PENGINE NI MIMI TU NA UDHAIFU WANGU WA KUNG'AMUA MAMBO HARAKA NA KWA USAHIHI WAKE ILA MPAKA HAPA HOJA YAKO INAKUSALITI NA KUKUTIA TU NDANI YA KAPUMOJA WAPIKA MAJUNGU WENGINE TU ENDAPO HUNA UTHIBITISHO
Kijana unalo hoja kuelekeza vidole vyako kwenye kile unachoamini kuwa pengine ni mapungufu ya chama chetu lakini bila kuweka utetezi wa madai yako hadi hapo kila ulisemalo ni vigumu sana kutenganishwa na MAJUNGU SUGU yaliozoeleka kwingineko tu.
Pengine kuna ka-ukweli uliouna mwenzetu tatizo tu ni kwamba umekua muoga na kuchagua kula KONA KALI kwa kutaja tu mambo bila ya kuyawekea mafiga kitakoni ili yeyote mwenye akili aweze kugutuka na wala kuanza kujiuliza kitu. Hebu acha uvivu, thibitisha kauli yako.
Kwa upande mwingine umejinyima maksi nyingi tu kwa kutokutufahamisha lolote juu ya hali halisi ilivyo kwa Vyama Vingine vya Siasa nchini na hasa kile kilichokua cha Baba yetu wa Taifa Mwl Nyerere. CCM ni chama ambacho kingekua ni binadamu, kwa umri wake, kingekua na wajukuu kibao sana tu.
Hivyo unapoamua kuchambua vyama vya siasa na silka zake ni kwamba picha haitokamilika bila kuelezea hali ilivyo huko kwa wenzetu pia. CHADEMA kimeanza majuzi tu na hivi sasa ndio kinapokea RUZUKU YA SERIKALI kwa mara ya pili tangu kusajiliwa hivyo kwa kipindi chote LAZIMA kilikua kikiegemea kwa wahisani wa eneo fulani tu na hilo ni jambo la kawaida sana.
Shida tu ni kwamba hali hiyo ifike mahala ijitenge kadiri chama kinavyoendelea kupata kujitegemea kama vile hivi sasa bwana mzee. Kosa liko wapi?? Kama kweli ulifanya homework yako vizuri labda ungeweza kugundua kwa nini Mzee Sykes amekua kiongozi wa taasisi zetu za ndege miaka nenda runi na uongozi kuendelea kung'anga'ania nyumbani kwake mpaka wanawe na vijuku kuja kutuongoza kama Ma-Meya hapa jijini.
Nasema pengine utabiri wako utakua mzuri kama wa kwangu tu kwamba huyu baba na Mzee Mbowe (Baba yake Mwenyekiti CDM) ni miongoni mwa watu wachache waliokua na uwezo wakati huo ambao kwa moyo wa kupenda nchi yetu waliweza kuchangishana nauli kwa ajili ya Mwalimu Nyerere na wenzake kuweza kupanda ndege kwenda Lancaster House Uingerera kutuletea uhuru chini ya TANU.
Endapo mtu anaanza kuwanung'unikia hawa wafadhili wetu CHADEMA walioona mbali sana kimageuzi ya kweli nchini wakati wengi wa wazazi wetu wakiona hata kukiunga tu mkono chama cha upinzani nchini ni dhambi achilia mbali kuanzisha kabisa chama na kukilea kutoka kwenye MIFUKO BINAFSI KWA KUJINYIMA MKATE WA FAMILIA, basi nawashauri wakakimbie haraka sana kwenda kwapiga mawe akina Mzee Kunambi, Mzee Sykes, nasema kacharazeni fimbo kaburi la Mzee Mbowe kwa fedha walizotoa TANU hadi leo hii wengine ni HAPPY-GO-LUCKY mtindo mmoja.
Hebu kimbieni, tukawachape hawa akina Mzee Mtei, Mzee Makani, tukampige mawe kabisa hata huyu Mbowe Mwenyekiti wa CDM sasa hivi kwa kuwa hawana lolote ni wapuuzi tu.
Unafikiri watu kama Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pindi wanapotukosea kama jamii tunabaki tunajiumauma tu ovyo huku makwetu Uswahilini unafikiri hatujui tulitendalo; kuna mchango walitoa huko nyuma ambao hakuna thamani ya hela inaweza ikawarudishia leo hii!! Ila ikija suala la hawa MACHEPELE wenye kuturubuni na fedha walizotuibia KIFISADI (umepatia; nilikua namaanisha hao hao RACHEL + JK) wala hatuwaonei aibu hata kidogo!!
Mwenzangu ukiniuliza mimi hapa kwamba nimechangia kwa kiasi gani cha fedha kukitegemeza chama chochote cha siasa nchini ili kisitegemee watu (ambao ni sharti watoke ukanda fulani katika nchi) jibu langu ambalo ni UKWELI NA UKWELI MTUPU (Mungu niadhibu nianguke nife sasa hivi nikidanganya) si zaidi ya ule mchango wa kadi yangu tu ya uanachama na zaidi huku kuchangia mawazo jinsi gani mambo yaendeshwe kunawirisha chama kwa lengo kuu la KUBORESHA MASLAHI YETU SOOOOTE KAMA UMMA WA TANZANIA bila kujali itikadi zetu.
Nakuambia kila unaponiona nikichangia hapa jukuani mimi malipo pekee ninayotarajia kutoka CHADEMA ni hilo hapo kwenye wino wa bluu ambapo endapo litakua halizingatiwi kwa Maslahi ya Walalahoi kwa ujumla wetu basi hadi hapo niko tayari kugeuka mbogo kwa mtu yeyote yule ndani ya CDM bila kujali umri wala wadhifa wake ndani ya chama chetu - MINE IS A UNITY OF PURPOSE and NOT a UNITY OF FESTIVITY as at CHADEMA Full Stop!!!
Kwa umri wa TANU, kama CHADEMA hivi sasa, kilikua kinahitaji msaaada wa wenye moyo na udhati wa kupenda nchi hii bila UFISADI - Shime sana kwa Familia za Mzee Sykes, Mbowe na wengine wachache wa wakati wao huo.
Nasema hivi kwa sababu mtu huwezi kusema ugali wa mtama ni mbaya sana bila kutufahamisha huo ubaya ulikua ukiulinganisha na nini pembeni mwake. Hebu kachukue hizo picha na ukaziakisi pia kwa TLP, CCM, NCCR-Mageuzi, CUF na kadhalika kisha ukatufahamishe kwamba kwenye maabara yako kisiasa mwenzetu umeona nini??
Hitimisho langu ni kwamba kwa mtu yeyote asiyejua historia ya jamii yake au taasisi anamojishughulisha wakati wote ni kwamba mtu huyu wala wapi tunakokusudia kwenda wala hana fununu nalo hata chembe isipokua macho yake yooote yanabakia yakiwa yamekodoleka kuhesabu tu Manemane ya hivi sasa na jinsi 'yanavyoendelea kunyesha zenyewe tu kama mvua' toka angani.
Mwana-CDM mwenzangu, endapo kuna kaukweli wowote utakua umebahatika kuumega toka kwenye haya mawazo binafsi niliyoyaandika basi chonde usikose kunijulisha. Mapambano mema, wont you???