Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,552
- 6,114
Dola ya Rumi au unaweza kuiita Roman Empire ni moja ya falme nne zenye nguvu zilizo tokea kuitawala duniani kama ilivyo tabiriwa kutoka kwenye maandiko matakatifu. Soma kitabu cha (Danieli sura ile ya pili)
Dola hii iliyo anza kuitawala Dunia kuanzia mwaka wa 27BC mara baada ya kuanguka kwa utawala wa Wayunani (Ugiriki ya Kale). Iliitawala Dunia kwa karne zisizo pungua tano mpaka hapo ilipo kuja kuvunjika yenyewe mwaka wa 476AD ikitoka katika mfumo wa Rumi ya kipagani na kuja Rumi ya kidini.
Dola hii iliongozwa na viongozi mbalimbali kama Julius Caesar aliye zaliwa mwaka wa 100BC na kufariki mwaka wa 44BC. Huyu ndiye chanzo cha viongozi wa dola hii ya Rumi kuanza kuitwa KAISARI yaani kama saivi tunavyo waita viongozi wa nchi Rais,
Basi bhana cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba tangu utawala wa Dola hii ya Rumi uanze viongozi wao wote sura zao zipo mpaka leo zinajulikana lakini sura ya Yesu Kristo haijulikani mpaka leo.
Ilikuwaje mtu ambaye alikuwa maarufu kipindi hicho kwa maajabu na miujiza yake aliyo kuwa anaitenda sura yake isijulikane mpaka leo maana Yesu Kristo popote alipo kuwa anaweka mguu maelfu ya watu walimfuata.
Inakuwaje mtu huyu sura yake mpaka leo iwe kitendawili lakini sura za watawala ziwepo tena wengine waliishi kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo mfano ni huyo Julius Caesar.
Kipindi Yesu Kristo anazaliwa Duniani mtawala alikuwa ni Kaisari Augustus akafuata Kaisari Tiberias, akafuata Kaisari Caligula, akafuata Kaisari Claudias, Kaisari Nero na wengine wengi ambao sura zao zipo.
Sura tunazo aminishwa ni za Yesu Kristo ni sura za binadamu ambao tunao hapa hapa duniani ambao ni wasanii wacheza filamu wakina Brian Deocon. Jim Caviezel, Diego Morgado na Robert Powell.
Chakushangaza na kusikitika ni kwamba watu hawa wamekuwa wakiabudiwa na kusujudiwa sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye nyumba za ibada majumbani mwa watu n.k.
Madhehebu yanayo fanya ibada siku ya Jumapili ndio vinara wa kuwaabudu hawa wasanii wakina Brian Deacon na genge lake. Je ni sahihi kuwapotosha maelfu ya watu kuamini hao ndio Yesu ilhali sura ya Yesu Kristo hakuna aijuaye?
Biblia inakataza katika zile amri kumi za Mungu kuwa tusiwe na miungu wengine ila Mungu pekee na wala tusiabudu chochote isipo kuwa Mungu pekee(kutoka 20).
Mwisho Namalizia kwa kusema shetani ananguvu sana hapa Duniani tuzidi kumuomba Mungu sana.