Swala la Mgombea Urais CHADEMA 2010 ni kimeo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swala la Mgombea Urais CHADEMA 2010 ni kimeo!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Fareed, Jun 21, 2010.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nimesikia kuwa kwenye Chadema kuna kasheshe kubwa ya kumpata mgombea Urais mwaka huu. In fact, wazee wa chama hiki wanaombea kigogo atoke CCM kutoka miongoni mwa Wabunge maarufu au viongozi wastaafu ili wampe nafasi ya kugombea Urais kupitia Chadema.

  Wale viongozi wawili wakuu wa Chadema -- Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa -- wanakwepa kugombea Urais 2010 kwa vile Rais Jakaya Kikwete ana uhakika mkubwa wa kushinda (this is sad but true.)

  Hivyo Freeman Mbowe kaamua kujitosa Bungeni kupitia jimbo lake la zamani la Hai na Dk. Wilbrod Slaa ameamua kutetea jimbo lake la Karatu. Hakuna aliyekuwa tayari kuacha nafasi ya kuwa Mbunge kwa kushindana na Kikwete kwenye mbio za Urais kwani wanaona kuwa its a losing battle kutokana na mazingira yaliyopo sasa hivi Tanzania.

  Ingekuwa Zitto Kabwe kafikisha umri wa miaka 40 kama Katiba ya Tanzania invyotaka, basi angekuwa na njia nyeupe ya kuwa mgombea Urais wa Chadema 2010.

  Kwa ufupi, swala la mgombea Urais Chadema ni kimeo!
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Nina uhakika wanajua wanachokifanya, sababu ulizozitoa za CHADEMA kutosimamisha mgombea sioni kama zina ukweli wowote. Pia CHADEMA hawajasema hawamsimamishi mgombea kwenye nafasi ya U-presdaa!
   
 3. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Si ndo maana zikaitwa tetesi mkuu....???
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sina tatizo na tetesi ya sentensi ya kwanza, tatizo langu lipo wenye red hapo.....IN FACT.....amemaanisha sio tetesi, then ameweka jambo kubwa hapo, Ikifikia wakati ambapo chama kinaomba Mungu ajitokeze mtu kutoka CCM wampe nafasi ya kuutafuta u-presdaa, basi hicho kitakuwa sio chama tena. KITU AMBACHO MIMI NAKATAA, na sikkubaliani na FAREED kwenye hili.

  Lakini pia, anataka kutuambia, CCM ndo kuna vichwa vya kufaa nafasi ya uraisi pekeee? au akimeguka Rostam, CHADEMA itamchukua?
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Jun 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Pole kwa kudanganywa..Usipende sana kuamani vya kuambiwa...
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kama hawana mgombea, hilo ni jambo jema sana, wanachotakiwa kufanya ni kumuunga mkono Lipumba au Mgombea atakayetoka NCCR mageuz (sijui atakuwa Mvungi na mwaka huu). Wakifanya hivyo nina uhakika upinzani mwaka huu utatoka na kura za kutosha, zinazoweza kuleta changamoto kwa Kikwete.
   
 7. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2010
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kimya kingi kina mshindo, tusubiri tuone
   
 8. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  Ni suala la muda tu,tusubiri.
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wapinzani wa tanzania wako kama ile Brethren Council ya Pirates of the Caribbean.. Kila Capt. Anajivotia mwenyewe when they want to choose a leader. So no one wins! Its just stupidly funny. I cant understand why these people do not unite when it comes to the Presidential cadidate... Vituko sana hawa watu. Mimi kwakweli naelewa kwanini watu mwisho wasiku wanaona bora wachague CCM tuu maana.
   
 10. m

  mapambano JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tetesi, mgombea uraisi CHADEMA atatoka CCM :smiling:
   
 11. C

  Calipso JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Labda Lwakatare atagombea...
   
 12. F

  Fareed JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama nilivyosema kwenye post yangu, hizi ni TETESI tu. Tuvute subira ifikapo Oktoba tutajua ukweli halisi. Chadema ndiyo chama kikubwa cha upinzani hapa Tanzania hivyo macho ya Watanzania yapo kwenye chama hiki kuona kitaleta kiongozi gani mbadala agombee Urais 2010 baada ya Kikwete wa CCM kuboronga kwenye uongozi wake. Tusidanganyane jamani, iwapo Mbowe na Dk. Slaa watakacha kugombea Urais ni dhahiri kuwa hakuna candidate yoyote mwingine ndani ya chama hiki ambaye anaweza kuleta ushindani kwa JK. Kama kuna mtu mwenye mfano wa kiongozi huyo atuambie. Ndiyo maana kumekuwa na shauku ya kuona kigogo atoke CCM, mfano Spika Samuel Sitta au Dk. Harison Mwakyembe, ili apewe nafasi ya kugombea Urais kupitia Chadema. Kwa kuwa it is highly unlikely that vigogo watajitoa CCM, Chadema imebaki haina mgombea Urais 2010. Rather than waste scarce resources and embarass the party by fielding a weak presidential candidate, huenda Chadema kisiweke mgombea Urais 2010. Hivyo basi, kuna uwezekano mkubwa sana Chadema kitamuunga mkono Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF agombee Urais ili kuonyesha kuwa at long last kumekuwa na umoja kwenye opposition. Ni dhahiri kuwa bila ya Mbowe au Slaa kugombea Urais, Chadema haina mgombea mwingine mwenye jina kubwa (Hii si tetesi, its simple logic). Fikra za walio wengi ni kuwa bora Chadema iweke nguvu zake kupata wabunge wengi zaidi ili ilenge kushinda Urais 2015.

  It is very frustrating to see that Kikwete wa CCM atashinda urais 2010 huku chama kikuu cha upinzani kikiwa hakina mgombea. Hizi ni tetesi tu, mwenye kujua zaidi atuhabarishe tafadhali.

  ALLAH BLESS TANZANIA!
   
 13. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CHADEMA wapewe muda, nijuavyo CHADEMA huwa haikurupuki katika maamuzi yake. Naamini ina panga mipango mizuri ilikuleta ushindani wa kweli. Kama mwaka 2005 Mbowe alileta changamoto bila kutarajiwa, hivyo tusubiri watakayemleta mwaka huu. Tuwe tayari kumpokea atakayependekezwa na chama maana CHADEMA ni chama pekee kilichoonyesha kwa matendo kushughulikia matatizo ya wananchi yaani ufisadi wa serikali inayoongozwa na CCM.

  Tuungane na vyama vya upinzani kuleta mabadiliko tofauti na vijana wa vyuo vikuu wanaojipendekeza kwa CCM na JK kisa kuganga njaa tu.
   
 14. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Chadema walishasema sema ni lazima watasimamisha mgombea wa Urais piga ua. Hivyo ni sula tu la subra linahitajika. Mtazamo wa kuwa hakuna candidate mwingine zaidi ya Mbowe na Slaa si sahihi sana ingawa nakubali so far Mbowe na Slaa ni strongest candidates. Lakini hata kama wao hawatajitokeza, yeyote atakayepitishwa atabamba tu.
   
Loading...