Sura na Picha ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sura na Picha ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, May 2, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nionavyo mimi sura na picha ya CHADEMA imejikita kwa mambo yafuatayo:


  1. Foudership syndrome! "Sisi ni waanzilishi"

  2. Ownership syndrome! "Bila ya mimi....., ......., na fulani hakuna CDM"

  3. Zonal syndrome! "Watu kutoka Kanda X ni wajasirialimali na wanauchungu zaidi kuliko watanzania wengine".


  Kuna waheshimiwa wengi tu ndani ya CDM wako frustrated kwa sababu ya hivi vigezo vilivyopitwa na wakati. Soon, yatajitokeza mengi ndani ya CDM.


  Huu ni mtazamo wangu, lakini yaweza ikawa picha ya ndani na nje ya CHADEMA kwa baadhi ya watanzania wakomavu na wenye uelewa katika maswala ya siasa, uchumi na jamii. Until CHADEMA realizes this truth......................
   
 2. d

  daniel.nickson Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wazo pia, lakini ili chama kiweze kuendelea ni lazima kiwe na compas, yaani watu wanaojua kusoma alama za nyakati.na watu kama hawa ni lazima wawe na sauti ndani ya chama ili chama kinapotaka kupoteza muelekeo/direction waweze kukirudisha katika line.lakini kama kitakuwa hakina watu kama hao na viongozi kama akina zito wanaobadilika kila sekunde kama kinyonga lazima kitakufa.mfano mzuri tazama nccr ilipoanzia na ilipo sasa, tazama TLP ( mwenyekiti ni ccm lakini hakuna mwenye uwezo wa kuhoji). na huo wasiwasi wa foundership, ownership na zonal mimi nafikiri ni kwasababu bado chama ni kichanga, ndio maana bado nasisitiza chadema watembelee kata zote na ikiwezekana kila kijiji ili baada ya muda mfupi tuweze kupata viongozi wanaotoka kila kona ya nchi katika ngazi mbalimbali.
   
 3. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mada yako sijaipenda wala nn.
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  c.r.a.p!
   
 5. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana CDM siku zote UHALISIA HATUUTAKI KUUSIKIA
   
 6. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je ni kweli, founder-syndrome, ownership-syndrome na zonal-syndrome ni vitu vipo ndani ya CDM?

  Kama ni kweli what next?

  Kama si kweli, lets hang on there, time will tell..........
   
 7. t

  thinktank Senior Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We know everything syndrome, mbona hii hujaitaja?
   
 8. m

  mkuki moyoni Senior Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashangaa kuona leo tumeanza kusikiliza jamani....sioni matusi wala ubishi,nadhani sasa watu mmeanza kuwa wasikivu ili mwisho wa siku mtoe jibu sahihi bila ushabiki,i knw cdm kuliko ww,meen,
  haya hii mada ni ya kweli kwani tumeona mengi sana na kinachomuumiza kichwa mbw ni nani atakuwa mwnykt baada yake,ila katba yetuinasema mwenykt hana ukomo,sooo tutamwona mbw akirejea tena na kugombea ili aaibike, hatutaki ujinga huu wa usultani..
  hata waliokuwa wnamwabudu hawako nae tena,akina mnyika hawana sauti kama awali hawaongei kwnye vikao kama zamani,tena nakumbuka kuna wakati mnyka alikorofishana na jamaa ilikuwa kazi aisee,dogo alionyesha kutaka kuahirisha siasa ila wakambembeleza akatulia... mbw hivi unayaona haya....je hujui ipo siku watz wote watajua mambo yako ya ajabu...nimesoma gazeti leo nikata nilie jamani....zitto alimwambia kuwa jamaa anajenga makundi ndani ya chama,na yatamgharim baadae...loo!!!!!!kwa nn hutaki cdm ienee kona zote na kwa nn hutaki ujenzi wa matawi ww au ndo ruzuku yako tu
   
 9. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hujaielewa utaipendaje???????
   
 10. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kuona utoe comment zaidi ya kuandika neno CRAP! kweli humu JF sio wote ni magreat thinker hata vichaa nao wamo!
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Crap...........
   
 12. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu una uhuru wa kutoa mawazo.
   
