Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,310
- 21,618
Nimepata kuona vipindi mbalimbali vya mheshimiwa Ayubu Mzee vinavorushwa na kituo cha televisheni kiitwacho Ben kila Jumanne na Alhamisi saa za jioni.
Mara ya mwisho kuona moja ya vipindi hivo ni kipindi kuhusu ziara ya aliekuwa waziri mkuu bwana Frederick Sumaye hapa UK na vipindi vingine tu vinavoonesha mambo mengine kwa lugha ya kiingereza.
Nafikiri vipo vipindi ambavyo huyu mheshimiwa amejaribu kuleta kwa hadhira ya hapa UK ambavo vina lugha yetu ya kiswahili ingawa mpaka sasa naona mwandishi huyu wa habari(kama anavojiita) sijaona "dynamic" yoyote ya vipindi vyake vikiwahusu watu wa Afrika mashariki ambao ni wengi tu hapa UK wakishiriki vipindi vyake.
Sasa hii ni moja ya "advert" yake alioiweka katika tovuti ya TZUK.net leo:
Every week Tuesdays at 10.00 pm and Thursdays 9.30 BEN TV SKY 194 broadcasts a program called Swahili diaries. It a program which show cases the cultural, social and economic aspects of Africans especially the Swahili in the Eastern Africa region. This program has been a source of information for Africans wanting to learn about what is going on in the Diaspora and when Europe wants to learn about Africa. This Program has receive several Awards. This program is presented and produced by experienced Journalist Mr Ayoub mzee.
Nimeangalia "profile" ya huyu mheshimiwa lakini naona haioneshi kazi au mtiririko unaoeleweka na unaoonesha kwamba labda amefanya wapi kazi yake hiyo la kama labda ni mwandishi wa kujitegemea au wa kuajiriwa.
Sina maana mbaya kwa kuhoji hili ila nnataka jua tu kuhusu hii sehemu.
Hoja yangu ni kutaka kuona kwamba mheshimiwa Ayubu Mzee anawashirikisha watu wanaozungumza lugha ya kiswahili katika vipindi vyake vya "Swahili Vibes" na kuvileta kwa hadhira vikiwa na lugha ya kiswahili.
Ayubu Mzee anatayarisha vipindi kwa ajili ya kuleta kwa watu wanaozungumza kiswahili kama kipindi kinavyoonesha -swahili vibes na si vinginevo asikiite swahili vibes.
Vipindi vingi ambavo anapeleka kwenye hiyo BEN television vinakuja kwa lugha ya kiingereza sasa nini maana ya swahili vibes?
Kama inawezekana ni budi kuweka "subtitles" za kiswahili ili kama mtu anapenda kusoma maneno ya kiswahili na kuelewa kwa ufasaha yale yanayoongelewa.
Vingivevo Ayubu Mzee aache kuleta vipindi ambavyo vinazungumzia mambo yasiyo ya kiswahili au abadilishe kichwa cha kipindi hicho.
Pia Ayubu Mzee anatakiwa aende na wakati kwani kuna "issues" nyingi tu zinazowahusu watu walio mbali na nyumbani kama wakati ule ambapo wawakilishi wa CRDB waliwahi kuja hapa London na yeye anaepata muda wa kutayarisha kipindi akiwahoji watu hao na kupata ufafanuzi kuhusu ufunguaji wa akaunti ya Tanzanite.
Au wakati huu wa kumkumbuka hayati mwalimu J.K.Nyerere basi ilikuwa ni nafasi kwa bwana Ayubu kuandaa kipindi kinachoonesha mjadala kuhusu J.K.Nyerere na nini ameacha kwa wabongo na waafrika kwa ujumla.
Kazi ya uandishi sio lelemama, ni kazi inayohitaji "dedication" ya hali ya juu,inabidi apate ushauri kuhusu kutengeneza "documentaries" kutoka kwa watu kama Sorious Samura mwandishi wa kutoka Sierra Leone.
Sorious ametengeneza "documentaries" za hali ya juu kama ile inayoitwa "living with illegals" ambapo anashiriki na wazamiaji wa kiafrika wanaotafuta maisha bora ughaibuni na sasa ametoa DVD!
Kwa hio kazi kwako mheshimiwa Ayubu Mzee, swahili vibes kiwe kioo kwa waafrika mashariki na wengine wazungumzao kiswahili katika kutela tija kijamii,kisiasa na kiuchumi.
Pia kiwe kweli chanzo cha habari kwao na si mambo mengine.