Swala la Watanzania kuto kuunganisha Mitaji yao ni sawa na Kujichimbia Kaburi la Biashara

sio kweli kwamba watanzania hawana elimu ya biashara.
Na sio kweli kuwa ni watanzania tuu ndio sio waaminifu.

Mkumbuke kwenye biashara kuna Partnership deed ina sura ya kisheria kuainisha na kulinda maslahi ya pande zote mili , na kama ni kampuni kuna Memorandom na bodi pia legally binded.Hakuna kudhulumiana hapo.

Tatizokubwa linatokea kama mmeungana kienyejienyeji, kirafikirafiki au kiunduguundugu bila kuhusisha mambo ya kisheria (gawiwo, liabilities, decision making, records keeping, asserts etc).

Tanzania kumejaa sana bureucrcy hasa kama ni mzawa unavisent vyako unataka kuanzisha kampuni Utakutana na vikwanzo vingi, majungu na kuombwa rushwa mpaka ukome.
 
wakuu huu ni wakati wa vitendo, nilishawahi kujaribu kuunganisha mtaji na wenzangu lakini kosa nililolifanya lilikuwa ni kuomba ushauri kwa watu wangu wa karibu..cha muhimu ni kuchagua mtu mwenye historia nzuri, aliye serious na kazi na mwenye njaa kali ya maendeleo hata kama hana fedha nyingi ya kuwekeza mchukueni tu c'se yeye ni mtaji tosha, mkiona mtu yupo busy sana na shughuli zake nyingine huyo hafai kuungana nae, ... mnatakiwa kufanya vikao vya mara kwa mara mkiwa wote pamoja ili kuepuka maamuzi ya mtu mmoja kwenye shughuli za kikundi

kwa wale wenye interest na kilimo/ufugaji/maliasili etc mliopo mikoani/wilayani kwenu mnaweza kutembelea ofisi za kilimo, maliasili, ufugaji kama kikundi huko kuna fursa nyingi sana na mtasaidiwa tuache kulalama ardhi inauzwa kwa wageni wakati wewe hujui hata ofisi ya kilimo ipo mtaa gani

Mkuu true kabisa, Tunapenda sana kulalamika huku tukiwa tumekaa tu, na kama ulivyo sema tatizo kubwa liko hapo unakuta watu wanachaguana, waote wako bise na mambo yao mengine matokeo yake ni biashara kufa, ni lazima wote wawe na njaa ya mafanikio kama ulivyo sema, hata kama hana pesa,

Na ishu ya Aridhi hapo, Ipo siku tutakuja kilia na kuswaga meno, Hii aridhi tutakuja kuikumbuka sana wakati huo kukiwa hakuna njia tena,
 
Hii mada inafaa kuendelea tena maana najua kuna watu walishajaribu partnership wakaona changamoto zake
Pia kuna watu wana mawazo mapya kuhusu kuunganisha nguvu kwenye mambo ya kibiashara.
 
Wabongo kutoboa tukiwa bado ni vijana wadogo vigumu sana, na hao wanaotoboa katika umri wa kijana wa kati(20-29 yrs old) ni wachache sana. Wengi wanatoboa wakiwa wanaelekea uzeeni(35+yrs old).

Tatizo la vijana wengi ni ubinafsi na ujinga. Mtu anajibania fursa kwa kumbania mwenzake fursa pasipo kujijua. Kuna watu wana access ya kupata financial aids lakini hawajui wafanye nini na kuna wana idea kibao tu lakini hawajui ni wapi waanzie kutokana na kukosa hela.

Kutoshirikiana kwa namna yoyote ile kwa sababu ya aibu na kujikweza upelekea watu kudumaa kiuchumi na wanakuja kushtuka muda umeenda na penyewe ni baada ya kuwa na chaneli nyingi.
 
Ukweli ni kwamba watanzania tuna tatizo la uaminifu kitu kilichosababisha watu tusiaminiane,kwa kawaida mtu usipokuwa muaminifu ni vigumu kumuamini mwenzako.Kuna muheshimiwa mmoja anasema,asilimia themenini ya matatizo ambayo nikikwazo kwa maendeleo yako,yanatokana na wewe mwenyewe,unachotakiwa kufanya ni kujitazama wewe mwenyewe na kubadirika kabla haujaanza kuwaambi wenzako wabadirike.Sidhani katika sisi tuliochangia kama kuna mmoja wetu anahisi na yeye ni sehemu ya tatizo.Mbaya zaidi tumekosa uaminifu karibia kila eneo hatuna uaminifu wa pesa achilia mbali uaminifu wa kazi,siku zote maneno yetu na matendo yetu havifanani.Sasa huu ukosefu wa uaminifu ukiongeza na ubinafsi unaojikita katika mioyo yetu kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya zaidi.Kwa kuwa wakati wa sisi kufunzwa na ulimwengu umewadia,subiri kusikia watu tutakavyokuwa tukilalamika.Shukrani mkuu kwa mada yako nzuri
Point, hata nami ni case study kwa hili
 
Very nice, Hawa jamaa walipoteleaga wapi? Enzi hizo kulijuwa na Mijadala ya kiutu uzima
 
mimi nathani waafrica ndio tulivyo. Tunapenda kuona mahela yakiwa benki mengi badala ya kuwa kwenye mzunguko. Bill gates ni billionaire but nina uhakika account yake haina hata 500 M dollars versus wenzetu hapa wameweka uswizi huko.
 
Huu uzi umenifunza jambo, ngoja nitafute vijana wenzangu tuunganishe mtaji tufanye biashara.
Inatakiwa twende kama marathon sio short race.
Fanya mkweli mkuu chukua hatua, yaani kama una rafiki yako ambae yeye kupata funding support sio inshu, mkalishe chini mfanye nae maendeleo.
 
Sawa sawa mkuu
Nitaletavmrejesho hapa nikifanikiwa kuwapata watu wa kuunganisha nao nguvu ya mtaji.
 
afu majuzi nimemuona felix mosha kwenye tv na yule babu wa iringa kidogo niwachomoe kwenye tv. Wakati nicol inakuja niligoma katu katu kununua shares nikamuambia finance director simuamini mswahili. Na serikali imekaa kimya tu! Zile ndoto alizokuwa anaongelea sijui ziko wapi. Tuunganishe mtaji at family level, basi!
Family level yenyewe tunashindana Nani atakuwa Na uwezo kushinda mwenzake
 
Back
Top Bottom