Swala ya Idd Msikiti wa Gaddafi

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Swala ya Idd Kitaifa inatarajiwa kufanyika Msikiti wa Gaddafi Dodoma huku JK akiwa mgeni rasmi. Hii inafanyika wakati kiongozi huyo wa Libya akiendelea kusakwa na majeshi ya waasi wa Libya.
 
Swala ya Idd Kitaifa inatarajiwa kufanyika Msikiti wa Gaddafi Dodoma huku JK akiwa mgeni rasmi. Hii inafanyika wakati kiongozi huyo wa Libya akiendelea kusakwa na majeshi ya waasi wa Libya.
Sijakuelewa kwenye thread yako unataka tujifunze nini. au tuchangie kitu gani. Na zaidi sioni tija ya thread yako kwa taifa letu. Can you come again with some tangible ideas.
 
Sijakuelewa kwenye thread yako unataka tujifunze nini. au tuchangie kitu gani. Na zaidi sioni tija ya thread yako kwa taifa letu. Can you come again with some tangible ideas.

If you have those tangible ideas be the first to share them with us.
 
Huo ni mchakato wa kumuenzi Gaddafi.
Kweli mkuu! Hao ndiyo ndugu zetu...! Huwa wanaenzi kila kitu cha ajabu.. Kama Osama bin Laden, Sadam Hussein, Idd Amiin n.k wote wanaenziwa mpaka leo itakuwaje kwa huyu aliyewajengea booonge la msikiti! hii kitu inafaa kwenye jukwaa la dini siyo hapa!
 
Kila kilicho kizuri tanzania kimejengwa kwa msaada wa nchi fulani au mtu fulan so haina maana kisitumia kisa tunaiezi hiyo nchi au mtu,kwa watanzania na waafrica Gadaf ametusaidia kwa kiasi kikubwa.bado huna haki ya kumchukia gadaf while aliwafanyia kila kitu ktk nchi yake,jiulize unasheherekea miaka 50 ya uhuru unakitu unachokipata bure kutoka serikali yako?kwa waafrica gadaf is hero kataa au kubali but he is hero,hayo mengine yanawahusu wenye kwa kukubali kuibiwa raslimal zao na wazungu
 
Sintashangaa kusikia wameanzisha Osama Day.
 
huyu ceremonial presdent anachekesha kweli nimemfuatilia karibu mwaka mzima kila ukimwona yupo kwenye sherehe.
haya bwana maisha bora.
 
Wanataka kutuingiza kwenye mgogoro na nchi za magharibi, kwanza kuna tetesi tanzania imempa hifadhi gadafi, na mambo yanavyoendelea inawezekana ikawa kweli
 
Hayanihusu haya! Nakumbuka mwaka jana waligombania sadaka pale msikitini dodoma!
 
Je n'ai jamais perdu mon calories se disputer avec un Paillasse parce que les gens à distance ne pourront pas dire qui est qui
Dah, siku hizi nimeisahau lugha hii any way naikumbuka kwa mbali ngoja niwape faida wana jf kidogo:- yaani "akili za magamba zinaweza kufikiri ya mbali kama ya libya lakini yanshindwa kufikiria matatizo ya bongo kama umeme, maji, petrol, disel mafuta ya taa na ufisadi" naddhani nimepatia kidogo.
 
Kila kilicho kizuri tanzania kimejengwa kwa msaada wa nchi fulani au mtu fulan so haina maana kisitumia kisa tunaiezi hiyo nchi au mtu,kwa watanzania na waafrica Gadaf ametusaidia kwa kiasi kikubwa.bado huna haki ya kumchukia gadaf while aliwafanyia kila kitu ktk nchi yake,jiulize unasheherekea miaka 50 ya uhuru unakitu unachokipata bure kutoka serikali yako?kwa waafrica gadaf is hero kataa au kubali but he is hero,hayo mengine yanawahusu wenye kwa kukubali kuibiwa raslimal zao na wazungu

Hela ni shetani! Gadaffi hawezi kuwa mtu wa maana hata chembe kwa Tanzania wala Africa. He is a symbol of a modern day dictactor who would buy his way out to be 'loved'. Watanzania tunatakiwa tule samaki kwa wingi ili tusipoteze kumbukumbu ya mambo aliyotufanyia huyu bwana. Gadaffi aliuungana na Idd Amin kutushambulia na alitumia hela za mafuta kununua makombora na kutuma Kagera! Na kwa miaka yote hiyo hakuna mahali popote huyu Gadaffi amesikika ku-regret au kuwaomba samahani watanzania for his cowardness actions.

Kama kweli Rais Kikwete ameenda kuswali kwenye msikiti wa Gadaffi niseme it is clearly an error of judgement on his part. Ni afadhali angekaa kimya kama alivyofanya wakati wa mgomo wa mafuta. NTC ni kama wameshachukua nchi so he needs to get used to that. Na hapa the choice he needs to make, on behalf of the people of Tanzania is either to stand with the people of Libya or remain on the side of a dictactor. Na nahisi kuna aibu inatunyemelea maana Kikwete is not his own man.! Sasa hivi anaonekana kufuata masharti ya Jacob Zuma na Mugabe, lakini kesho Hillary Clinton akimpa masharti atageuka jiwe kama alivyofanya kwa barabara ya Serengeti. Na ataaimbiwa achague kuwa na tafiki yake au vyandarua vya mbu! Tukae mkao wa aibu.Inakuja!

Kwetu watanzania rafiki wa kweli ni yule anaukujali wakati wa shida. Tulikuwa tumevamiwa na Idd Amin lakini Gadafi aliamua kuungana na adui yetu kutuangamiza. Leo hii kuna watu wanamtukuza kwa sababu ya hela? bloody money.

Once a traitor always a traitor.
 
Kweli mkuu! Hao ndiyo ndugu zetu...! Huwa wanaenzi kila kitu cha ajabu.. Kama Osama bin Laden, Sadam Hussein, Idd Amiin n.k wote wanaenziwa mpaka leo itakuwaje kwa huyu aliyewajengea booonge la msikiti! hii kitu inafaa kwenye jukwaa la dini siyo hapa!

Kwani hilo jina la msikiti lilikuwepo au wamelianzisha ili kumuenz Gaddaf. Acha ushabiki wa kijinga.
 
Swala ya Idd Kitaifa inatarajiwa kufanyika Msikiti wa Gaddafi Dodoma huku JK akiwa mgeni rasmi. Hii inafanyika wakati kiongozi huyo wa Libya akiendelea kusakwa na majeshi ya waasi wa Libya.

so what? haina kichwa wala miguu eti na wewe thread. Mod hebu tulia hii kitu kunakofaa haifai kuwa kwenye hili jukwaa bana
 
Labda hujafahamu kwamba bado kuna wapuuzi kama huyo Mwita 25 wanaodhani kwamba kiingereza ni usomi, hawa ni washamba waliosalia katika karne ya leo. najisikia furaha sana ninapotumia lugha ya kiswahili licha ya kwamba nina uwezo wa kuongea lugha 3 za kimataifa.

I never waste my calories arguing with a merry-andrew because folks at distance will fail to tell who is who

Non ho mai sprecare il mio calorie litigare con un allegro-andrew, perché la gente a distanza non riuscirà a dire chi è chi
Mimi kinapanda kiswahili tuu, hivyo mmenipa kazi ya kuomba mtu anitafsirie
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom