Swala la Watanzania kuto kuunganisha Mitaji yao ni sawa na Kujichimbia Kaburi la Biashara

Kweli mkuu,lakini ki ukweli wa tz wengi hawana nidhamu kwenye ushirika,nafikiri ubinafsi huu, ndio ulioua mashirika ya uma, maunganiko ya makampuni mengi yameishia mahakamani
 
Maneno ya msingi ila tatizo ni uaminifu na watu wengi kupenda mafanikio kwa muda mfupi hivyo kila mmoja anapiga hesabu namna ya kumzidi mwenzake kwa kumfanyia timing. Kiukweli point ni nzuri sana kama tutabadilika maana inapunguza gharama ya uendeshaji, mfano mzuri kwa wale wanaofanya kazi ya kutoa bidhaa flani kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine, unakuta mtu anasafirisha mzigo mdogo kwa gharama kubwa kumbe kama wameunganisha nguvu wangeweza kusafirisha mzigo mkubwa kwa ku-share gharama za usafirijaji (nadhani tukianza hapa ni vizuri kisha tunakuja kwenye kuunganisha mitaji yetu)
 
chasa umeongea points tupu.... pia hapa tatzo wafanyabiashara wengine wanafanya biashara zao kimagendo magendo.... ni ngumu mtu wa hivyo kukubali kuunganisha nguvu. halafu naona wengi mmeongelea makampuni makubwa tu...... hata kama una kisaluni chako kitaa na mwenzio anacho eneo hilo hilo mnaweza kuunganisha mitaji na kutoa services za nguvu. lol... ngoja nikatafte wa kuunganisha nae mtaji sasa. nice thread kwakweli.
 
Sio kama Watanzania hawapendi.
Ndugu yangu, kwa tanzania kuna vitu vitatu. Vinafanya hilo jambo kutowezekana

1) Uaminifu. Watanzania uaminifu ni zero. Mkiunganisha mtaji, unakuta mwenzako anazunguka nyuma, anataka faida zaidi.. Hii mimi imenitokea sana, na ndicho kikwako kikubwa hapa Tanzania.
Hatukulelewa kwenye uvumilivu na uaminifu. Kila mtu anajifanya much know na mjanja zaidi ya mwenzake.

2) Elimu. Bado Hatujui kuendesha shughuli as joint venture. As a result tunaingia kichwa kichwa. Tunaambulia disapointment ya kuzidiana ujanja na kudhulumiana.

3) Mazoea ya kushirikiana. WaTz hatupendi fanya kazi pamoja. Ikitokea Mnafanya lazima mmoja ataona anamfaidisha mwenzake.

kama kila mtu anaona mwenzie si muaminifu je nani muaminifu? unajua kinachotuponza ni kuaminiana kupita kiasi...... unakuta watu wanauziana assets bila hata maandikishiano ( hapa hujifanya wanaaminiana); mwisho wa siku mambo yakiharibika tunalaumu fulani si mwaminifu wakati hata wewe umechangia kutokea yaliyotokea. tubadilike sasa.
 
The best idea ever Chasha...hasa hasa sisi weusi,,,tumegawanyika kwa sababu ambazo hata hazieleweki kabisa..utaliona hili kama ukiwa karibu na hawa wa-Asia waliokulia kati yetu..wote huzungumza kuhusu kuwa kwenye 'community' fulani hivi za kwao..wakikutana jioni tender zote hugawanywa huko kwanza, wenye kuhitaji mitaji, kusomeshwa n.k husaidika huko huko...hii ikiwa na nia ya kuona jamii yote inaendelea na hakuna anayebaki nyuma..ni ngumu sana kukuta muhindi anatoa hela yake kwa mweusi kwa dili yoyote wakati kuna muhindi mwenzie anatoa hiyo service,,,
 
Last edited by a moderator:
chasa umeongea points tupu.... pia hapa tatzo wafanyabiashara wengine wanafanya biashara zao kimagendo magendo.... ni ngumu mtu wa hivyo kukubali kuunganisha nguvu. halafu naona wengi mmeongelea makampuni makubwa tu...... hata kama una kisaluni chako kitaa na mwenzio anacho eneo hilo hilo mnaweza kuunganisha mitaji na kutoa services za nguvu. lol... ngoja nikatafte wa kuunganisha nae mtaji sasa. nice thread kwakweli.

Hapo nilipo-bold ndio sababu inayotufanya yusifike maana wengi hufikiria mitaji mikubwa bila kuangalia kipengele cha ujuzi na uzoefu matokeo yake anawekeza ela nyingi ujuzi na uzoefu hana akila loss anakata tamaa, nimependa hapo kwenye saluni za kitaa maana kama watu wataunganisha nguvu service ikawa bomba maana yake hata price itakua kubwa kutokana na mandhari mtakayokuwa mmetengeneza
 
Hapo kwenye bold ndipo shida kubwa ilipo. Watu wanakopa benki mikopo mikubwea bila kuwa na business plans za kueleweka, au wanakuwa na business plans za kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Ni bora kuanza na mitaji midogo midogo na kukua polepole kuliko kuanza kwa mitaji mikubwa na kufilisika baada ya muda mfupi. Kuna kampuni kadhaa ambazo zimeungana na kufanikiwa hapa Tanzania na zinafanya vizuri sana kwenye soko, ingawa nazifahamu chache. Mfano ni Chemi Industries and Cottex Industries walio Mbezi Beach Dar. Hawa walikuwa ni kampuni mbili tofauti, lakini waliungana na kufanya Sumaria Group ambao ndio wanatengeneza dawa za meno, sabuni na bidhaa za plastiki na vitu vingine vingi tu.
 
chasa umeongea points tupu.... pia hapa tatzo wafanyabiashara wengine wanafanya biashara zao kimagendo magendo.... ni ngumu mtu wa hivyo kukubali kuunganisha nguvu. halafu naona wengi mmeongelea makampuni makubwa tu...... hata kama una kisaluni chako kitaa na mwenzio anacho eneo hilo hilo mnaweza kuunganisha mitaji na kutoa services za nguvu. lol... ngoja nikatafte wa kuunganisha nae mtaji sasa. nice thread kwakweli.

Si lazima awe wa salon kama wewe,unaweza kushirikiana na mtu anaefanya biashara ingine,mfano mpesa,halafu mnashirikiana kulipa kodi ya pango,kwa pamoja mnajikuta mnasaidiana kuleteana wateja na pia unajikuta unapata kipato cha kutosha kuongeza mtaji wa biashara yako kwa kupunguza gharama za uendeshaji.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mmmh jamani; mie nimetoa mfano tu ni wapi nimesema nna saluni.
 
Si lazima awe wa salon kama wewe,unaweza kushirikiana na mtu anaefanya biashara ingine,mfano mpesa,halafu mnashirikiana kulipa kodi ya pango,kwa pamoja mnajikuta mnasaidiana kuleteana wateja na pia unajikuta unapata kipato cha kutosha kuongeza mtaji wa biashara yako kwa kupunguza gharama za uendeshaji.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
nimependa mfano wako wa MPESA. mtu unaenda kwenye kibanda unaambiwa hatuna pesa na mtaani unakuta kuna tuvibanda hata tutano unajikuta unatoa pesa kidogo kidogo kila kituo. sasa wakiungana hawa kila mtu akiweka mtaji wake hapo na kugawana mapato kulingana na share waliyoweka si watapata wateja wengi maana kituo kitakuwa cha kuaminika wanajikuta baadae kinakua kama benki.
 
naogopa kuunganisha mtaji kwasababu ya yaliotokea baada yakuunganisha mtaji kupitia NICOL sasa hata siisikiitena lakini wakati ina anza tuliaidiwa mambo mengi.

You shouldn't be running away from the problems. Remember, a problem identified is a problem half-solved. Kwa nini usiunganishe mtaji wako na mwingine/wengine ila u-avoid the previous identified issues?
 
chasa umeongea points tupu.... pia hapa tatzo wafanyabiashara wengine wanafanya biashara zao kimagendo magendo.... ni ngumu mtu wa hivyo kukubali kuunganisha nguvu. halafu naona wengi mmeongelea makampuni makubwa tu...... hata kama una kisaluni chako kitaa na mwenzio anacho eneo hilo hilo mnaweza kuunganisha mitaji na kutoa services za nguvu. lol... ngoja nikatafte wa kuunganisha nae mtaji sasa. nice thread kwakweli.

Mkuu biashara za Magendo si Endelevu, ni maswala ya Muda tu, Chukulia mfano zamani kulivyo kuwa na Magendo ya Kuto bidhaa kenya na kuleta Tz ila baada ya kuondolewa ushuru hakuna anaye fanya magendo tena. na point inabakia kuweza kushindana na makampuni ya Nje, na kinacho bakia ni siku moja kuja kufunga biashara zetu.

Na kuunganisha mitaji si kwa makapun i makubwa bali hata wanao anza kabisa, Wafanya baishara wengi hupata shida ya Mitaji kutokana na upya wao na kukosa dhamana, lakini laiti wangeunganisha nguvu wangeweze kufanya kazi. Watanzania kila mtu anataka awe chake, hata ndugu kuunganisha mitaji ni ishu sana.

Hawa wachina tunao waona wanakuja kwa kasi si kwamba kuna kipindi wataondoka no wanazidi kuja na serikali haiwezi kuwaondoa, na wataleta changamoto kubwa sana kwa upande wa Watanzania,
 
Hapo kwenye bold ndipo shida kubwa ilipo. Watu wanakopa benki mikopo mikubwea bila kuwa na business plans za kueleweka, au wanakuwa na business plans za kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Ni bora kuanza na mitaji midogo midogo na kukua polepole kuliko kuanza kwa mitaji mikubwa na kufilisika baada ya muda mfupi. Kuna kampuni kadhaa ambazo zimeungana na kufanikiwa hapa Tanzania na zinafanya vizuri sana kwenye soko, ingawa nazifahamu chache. Mfano ni Chemi Industries and Cottex Industries walio Mbezi Beach Dar. Hawa walikuwa ni kampuni mbili tofauti, lakini waliungana na kufanya Sumaria Group ambao ndio wanatengeneza dawa za meno, sabuni na bidhaa za plastiki na vitu vingine vingi tu.

