Surupwenye la Mkapa JK halimtoshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Surupwenye la Mkapa JK halimtoshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwigamba son, Apr 14, 2012.

 1. Mwigamba son

  Mwigamba son Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu wana JF wakati JK anafanya kampeni za urais mwaka 2005 nilivutiwa na mwonekano wake pamoja na kauli mbiu yake ya maisha bora kwa kila mtanzania. Nilikuwa na imani kubwa na ile kauli mbiu japo kisera Mbowe alionekana kumzidi JK namna ya kuzinadi. Ni mtangulizi wake Mkapa ndiye aliyenishawishi kumuunga mkono JK hii ni kutokana na mambo mengi mazuri aliyoyafanya Mkapa ktk uongozi wake.
  *wakati mkapa anaingia madarakani nchi ilikuwa na madeni mengi ya nje na ndani, alijitahidi akalipa na mengine akasamehewa hivyo mpaka anaondoka madarakani aliiacha nchi ikiwa na ziada (surplus) hazina.Tofauti na kipindi cha JK ambapo deni limeongezeka takribani 30%.
  *Zaidi ya hapo elimu ya juu ilikuwa ni bure kwa yeyote bila ubaguzi kwa tajiri na maskini, equivalent na mature age wote walikuwa na haki sawa na fani zote zilikuwa na fursa sawa ilimladi tu mtu uwe umefauru kuingia chuo.Tofauti na kipindi hiki cha Jk ambapo elimu hiyo imekuwa ya kulipia kwa mfumo wa mikopo ambayo pia inawabagua equivalent na mature age ambao wengi wao ni watoto kutoka familia duni ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia njia hizi mbili kutokana na hali zao za maisha kuwalazimu kufanya hivyo. Kwa namna nyingine hii inatoa tafsiri kuwa watoto wa maskini hawana haki ya kupata elimu ya juu.alibuni miradi yenye kufufua uchumi kama bomba la maji la kahama, kudhibiti mfumuko wa bei,aliipandisha thamani pesa yetu 1$=1000tsh tofauti na sasa ambapo 1$=1600. mkate,sukari,unga maharage,mchele vilikuwa kati ya sh 200-400 tofauti na sasa ukienda sokoni una kuwa huna hakika ya bei kama ni ileile kutokana na kupanda kila uchwao ambapo ni kati ya sh 1200-2400.Mkapa aliasisi mpango wa mmem,mageuzi ya ujenzi wa barabara za rami na ujenzi wa uwanja wa taifa.haya nibaadhi ya mambo makubwa aliyoyafanya Mkapa pamoja na kasoro ndogo alizonazo na ndio maana Jk wakati analihutubia bunge kwa mara ya kwanza alisema viatu alivyomwachia Mkapa ni vikubwa kwake na kuonesha shaka ya kufikia mafanikio ya Big Ben " THE END JUSTIFY THE MEANING". SURUPWENYE LA MKAPA KIKWETE HALIMTOSHI
   
 2. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa na hapo ndio huwa namshangaa Mkapa. Yaani badala ya kumtukana ....... au kuwatukana chama tawala kwa kushindwa walao kuendeleza juhudi zake katika ukusanyaji wa kodi na kudhibiti thamani ya shilingi anawatukana wapinzani.
   
 3. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
 4. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Good analysis, big up Ben
   
Loading...