Supu ya pweza inanimalizia hela nashindwa kuiacha

Za jioni wakuu, supu ya pweza ni maarufu sana Dar es salaam mida ya jioni ambapo tunaona watu wanauza supu kwenye vimeza vyao.

Sasa kitu kinachofanya nije leo ni ulevi wa supu ya pweza aisee nimejitahidi kuacha nimeshindwa yaani kila nikitoka kazini njia ya kwenda nyumbani kuna kibanda cha pweza kama wana dawa vile hawa watu unasema ninywe supu ya mia tatu ,mara unapiga kachori, paap kata mkia wa elfu mbili, weka na prawn puuh elfu tano imeenda.

Nikaamua nipige hesabu kila nikila pweza niandike kwenye google notes aiseee nimekuja kupiga hesabu mwezi december 2023 nimetumia elfu 65600 ukichezesha mwaka mzima kama laki 7 hv jamani si Tv mpya hiii.
Nifanyeje niache huu ulevi wa supu ya mdudu pweza.

Tushee experience walevi wenzangu
Hebu acha ujinga. Kuna siku utasema chakula kinakumalozia fedha. Hii 60,000 ni hela natumia siku moja kwenye bia na washkaji.
 
Chakula kwaajili ya tumbo lako gharama yake haiwezi kukufilisi labda kama hicho chakula kina madhara kwako, maana hiyo siyo pombe wala kilevi chochote ni chakula tu
 
Back
Top Bottom