 13. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mbowe mtamsema mtakavyo ila history ilishajiandika ndiye mkiti aliyeisongesha cdm kuliko mwingine yyt hata vijana kujiunga na siasa alifanya effort kubwa kuwang'oa wababaishaji waliokuwa makao makuu na kuwaingiza vijana mnyonge mnyongeni haki yk mpeni , as human being hajakamilika ila na mazuri yk muyaweke
   
 14. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja, acha sura ya CDM iiendelee kubaki hivyo hivyo mimi kwa mtazamo wangu sioni kama pana madhara kwani hao wanaosemwa wa ukanda X sisi sote ni mashahidi ndiyo walioifikisha CDM hapo ilipo na sasa imekuwa ni chama cha TZ nzima si cha ukanda tena , nalithibitisha hili kwa wawakilishi wabunge tulionao wa viti maalum
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  PENGINE NI MIMI TU NA UDHAIFU WANGU WA KUNG'AMUA MAMBO HARAKA NA KWA USAHIHI WAKE ILA MPAKA HAPA HOJA YAKO INAKUSALITI NA KUKUTIA TU NDANI YA KAPUMOJA WAPIKA MAJUNGU WENGINE TU ENDAPO HUNA UTHIBITISHO

  Kijana unalo hoja kuelekeza vidole vyako kwenye kile unachoamini kuwa pengine ni mapungufu ya chama chetu lakini bila kuweka utetezi wa madai yako hadi hapo kila ulisemalo ni vigumu sana kutenganishwa na MAJUNGU SUGU yaliozoeleka kwingineko tu.

  Pengine kuna ka-ukweli uliouna mwenzetu tatizo tu ni kwamba umekua muoga na kuchagua kula KONA KALI kwa kutaja tu mambo bila ya kuyawekea mafiga kitakoni ili yeyote mwenye akili aweze kugutuka na wala kuanza kujiuliza kitu. Hebu acha uvivu, thibitisha kauli yako.

  Kwa upande mwingine umejinyima maksi nyingi tu kwa kutokutufahamisha lolote juu ya hali halisi ilivyo kwa Vyama Vingine vya Siasa nchini na hasa kile kilichokua cha Baba yetu wa Taifa Mwl Nyerere. CCM ni chama ambacho kingekua ni binadamu, kwa umri wake, kingekua na wajukuu kibao sana tu.

  Hivyo unapoamua kuchambua vyama vya siasa na silka zake ni kwamba picha haitokamilika bila kuelezea hali ilivyo huko kwa wenzetu pia. CHADEMA kimeanza majuzi tu na hivi sasa ndio kinapokea RUZUKU YA SERIKALI kwa mara ya pili tangu kusajiliwa hivyo kwa kipindi chote LAZIMA kilikua kikiegemea kwa wahisani wa eneo fulani tu na hilo ni jambo la kawaida sana.

  Shida tu ni kwamba hali hiyo ifike mahala ijitenge kadiri chama kinavyoendelea kupata kujitegemea kama vile hivi sasa bwana mzee. Kosa liko wapi?? Kama kweli ulifanya homework yako vizuri labda ungeweza kugundua kwa nini Mzee Sykes amekua kiongozi wa taasisi zetu za ndege miaka nenda runi na uongozi kuendelea kung'anga'ania nyumbani kwake mpaka wanawe na vijuku kuja kutuongoza kama Ma-Meya hapa jijini.

  Nasema pengine utabiri wako utakua mzuri kama wa kwangu tu kwamba huyu baba na Mzee Mbowe (Baba yake Mwenyekiti CDM) ni miongoni mwa watu wachache waliokua na uwezo wakati huo ambao kwa moyo wa kupenda nchi yetu waliweza kuchangishana nauli kwa ajili ya Mwalimu Nyerere na wenzake kuweza kupanda ndege kwenda Lancaster House Uingerera kutuletea uhuru chini ya TANU.

  Endapo mtu anaanza kuwanung'unikia hawa wafadhili wetu CHADEMA walioona mbali sana kimageuzi ya kweli nchini wakati wengi wa wazazi wetu wakiona hata kukiunga tu mkono chama cha upinzani nchini ni dhambi achilia mbali kuanzisha kabisa chama na kukilea kutoka kwenye MIFUKO BINAFSI KWA KUJINYIMA MKATE WA FAMILIA, basi nawashauri wakakimbie haraka sana kwenda kwapiga mawe akina Mzee Kunambi, Mzee Sykes, nasema kacharazeni fimbo kaburi la Mzee Mbowe kwa fedha walizotoa TANU hadi leo hii wengine ni HAPPY-GO-LUCKY mtindo mmoja.

  Hebu kimbieni, tukawachape hawa akina Mzee Mtei, Mzee Makani, tukampige mawe kabisa hata huyu Mbowe Mwenyekiti wa CDM sasa hivi kwa kuwa hawana lolote ni wapuuzi tu.

  Unafikiri watu kama Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pindi wanapotukosea kama jamii tunabaki tunajiumauma tu ovyo huku makwetu Uswahilini unafikiri hatujui tulitendalo; kuna mchango walitoa huko nyuma ambao hakuna thamani ya hela inaweza ikawarudishia leo hii!! Ila ikija suala la hawa MACHEPELE wenye kuturubuni na fedha walizotuibia KIFISADI (umepatia; nilikua namaanisha hao hao RACHEL + JK) wala hatuwaonei aibu hata kidogo!!

