-raise topic nyingine
 
Waberoya, ahsante. Lakini bado hatujajua kwa nini 'chama cha mapinduzi'. Kilipindua nini? ASP na TANU si viliungana ndio kikazaliwa? Kuna wenye umri ambao watatusaidia.

Kwa wakati huo, neno mapinduzi lilikuwa pia ni tafsiri ya neno REVOLUTION na si kupindua tu (coup de etat). Kwa hiyo chama kilikuwa Revolutionary Party ambacho ukitafsiri kwa kiswahili kinakuwa chama cha mapinduzi.
 
Guys, I just told you so..... hawatajibu hoja, hawana uwezo huo na hawajazoea

Chama Cha Mapinduzi ni jina tu la chama kama ilivyo kwa CCDM (Chama Cha Demokrasia na Maendeleo), NCCR-Mageuzi, CUF,TLP, UDP etc. sasa ukitaka kufahamu maana ya kila jina la chama ina depend na mtu mwenyewe. au mtoa mada angetuambia tafsiri ya chama chake Chadema maana yake ni nini then aulize maana ya vyama vingine. Afterall, Dr WS alikua kada mzuri tu wa CCM hata Nyerere akampa udiwani wakati ule bado akiwa padre, hivyo anajua maana halisi ya CCM. So I see no point ya kupoteza muda kutafsiri acronyms za majina ya vyama vyote vilivyopo hapa nchini lets judge them by their deeds!
 
Jibu ni rahisi tu, wakati wa vuguvugu la muungano kulifanyika makubaliano ambayo ndio yalileta muungano wetu.
Moja ya kikwazo kikubwa ni kwa wazanzibar kuogopa sana kumezwa na tanganyika kwa maana ya ukubwa wa eneo na idadi ya watu, pia kuyaenzi mapinduzi yao hii ilipelekea kutaka serikali yao ya mapinduzi iwepo na chama chao kwakuwa kinaungana na tanu basi lazima neno mapinduzi liwepo ktk chama kipya ili kuenzi mapinduzi ya chama chao, hapo ndipo neno mapinduzi likaingizwa na kuwa ccm.
Hayo ndio waasisi wa muungano walikubaliana na kupelekea huu mungano wetu, usiniulize mbona tanu na tanganyika sijui nini?aah a,nimekupa sababu mengineyo nyerere na karume ndio wangeweza kujibu
 
Acheni blablah. Ina nyie wote hamkuwahi wanachama wa CCM kabla ya mwaka 1990?
Neno mapinduzi kwenye hicho chama lina maana ya revolution. Halina maana ya kupinduapindua serikali. Mwisho mtasema na ugonjwa wa kipindupindu unahusiana na kupindua.

The Chama cha Mapinduzi (Party of the Revolution in Swahili) is the ruling political party of Tanzania.

Soma hapa:
Chama cha Mapinduzi - Wikipedia, the free encyclopedia
Political party flags in Tanzania
Revolutionary Party of Tanzania (political party, Tanzania) -- Britannica Online Encyclopedia
 

Mkuu, HESHIMA KWAKO.
sijajiongelea mimi ni mfuasi wa chama gani, tatizo lisiwe pale mtanzania anapohoji mambo muhimu na ya msingi basi atafsiriwe kwa itikadi ya chama anachoegemea. Naomba urejee thread yangu, nahitaji kutoa ukungu ili nitambue maana halisi ama uwakilishi wa mtanganyika katika alama za chama tawala tangu enzi hizoooooo.
Nisaidie na tubaki kwenye mada hii.
 
Naomba urejee thread yangu, nahitaji kutoa ukungu ili nitambue maana halisi ama uwakilishi wa mtanganyika katika alama za chama tawala tangu enzi hizoooooo.
Nisaidie na tubaki kwenye mada hii.

Mkuu nimekupa sababu ya kuingiza mapinduzi ktk chama lakini sasa naona unataka na uwakilishi wa tanganyika ktk hili, hapo sasa unakwenda ktk kero za muungano ambazo ni tata na nyingi mno.
Sidhani neno mapinduzi kama ni tatitizo its only a name it doesnt effect anything, unless unamatatizo na muungano kwa mambo mengine ya msingi hapo ntakubaliana na wewe
 

Nimekusoma, ahsante.
 

Ahsante kwa hizo links mkuu,
 

...Chama Cha Mafisadi befits them!
 
Ccm wamechoka kufikiri walichobaki sasa ni kuwaibia tu watz kukiwa mchana kweupe na wezi tunawafahamu wote na wala hatuwachukulii hatua yoyote wanatamba hii ndiyo alama halisi ya ccm na mapinduzi yake..........wametupindua watz hatuiwezi hata kudai haki zetu
 
Haaa! wewe ni Mwiba au nimekosea? na kama kweli wewe ni mwiba basi nimefurahi sana kupita maelezo.
Mara nyingi tunawahubiria sana watu humu jamvini kuwa ccm ni maafa na haifai hata kwa bure.
kama wewe mwiba ushaona hilo,basi hata jeykey,topical,maralia sugu nk. nao watakubaliana na sisi tu oneday
 

Samahani Mpevu kama nimeenda nje ya mada na thanx kwa kunirekebisha and tuko pamoja.
 
jibu hoja kijana,
acha kuruka ruka kama jogoo,
hili ni jukwaa la great thinkers


Mlengo wa Kati
Join Date : 16th February 2011
Posts : 42
Thanks4Thanked 6 Times in 5 Posts

Rep Power : 0

 
Mwiba alishabadirika, tena siku hizi amekuwa mstari wa kwanza wa kuyaanika madudu ya CCM
Inaonyesha wazi kabisa kuwa watu wengi walikuwa hawajui CDM wanafanya nini na wako kwa ajiri ya nani?
 
Naomba ufafanuzi juu ya hili jambo manake jina la chama mara nyingi kama si zote huwa ni kama kifupisho cha lengo na madhumuni yake. Sasa hiki chama cha mapinduzi kwetu MAPINDUZI maana yake nini sitaki kuamini kuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar ndio yanayozungumziwa hapo. Tell me Greatthinkers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…