True mkuu, Makampuni yote tunayo yaona Duninia yalianza chini, hakuna kapuni iliyoa anzia juu, na watalamu wa Biashara wanasema Biashara nyingi zinazo fanikiwa ni zile zinazo anzia chini kabisa,

Watu wanashindwa kuanzisha biashara kwa sababu hawana mitaji lakini tunasahau kwamba hata buku 10 inatosha kuanzisha biashara na mwisho wa siku ukajikuta iko kwenye orodha ya matajiri,
 
The best idea ever Chasha...hasa hasa sisi weusi,,,tumegawanyika kwa sababu ambazo hata hazieleweki kabisa..utaliona hili kama ukiwa karibu na hawa wa-Asia waliokulia kati yetu..wote huzungumza kuhusu kuwa kwenye 'community' fulani hivi za kwao..wakikutana jioni tender zote hugawanywa huko kwanza, wenye kuhitaji mitaji, kusomeshwa n.k husaidika huko huko...hii ikiwa na nia ya kuona jamii yote inaendelea na hakuna anayebaki nyuma..ni ngumu sana kukuta muhindi anatoa hela yake kwa mweusi kwa dili yoyote wakati kuna muhindi mwenzie anatoa hiyo service,,,

Ni kweli mkuu, wahindi wana umoja sana katika swala zima la Mitaji na kushirikiana, Na wao siraha yao ya kushindana na wabongo ni umoja wao, that is why wako juu sana na ni vigumu kufilisika,

Hili nalo ni moja ya vitu vitakavyo tumaliza, Watanzania tuna wivu sana hatutaki kuinuana kabisa, mtu anaona anamfaidisha mwingine, hata wazungu huku Arusha pamoja na kwamba wametoka Mataifa tofauti laikini wana Umoja wao na huwa wanakutana kwa ajiri ya Chai na kujadili jinsi ya kuifaidi Tanzania, Lakini Hebu itisha kikao kwamba Wafanya biashara watanzania tukutane kujadili maswala ya Biashara, hutamuona mtu na wengi wetu tutaishia kwenda Baa na kwenda Kutazama Ligi za Wingereza vitu ambavyo havina tija kabisa,

Tatizo watanzania bado tunazania furusa ni za kwetu na Serikali itatusaidia, kitu ambacho sio,
 
Ni kweli unasema lkn tatizo ni ubinafsi na kukosa uaminifu

Ok, ila haya yatakuja kutughalimu sana huko tuendako, na time tutakuja kuamuka tutajikuta muda hauko na sisi tena, kwa sasa Dunia imekuwa kijiji na Ulaya, Marekani, Asia, na Amerika ya Kusini wanakimbilia Africa kufanya biashara wanahamishia biashara na makampuni yao Africa, sasa hakuna njia ya kushindana na hawa watu zaidi ya Kuunganisha nguvu la sivyo tujiandae kuwa vibarua,

Fikilia Mfano wa hayo makapuni yanayo pewa Aridhi ya Kulima, ni kampuni zenye Mitaji ya Kufa mtu ni mitaji ya Bilion of Dolla,

Kama tumeshindwa kusoma alama za nyakati basi tusubirie kushindana, kitu ambacho kitakuwa kigumu sana kwa Upande wetu
 
Si lazima awe wa salon kama wewe,unaweza kushirikiana na mtu anaefanya biashara ingine,mfano mpesa,halafu mnashirikiana kulipa kodi ya pango,kwa pamoja mnajikuta mnasaidiana kuleteana wateja na pia unajikuta unapata kipato cha kutosha kuongeza mtaji wa biashara yako kwa kupunguza gharama za uendeshaji.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Point mkuu kinachotakiwa ni kuchukua hatua
 
tatizo la kuunganisha mitaji ni katika mapato, biashara za partnership zina hatari yake kama vile watu kuuana ili m1 afaidike usione tu hizo kampuni zimekuja tu tanzania huwez jua nani damu yake imemwagika mpaka zilipo fika hapa...hizo za kutoka nje...halafu tatizo lingine ni ubinafsi daaah yan ukicheki waarabu wanaumoja kichizi mtoto wa uncle na mjomba shangazi wote wanakaa pamoja na kupiga bizness pamoja lakini ukute mswahili ana ghorofa ukiwaleta na ndugu wengine hapo siku mshua kadanja unakuta uncle anapiga mishe mjengo aurithi yeye yan kwa kifupi si si ni bado sana yan
 
Back
Top Bottom