Swala la Watanzania kuto kuunganisha Mitaji yao ni sawa na Kujichimbia Kaburi la Biashara

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
Niliwahi kuleta Mara Mbili humu Janvini swala la watu kuunganisha Mitaji, hakuna aliye jari, watu wanataka kila mmoja aonekane kwamba anaweza, kila mtu anataka aonekane kwa Ndugu, jamaa, marafiki, majirani na kazalika kwamba ana biashara yake yeye pekee, hii ni hatari sana huko Tuendako,

Raisi Msatafu Mkapa aliwahi kuongelea hili swala katika Moja ya Hotuba zake, kwamba Watanzania bila kuunganisha Mitaji watabakia kulalamika kwamba wanatengwa na tenda na Miradi mikubwa wanapewa Wazungu, Ni kweli hata ukija kwenye swala la MIGODI pamoja na kwamba hawa GGM na wakina Barick ni wahuni lakini Ukweli ni kwamba Hizi Kampuni zina Mitaji Mikubwa kabisa na ni Makampuni makubwa kabisa hapa Dunini,

Mfano:
Kwa Arusha nimetonywa kwamba ile Kampuni kubwa kabisa ya Biashara za Kuku kenya wanataka kusimika Mitambo yao Arusha ili kuteka soko la Tanzania na tiyali wamenunua eneo la hekta 40, hii ni habari mbaya sana kwa watanzania, hawa wakenya wana Mitambo ya kutotoresha Vifaranga 500,000 kila wiki, na wanauza vifaranga, kuku na mayai katika bei ya chini kabisa,

Hii ni habari za kutisha kwa biashara zetu hapa Bongo, mimi binafisi napenda waje ili watuamushe, watanzania tunapenda sana Individuality

Hapa Bila watanzania Kuunganisha Mitaji, hakika tutafunga biashara nyingi sana, ni swala la Muda tu wakuu,

Hapa hata wakina Interchick wanaweza wasiweze kufurukuta, achulia mbali individual ambao kila mtu anafuga kuku wa mayai na nyama,

Bila kuunganisha Mitaji, hakika tutafunga biashara muda siu mrefu, naomba tusiandikie Mate tusubiri kujionea wenyewe

SWALA LA DALADALA ZA DAR

- Juzi nilisikia SUMATRA wanasitisha kutoa leseni kwa mmiliki mmoj mmoja, hii mimi nimeipenda sana, haiwezakani Dar iwe na watoa huduma za Usafiri zaidi ya elfu 10 wakati Mjaiji makubw akabisa Duniani yana watoa duma wasiozidi 10 tu

- Hapa napo ninauhakika zikipatikana kampuni mbili tu zenye mitaji ya uhakika, zile Costa, na Haice, zitabadilishwa kuwa za kubeba mizigo, na hii yote ni kwa sababu Watanzania hawataki kabisa kubadilika kuendana na DUNIA, haiwezekani kila mtu awe na Daladala yake,

SWALA LA MAKAMPUNI YA UJENZI

- Hawa nao mpka wanaombwa na Serikali waunganishe Makampuni yao hawataki, na kwa sasa Makampuni mengi ya Kibongo yanaishia kupata tenda za kutengeneza Barabara za Vijijiji na za Mitaa, HAKUNA KAMPUNI YA NDANI HATA MOJA INAWEZA SHINDANA NA KAMPUNI KAMA SOGEA SATOM, ya Ufaransa inayo jenga Barabara ya Arusha Minjingu, au Kuna Kampuni ya kushindana na STRABAG? jibu ni hakuna,

Ila kampuni za Kibongo zingeweza Kuunganisha Mitaji wangeweza hata kupambana na hizi Kampuni,
 
englibertm

JF-Expert Member
May 1, 2009
9,256
2,000
naogopa kuunganisha mtaji kwasababu ya yaliotokea baada yakuunganisha mtaji kupitia NICOL sasa hata siisikiitena lakini wakati ina anza tuliaidiwa mambo mengi.
 
CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
naogopa kuunganisha mtaji kwasababu ya yaliotokea baada yakuunganisha mtaji kupitia NICOL sasa hata siisikiitena lakini wakati ina anza tuliaidiwa mambo mengi.

