Suzuki Carry Truck | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suzuki Carry Truck

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pinokyo Jujuman, Jun 20, 2012.

 1. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani mtakubaliana nami kuwa mshahara wa mfanyakazi wa kawaida wa serikali kuwa hautoshi kwa maisha ya sasa.
  Kutokana na suala hilo wengi wetu huona ni heri mtu akifanya kitu cha ziada ili aongeze kipato kutoka vyanzo vya nje, sasa kwangu mie nimeona nijaribu kufanya biashara ya gari ndogo za mizigo(Suzuki carry).
  Mie ni mgeni katika ujasiriamali wa namna hii tafadhari kwa wale wazoefu, naomba mnijuze ni maeneo gani mazuri kwa biashara hii hapa Dsm, na gari hulaza bei gani kwa siku na mengine muhimu!!.
   
 2. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Nilivyosiakia hicho kijigari zamani kilikuwa kinalaza elfu 20 but nasikia hesabu imepanda hadi elfu 25 per day safi sana jioni kinalala..

  ila nawasi wasi navyo kwani nimekuwa nikiviona vinavutana sielewi huwa vinakuwa na matatizo gani ya kuharibika halibika...

  nilitaka kukinunua kimoja but muuzaji aliniboa aliponiambia anauza m7.2 alinichefua kuliko maelezo mie nilikiona kama kibajaji kumbe ni deal....

  ila mkuu kama ungekuwa na pesa kiasi ungenunua daladala kwani waweza pata hata kwa 10m lililotumika then uka lipiga service ya nguvu kuanzia engene na body ambayo inaweza kukugharimu kama 3m au pungufu theni hesabu unakuwa unapata elfu 60 hadi 70 per day yaani unachumpa kimahesabu kisuzuki utapata laki nne hadi sita kwa mwezi na ukiwa na daladala unapata kuanzia 1.5 hadi 1.8 kwa mwezi... na biashara ni ya uhakika... hata kama umekopa pesa zitarudi ila usisahau kukata Insurance Kubwa yaani Comprehensive... achana na vi third party
   
 3. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duduwasha: aksante kaka kwa comment yako lakini kwa bahati nzuri au mbaya nshakinunua na nshakikatia Comprehensive insurance sasa nakitafutia kituo au tenda na dereva nshampata"
  Kaka ujue hivyo vigari hapo awali vilikua ni m4 tu unapata bt sisi wenyewe ndio tumevipaisha vinapanda bei kila leo coz demand yake ni kubwa mno; ukienda show room ni m7.5 had m8.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu, asubuhi na mapema baada ya salaat alfajir nenda mitaa ya Tandika pale kituoni na ukipata deals za kariakoo ambazo ni nyingi, pitia kilwa road. HUkosi 70 mpaka laki kila siku na ujanja mzuri, viinulie machuma pembeni ili watu na mizigo yao midogomidogo, waweze kupanda nyuma hasa nyakati za magharibi wakirudi uswazi kutoka mitaa ya k,koo, ubungo.
   
 5. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka ujue hiki kigari kidogo sasa ukikifunika na bomba unakua unakibana,mizigo kama fridge huwezi beba, labda pemben.
   
 6. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Hufuniki na bomba, unaziongeza pembeni usawa wa kiuno, hizo ni kama Toyo tu, sema zina cabin ya gari.
  ONGEZA vyuma pembeni usawa wa kiuno, acha ubishi mi nakupa deal upate fedha za bure.
   
 7. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahaaa; kaka sio ubishi, nadhani sikukuelewa tu, nilidhani wamaanisha niifunike kuhusu kueka vyuma pembeni hilo halina ubishi nitaweka lakini kwa sasa kipato bado ni tatizo ni mjasiria mali mchanga wacha iokote visent kdogo itajiwekea yenyewe bomba za pembeni"
  Nashukuru kwa ushauri.
   
Loading...