  Mwenzangu ukiniuliza mimi hapa kwamba nimechangia kwa kiasi gani cha fedha kukitegemeza chama chochote cha siasa nchini ili kisitegemee watu (ambao ni sharti watoke ukanda fulani katika nchi) jibu langu ambalo ni UKWELI NA UKWELI MTUPU (Mungu niadhibu nianguke nife sasa hivi nikidanganya) si zaidi ya ule mchango wa kadi yangu tu ya uanachama na zaidi huku kuchangia mawazo jinsi gani mambo yaendeshwe kunawirisha chama kwa lengo kuu la KUBORESHA MASLAHI YETU SOOOOTE KAMA UMMA WA TANZANIA bila kujali itikadi zetu.

  Nakuambia kila unaponiona nikichangia hapa jukuani mimi malipo pekee ninayotarajia kutoka CHADEMA ni hilo hapo kwenye wino wa bluu ambapo endapo litakua halizingatiwi kwa Maslahi ya Walalahoi kwa ujumla wetu basi hadi hapo niko tayari kugeuka mbogo kwa mtu yeyote yule ndani ya CDM bila kujali umri wala wadhifa wake ndani ya chama chetu - MINE IS A UNITY OF PURPOSE and NOT a UNITY OF FESTIVITY as at CHADEMA Full Stop!!!

  Kwa umri wa TANU, kama CHADEMA hivi sasa, kilikua kinahitaji msaaada wa wenye moyo na udhati wa kupenda nchi hii bila UFISADI - Shime sana kwa Familia za Mzee Sykes, Mbowe na wengine wachache wa wakati wao huo.

  Nasema hivi kwa sababu mtu huwezi kusema ugali wa mtama ni mbaya sana bila kutufahamisha huo ubaya ulikua ukiulinganisha na nini pembeni mwake. Hebu kachukue hizo picha na ukaziakisi pia kwa TLP, CCM, NCCR-Mageuzi, CUF na kadhalika kisha ukatufahamishe kwamba kwenye maabara yako kisiasa mwenzetu umeona nini??

  Hitimisho langu ni kwamba kwa mtu yeyote asiyejua historia ya jamii yake au taasisi anamojishughulisha wakati wote ni kwamba mtu huyu wala wapi tunakokusudia kwenda wala hana fununu nalo hata chembe isipokua macho yake yooote yanabakia yakiwa yamekodoleka kuhesabu tu Manemane ya hivi sasa na jinsi 'yanavyoendelea kunyesha zenyewe tu kama mvua' toka angani.

  Mwana-CDM mwenzangu, endapo kuna kaukweli wowote utakua umebahatika kuumega toka kwenye haya mawazo binafsi niliyoyaandika basi chonde usikose kunijulisha. Mapambano mema, wont you???
   
 16. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CDM ni chama kikubwa cha upinzani Tanzania, ukiachana na CUF ambao tayari wako na chama tawala. Ili CDM iimarike zaidi, ni vema wadau tuondolewe hofu itokanayo na huo usisi ndo waanzilishi, sisi ndo wenye chama, sisi ndo wenye uchungu na nchi hii na sisi ndo tunajua kila kitu!

  Kwa wenye 'Magamba" tumeona wanaweza kusurvive na kunyosheana vidole kwa baadhi ya watu tuliodhani ni untouchable kwenye chama chao. Swali langu dogo, can CDM survive without Hon. Mbowe and Mzee Mtei?
   
 17. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CDM bila hao kitachanja mbuga Tanzania yote, Mbowe na Mkwewe wanataka chama kibaki na IDENTITY YA KANDA MOJA TU kwa upande wa mamlaka na maamuzi, wa kanda zingine ni abiria ndani ya boti
   
 18. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tuanze kujibu kwa Hoja, panga list ya viongozi wote wa CDM tione kama hilo lipo

  1. M/kiti - K'njaro - mkristo
  2. Makamu M/Kiti - Katavi - muislamu
  3. katibu Mkuu - Arusha - mkristo
  4. Naibu katibu mkuu - Kigoma - muislamu

  nadhani huna hoja hapa na hawa wote sio waanzilishi wa chama
   
 19. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #19
  May 3, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huu uwongo haujadiliki. mtu anayejua Chadema kwa kiwango cha mwanachama wa kawaida mfuatiliaji mzuri wa mambo anajua hilo.
   
 20. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema wananipa raha! Cdm ni basi ndogo lisilo na nafasi, njooni katika luxury bus la ccm linalotembea kanda zote za tanzania
   
Loading...