Mkuu mimi simanishi Aina ile ya NICOL, no hii inamanisha watu wanao fahamiana na wenye biashara zinazo fanana, Mfano wafuga Ng,ombe, Kuku, mbuzi, na Business zingine, Ile ya NICOL ili kuwa na mchanganyiko wa kila aina,

Hata hivyo Risk ipo kila mahali mkuu, na NICOL inaweza tumika kama case study kwa sasa hata ikija ishu kama hiyo lazima kwanza waangalie kilicho fanya NICOL kushindwa. Lengo la NICOL lilikuwa zuri endapo hata ingepata uungaji mkono wa Serikali, kwa sababu walikuwa wanataka kununu Makampuni ya Serikalai yanayo uzwa badala ya kuwauzia wazungu,

Na NICOL ilifanya hivyo baada ya jamaa kugundua hakuna Njia nyingine ya Kushindana na Kampuni kubwa kama za Makaburu zilizo nunua Mabenki na Viwanda vya Bia,

Na Bila hivyo mkuu jiandae kushindana Kufa Na kupona na wawekezaji kutoka Nje wenye Mitaji waliyo kopeswa na Mabenki ya kwao kwa Riba nafuu, na kama hawa Majirani zetu watatukimbiza ile mbaya jamaa wanakuja speed kama Makaburu wa South Vile
 
Lonestriker

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
640
250
Sawa kabisa,kwa kweli Tanzania tunahitaji kujirekebisha kwenye suala la investment.Bila kuzungumzia kampuni za wazungu,naangalia wenzetu wa Kenya wana consolidated holdings nyingi sana kulinganisha na sisi.Ni vigumu kwa sisi kuendelea kwa kutegemea miradi mikubwa yote kuanzishwa na serikali.Yaani hata miradi ya mabasi tunategemea serikali.Kiukweli hatua ya Sumatra ni positive move kwa sababu kampuni kubwa zitaweza kuja na mabasi mengi na kuondoa usumbufu wa kusubiri mabasi kwa muda mrefu...tofauti ya Dar na Nairobi si Traffic jam bali ni muda wa kusubiri dala dala.Wakati sisi tunasubiri mabasi kwa muda mrefu wenzetu wanalalamikia traffic jam pekee. Cha ajabu watanzania tuna amani na kuaminiana kuliko wakenya lakini tunashindwa kuunganisha mitaji ya kufanya biashara kubwa na kuishia kuwa kila mtu kivyake.Binafsi nafikiri ni kwa sababu ya kuaminiana huku ndio maana mara nyingi tunafanya mambo bila kufuata proper legal rules mwishowe wajanja wachache wakituibia tunazidi kuogopa kuunganisha mitaji.Mbona tunaongoza kuchangiana kwenye misiba,harusi na birthday,why can't we extend this to investment ventures and be a force to reckon with in the regional market.We have the smallest private sector in the the region because of capital restrictions.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,455
2,000
Mleta mada umegusia kitu cha msingi sana. Hata Dr. Magufuli amekua akisisitiza wazawa kuunganisha mitaji yao, hasa wale wenye kazi za kufanana km vile wajenzi wa nyumba na miundombinu. Karibu kampuni zote zinazoshinda zabuni za ujenzi wa barabara ni joint ventures (ukiacha za wachina). Kumbuka waliojenga Morogoro road, Skanpihl Colas Jv, Ncc Aarslef Jv etc. Umoja ni nguvu. Natarajia siku moja Nandhra Engineerinng na Skol Engineering wataunganisha nguvu na kushinda tenda ya kujenga barabara ya Kidatu-Ifakara (ni mfano tu).
 
Mkuu ni kweli Kabisa, Hizi Kampuni za Ujenzi za Kutoka Nje ya Nchi hasa Wazungu na Wachina umekuta wameungana na wanamitaji mikubwa sana na Vyomba vya Hali ya Juu, na wakianza kujenga Barabara kila kitu hununu kipya kuanzia Magari, Mitambo na kazalika sasa njoo kwa Watanzania wanavyo unga unga mambo.

Kuna siku nilisikia Mwakyembe akilalamika kwamba Kampuni za Ujenzi wa Barabara za kutoka Tanzania baada ya kuambiwa waunganisje Mitaji/au waungane kampuni mbili, wao hawafanyi hivyo na Badala yake wanafanya hivi
MWENYE KAMPUNI HUENDA BRELA KUSAJILI KAMPUNI YA UJENZI NYINGINE HUSAJILI HATA NNE, NA HUENDA KUOMBA TENDA KWA KIGEZO KWAMBA WAMEUNGANA KUMBE ZOTE NI ZAKE, sas huu ni ujanja ambao huwezi kuwasaidia watanzania,

