BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,115
Posted Date::11/22/2007
Suala la madini: Mwanasiasa mkongwe ataka uzalendo kwanza, itikadi baadaye
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi
MJADALA wa uteuzi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe katika kamati ya kuangalia upya mikataba ya uchimbaji wa madini, umeingia katika sura mpya, baada ya viongozi wa dini na waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuunga mkono huku wakiwataka Watanzania kuweka kando itikadi zao katika kushughulikia masuala ya kitaifa.
Kati ya viongozi wa dini na CCM, waliojitokeza kutoa maoni yao kuhusu suala hilo, ni pamoja na Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini na muasisi na mmoja wa wadhamini wa CCM, Peter Kisumo.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro jana, Kisumo, alisema mabishano aliyoyaita ya "kitoto" katika kushughulikia masuala mazito kama ya madini, hayawasaidii Watanzania.
" Hoja kubwa iliyo mbele ya Watanzania sasa, ni suala la madini. Na unapozungumzia suala hilo, utavuka nje ya mipaka ya Tanzania. Na kama tunataka kushinda katika suala hilo, lazima tuungane. La sivyo, hatutashinda," alisisitiza Kisumo.
Alisema katika kujadili ili kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoikumba sekta ya madini, Watanzania wasifungwe na itikadi, bali waweke mbele uzalendo kwani suala la madini linagusa makampuni makubwa duniani na kuonya kuwa, kusipokuwa na umoja katika kukabili suala hilo, ni rahisi kushindwa.
Unapozungumzia suala la madini unagusa maslahi na makampuni yaliyo nje ya mipaka ya Tanzania, unagusa Congo, Lesotho, Afrika Kusini, Ghana, Peru na hata Canada. Hivyo, bila umoja, ni kazi kubwa kushinda vita hivyo, alisema Kisumo.
Aliendelea kuonya kuwa, kitu chochote kinachohusu mataifa mengine kukabiliana nacho kinahitaji kuunganishwa kwa nguvu, kwani linapojadiliwa suala la madini, linagusa mataifa na makampuni makubwa duniani.
Kisumo, alisema mjadala unaoendelea Chadema kuhusu ushiriki wa Zitto Kabwe au la kwa sababu tu kwamba, wakati Rais Jakaya Kikwete anaunda tume hiyo, hoja iliyokuwako katika jamii iliibuliwa na mbunge huyo bungeni, ni mtazamo finyu unaotakiwa kuachwa mara moja.
Alisema hatua ya Kikwete kuunda tume hiyo hakusukumwa na hoja ya Zitto kama watu wengi wanavyojaribu kuionyesha, bali ilikuwa ni hoja na Rais tangu siku yake ya kwanza ya urongozi wake aliithibitisha wakati akizindua rasmi Bunge la Jamhuri ya Muungano, Desemba 2005.
Ni kweli wakati Rais Kikwete anaunda tume hiyo, hoja ya Zitto ilikuwa imetanda katika taifa letu, lakini pia inawezekana hata huyo Zitto alipata nguvu ya kuibua hoja hiyo kwa sababu ya msingi wa hoja hiyo ambayo aliitoa Rais, ? alisema Kisumo.
Aliwataka Watanzania kumuunga mkono Rais Kikwete katika jitihada zake za kulipatia taifa haki yake katika madini, ambayo sehemu kubwa sasa inatwaliwa na makampuni ambayo aliyaita kuwa ni ya mabepari.
Vilevile, aliwapongeza waasisi wa Chadema, Edwin Mtei na Bob Makani kwa msimamo wao ambao umelenga katika utaifa zaidi badala ya maslahi ya kisiasa na kuwashauri Watanzania kufika mahali watenganishe maslahi ya taifa na ya kisiasa.
Kauli ya Kisumo imetolewa huku kukiwa na malumbano makubwa ndani ya Chadema baada ya Kikwete kumteua Zitto katika tume ambayo itaangalia mustakabali wa madini nchini.
Kumeibuka makundi mawili ndani ya chama hicho, moja linapinga ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo kwa hofu ya CCM kutumia ushiriki wake kumrubuni ili asiendelee na msimamo wake katika suala la madini.
Jingine likiongozwa na Mtei na Bob Makani, linataka Zitto kushiriki katika kamati hiyo, aweze kupakua ukweli kuhusu sheria na masuala yote ya madini ili kuhakikisha madini yanamsaidia Mtanzania.
Kwa kuona uzito wa mjadala huo, Chadema imeitisha kikao cha Kamati yake Kuu kwa ajili ya kujadili suala hilo, kinachotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, kesho.
Wakati Kisumo akisema hayo, Askofu Kilaini, ameitaka Chadema kumruhusu Zitto kuwa katika kamati hiyo, kwa kuwa ataweza kuibua mambo mengi zaidi wakati wa kupitia mikataba hiyo.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake, Askofu Kilaini, alisema Chadema na watu wengine hawapaswi kupinga uteuzi huo kwa kuwa wapinzani wamepata nafasi ya kubaini kilichopo katika sekta ya madini nchini.
Alisema kuchaguliwa kwa wapinzani katika kamati hiyo, kutawasaidia kuunda na kujenga nchi kwa kuwa watakuwa wamebaini mambo ya msingi yaliyoko katika sekta hiyo.
Sisi tumefurahi sana kusikia wapinzani wamechaguliwa katika kamati hiyo kwa sababu tunataka waingie huko na watueleze kuna nini na wala Chadema isimpinge Zitto, alisema Askofu Kilaini.
Alisema endapo Chadema ina wasiwasi kuwa Zitto atarubuniwa, basi wasikubali awepo katika kamati hiyo na kama inamwamini imwache aendelee kuwapo.
Kama wanadhani (wapinzani) atarubuniwa, hatufai (Zitto) na hivyo basi Chadema wasikubali aaende huko, wakatae kwani hatatusaidia hata kidogo, alisema Askofu Kilaini.
Alimpongeza Kikwete kwa kuunda kamati hiyo na zaidi baada ya kuwajumuisha wajumbe kutoka kambi ya upinzani.
Kamati iliyoteuliwa na Rais Kikwete ina wajumbe 12 na iko chini ya uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani.
Tangu aunde kamati hiyo na kumteua Zitto, baadhi ya watu wakiwamo wafuasi wa chama hicho, wakiongozwa na Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe, wamekuwa wakipinga uteuzi wake kwa madai kuwa unadhoofisha hoja za wapinzani na kujenga usaliti baina yao, kuhusiana na suala la madini nchini.
Novemba 13, mwaka huu Kikwete alitangaza kuundwa kwa kamati ya kuangalia upya mikataba ya madini na kuwateua wajumbe wake.
Wengine ni mbunge wa wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera wa Wizara ya Fedha, Mugusha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe.
Wamo Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige, Peter Machunde wa Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu wa Kampuni ya ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, Price Water Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai ya Sheria za Kimataifa, Maria Kejo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.