Kwa ushindani Ulivyo Mgumu kwa sasa Kampuni nyingi sana Dunini huungana ili kuweza kuhimili ushindani lakini kwa Tanzania sijawahi kusikia hilo, Kampuni kama BP zimeungana na kampuni kubwa kabisa ya Nishati ya URUSI Rosneft kununu kampuni ya T.NK , na hii Rosneft kwa sasa ndo kampuni ya pili kwa Mapato Duniani kwa ripoti ya hivi karibuni na imeipiku EXON Mobile ya USA, na hata kampuni za Ndege zinaungana, Mabenki yanaungana

Ukija kwa Tanzania Tatizo liko kwa UMIMI kila mtu anataka awe na chake mwenyewe, so kwa staili hii hatutaweza hata kushindana na Kampuni kutoka Kenya
 
wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
10,651
2,000
nadhan ndo mana wakandaras 13 wazawa wameungana kujenga lile daraja la igunga litakalogharim aproximately bil
12 ka kumbukumb zangu n nzur
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,647
2,000
mkuu mi naona watanzania wana matatizo yafuatayo
1.hawana elimu ya kutosha kuhusu biashara hivyo wanakuwa waoga kwamba wakiunga nguvu basi wenzake walioungana nao watamzidi ujanja.
2.pili watanzania hawako honest. unakuta anakuwa na mashaka kwamba mkiunga nguvu hamtafanikiwa ila hawezi kwambia kwanini hamtafanikiwa sijui anaogopa ataonekana ametoa sababu ya kijinga.kumbe hajui hizo ni challenge mojawapo ya kuunganisha nguvu yaani kutoana mashaka. kuna jamaa zangu niliwaitrodyuzia project ambayo haiitaji hata mtaji tunatumia tu kumpyuta walikuwa excited mno ila hadi leo kazi iko mwishoni nimefanya peke yangu sasa sijui walishindwa kuniambia kwamba project haiwezi kulipa au ni uvivu!?
3.watanzani wakipata hela wanahali ya kujisikia na kuamini kwa vile njia alizotumia zimemsaidia kuwa tajiri basi hakuna njia nyingine nzuri kushinda zake.
4.....................
5...................................
maprofesa wamesoma uchumi kazi yao ni kuandika proposals na kupublish papers wanashindwa kuandika vitabu kama hivi ili kutusaidia. nakushauri mkuu hata kama hujasoma uchumi fanya utafiti na andika kitabu kuhusu hii ishu.
 
KIFARU

Senior Member
Apr 6, 2009
172
0
kiongozi umeongeajambo linalo make sense,ila kwanini usituandikie changamoto zake na jinsi ya kuzikabili?
 
collezione

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
352
250
Sio kama Watanzania hawapendi.
Ndugu yangu, kwa tanzania kuna vitu vitatu. Vinafanya hilo jambo kutowezekana

1) Uaminifu. Watanzania uaminifu ni zero. Mkiunganisha mtaji, unakuta mwenzako anazunguka nyuma, anataka faida zaidi.. Hii mimi imenitokea sana, na ndicho kikwako kikubwa hapa Tanzania.
Hatukulelewa kwenye uvumilivu na uaminifu. Kila mtu anajifanya much know na mjanja zaidi ya mwenzake.

2) Elimu. Bado Hatujui kuendesha shughuli as joint venture. As a result tunaingia kichwa kichwa. Tunaambulia disapointment ya kuzidiana ujanja na kudhulumiana.

3) Mazoea ya kushirikiana. WaTz hatupendi fanya kazi pamoja. Ikitokea Mnafanya lazima mmoja ataona anamfaidisha mwenzake.
 
Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
0
Ukweli ni kwamba watanzania tuna tatizo la uaminifu kitu kilichosababisha watu tusiaminiane,kwa kawaida mtu usipokuwa muaminifu ni vigumu kumuamini mwenzako.Kuna muheshimiwa mmoja anasema,asilimia themenini ya matatizo ambayo nikikwazo kwa maendeleo yako,yanatokana na wewe mwenyewe,unachotakiwa kufanya ni kujitazama wewe mwenyewe na kubadirika kabla haujaanza kuwaambi wenzako wabadirike.Sidhani katika sisi tuliochangia kama kuna mmoja wetu anahisi na yeye ni sehemu ya tatizo.Mbaya zaidi tumekosa uaminifu karibia kila eneo hatuna uaminifu wa pesa achilia mbali uaminifu wa kazi,siku zote maneno yetu na matendo yetu havifanani.Sasa huu ukosefu wa uaminifu ukiongeza na ubinafsi unaojikita katika mioyo yetu kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya zaidi.Kwa kuwa wakati wa sisi kufunzwa na ulimwengu umewadia,subiri kusikia watu tutakavyokuwa tukilalamika.Shukrani mkuu kwa mada yako nzuri
 
CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
nadhan ndo mana wakandaras 13 wazawa wameungana kujenga lile daraja la igunga litakalogharim aproximately bil
12 ka kumbukumb zangu n nzur

Wale walirazimishwa kufanya hivyo na hawajafanya kwa mapenzi yao, na kinacho takiwa ni kuunganisha mitaji na kuja na Kampuni Moja yenye nguvu kabiosa, hii ya kujiunga kisa tenda, leo na kesho wengine utakuta wameisha firisika,
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
naogopa kuunganisha mtaji kwasababu ya yaliotokea baada yakuunganisha mtaji kupitia NICOL sasa hata siisikiitena lakini wakati ina anza tuliaidiwa mambo mengi.
afu majuzi nimemuona felix mosha kwenye tv na yule babu wa iringa kidogo niwachomoe kwenye tv. Wakati nicol inakuja niligoma katu katu kununua shares nikamuambia finance director simuamini mswahili. Na serikali imekaa kimya tu! Zile ndoto alizokuwa anaongelea sijui ziko wapi. Tuunganishe mtaji at family level, basi!
 
CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
Sio kama Watanzania hawapendi.
Ndugu yangu, kwa tanzania kuna vitu vitatu. Vinafanya hilo jambo kutowezekana

1) Uaminifu. Watanzania uaminifu ni zero. Mkiunganisha mtaji, unakuta mwenzako anazunguka nyuma, anataka faida zaidi.. Hii mimi imenitokea sana, na ndicho kikwako kikubwa hapa Tanzania.
Hatukulelewa kwenye uvumilivu na uaminifu. Kila mtu anajifanya much know na mjanja zaidi ya mwenzake.

2) Elimu. Bado Hatujui kuendesha shughuli as joint venture. As a result tunaingia kichwa kichwa. Tunaambulia disapointment ya kuzidiana ujanja na kudhulumiana.

3) Mazoea ya kushirikiana. WaTz hatupendi fanya kazi pamoja. Ikitokea Mnafanya lazima mmoja ataona anamfaidisha mwenzake.

Mkuu hivyo ni visingizio ambavyo havina Ukweli wowote Ule, Uendeshaji wa Kampuni unaujua lakini? sasa watu wameunganisha Mitaji na Kuunda kampuni moja yenye waendeshaji kuanzia Directa mwjiriwa, katibu wa kampuni, na wafanyakazi, huo ujanja utatotokea wapi?

Mara nyingi hii ndo sababu kubwa sana wanayo tumia kuhararisha hili,

2, Elimu- hapa napo si dhani kama ni kweli, kwa sababu Biashara inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu kampuni inakua na taratibu zake nanai signatory nani anafanya nini na mipaka yake ni wapi,

3. Kwenye Mazoe hapo ni kweli kabisa

So mwisho wa haya ni Watu kuja kufunga biashara zao, ni watanzania wachache watakao weza kufurukuta zidi ya Makampuni makubwa, mimi nazania tusubirie tu wakati waja
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
8,051
2,000
na ndo maana vyama vya USHIRIKA vingi hasa SACCOS vinasuasua sana kwa kuwa watz wengi ni wagumu mno kuviongezea MITAJI kwa kuongeza HISA zaidi,hali inayowalazimu wawe TEGEMEZI kwa MIKOPO ya NJE hasa ya MABENKI ambayo kiukweli ni KANDAMIZI kwani Ina RIBA KUBWA ambayo haiinui MITAJI ya vyama hv vya kutosha zaidi ya kufaidisha MABENKI TU
 
CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
mkuu mi naona watanzania wana matatizo yafuatayo
1.hawana elimu ya kutosha kuhusu biashara hivyo wanakuwa waoga kwamba wakiunga nguvu basi wenzake walioungana nao watamzidi ujanja.
2.pili watanzania hawako honest. unakuta anakuwa na mashaka kwamba mkiunga nguvu hamtafanikiwa ila hawezi kwambia kwanini hamtafanikiwa sijui anaogopa ataonekana ametoa sababu ya kijinga.kumbe hajui hizo ni challenge mojawapo ya kuunganisha nguvu yaani kutoana mashaka. kuna jamaa zangu niliwaitrodyuzia project ambayo haiitaji hata mtaji tunatumia tu kumpyuta walikuwa excited mno ila hadi leo kazi iko mwishoni nimefanya peke yangu sasa sijui walishindwa kuniambia kwamba project haiwezi kulipa au ni uvivu!?
3.watanzani wakipata hela wanahali ya kujisikia na kuamini kwa vile njia alizotumia zimemsaidia kuwa tajiri basi hakuna njia nyingine nzuri kushinda zake.
4.....................
5...................................
maprofesa wamesoma uchumi kazi yao ni kuandika proposals na kupublish papers wanashindwa kuandika vitabu kama hivi ili kutusaidia. nakushauri mkuu hata kama hujasoma uchumi fanya utafiti na andika kitabu kuhusu hii ishu.

Mkuu sababu kuu ni hizi
1. Umaninfu kama ulivyo sema- Hii inatumika kama kigezo ingawa sio sababu kubwa. make kila mtu anataka kutumia hii ya uaminifu

2. Umimi- Hii ndo sababu kuu kabisa ya watanzania kutofanya kuungana, Kila mtu anataka aonekane yeye ni yeye, anataka ndugu, jamaa, marafiki, mke, mchumba na kazalika wamuone yeye anamiliki biashara yake mwenyewe, sasa hapa ndo matatizo yanapo anzia

3. Swala la Elimu nalo lina nafasi yake- Tunafanya biashara ilimuradi tunafanya, Mtu akisha jenga gest yake na wateja wakaanza kuingia basi anaona amemazlia kila kitu, watu hawahangaiki kutafuta mbinu za kusonga mbele,

Na moja ya mbinu za kampuni kusonga mbele kibiashara ni kuungana na kampuni mwenzake au kununua kabisa kampuni mwenzake na kuifanya kuwa moja au kuwa hizo mbili

Mfano,
Kuna kipindi nilikuwa Karatu Arusha, Karatu ni Moja ya miji yenye Magest Mengi kabisa Tanzania hii, Magest ni mengi kuliko Maduka, na wengi wa wateja ni wabongo kama mimi, Na kila mtu analala anaota kujenga Gest, Ila jirani tu kuna Hoteli ya kitalii ya Serena hoteli ambayo ni kampuni kubwa kabisa, na wakati wa watalii wengi inaweza kuingiza Milioni 100 kwa siku, sasa hapo nilini tutakuja kushindana na Hoteli inayo ingiza milioni 100 na zaidi kwa siku? ni kupitia kuungana
 
CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,224
2,000
Ukweli ni kwamba watanzania tuna tatizo la uaminifu kitu kilichosababisha watu tusiaminiane,kwa kawaida mtu usipokuwa muaminifu ni vigumu kumuamini mwenzako.Kuna muheshimiwa mmoja anasema,asilimia themenini ya matatizo ambayo nikikwazo kwa maendeleo yako,yanatokana na wewe mwenyewe,unachotakiwa kufanya ni kujitazama wewe mwenyewe na kubadirika kabla haujaanza kuwaambi wenzako wabadirike.Sidhani katika sisi tuliochangia kama kuna mmoja wetu anahisi na yeye ni sehemu ya tatizo.Mbaya zaidi tumekosa uaminifu karibia kila eneo hatuna uaminifu wa pesa achilia mbali uaminifu wa kazi,siku zote maneno yetu na matendo yetu havifanani.Sasa huu ukosefu wa uaminifu ukiongeza na ubinafsi unaojikita katika mioyo yetu kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya zaidi.Kwa kuwa wakati wa sisi kufunzwa na ulimwengu umewadia,subiri kusikia watu tutakavyokuwa tukilalamika.Shukrani mkuu kwa mada yako nzuri

Haya yanasabaisha kila mtu atake kuwa na Kampuni yake, chukulia mfano tu wa Usafiri Dar, pale kuna wamiliki wa Daladala wa kufa mtu ni wengi mno, kila mtu anadaladala lake pale na hakuna tija kabisa, na yakija hayo mabsi ya kasi na makampuni mengine Makubwa nina uhakika zile daladala either ziplelekwe huko Lindi au zigeuzwe za kubeba mizigo, hapa kwenye mabasi yaendayo kasi ndo Wabongo wa nao miliki Daladala wangekuja na mbinu za kushindana nayo kibiashara, na Badala yake wamebakia kulalamika hawayataki,

Kama kuna Mfanya biashara Bongo anaye invest kwenye Utafiti basi hawazidi wa tatu, tunashindwa kuproject kesho itakuwa vipi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom