Suprise iliyobeba maumivu yangu

Suprise iliyobeba maumivu yangu

Pole sana maisha lazima yasonge haijalishi umepata maumiv kiasi gani na vile tumeumbiwa kusahau utasahau utapenda tena
Kweli lakini itanichukua muda .
 
Tatizo wanaume huwa hatutabiriki, mimi naona amefanya poa tuu
 
Sijawahi kutegemea kama ipo siku ningefanyiwa suprise kama hii inshort is hurt inauma sana.

Asee kuna msichana fulani nilikuwa na mahusiano naye nilimpenda sana ila ndo hivyo kigeto geto si mnajua maisha yalivyo.

Alafu msichana ndio kwanza alikuwa kidato cha sita basi mipango kibao akimaliza pepa tu mwenyewe anataka nichukue jiko nimuweke ndani ila kikwazo ilikuwa mimi bhana ukicheki nilikuwa sijaseti mipango yangu fresh.

Basi mzee mwenyewe msichana alivyomaliza pepa alikuwa anasimamia msimamo wake eti nimuoe basi mtoto wa kiume nilikuwa nampa sound tu atulie tulie niweke mambo sawa maana usawa wenyewe wa magu uuh isije siku tukalala njaa na ukicheki ata hela ya posa yenyewe sina.

Basi dogo alionyesha kama kukubali flani hivi zile sound zangu kumbe moyoni ana yake .

Da ile Juzi kati sasa kidume nimeingia facebook niperuzi kidogo nikakuta mtoto kapost picha akiwa na shela juu alafu stutus za kumshukuru Mungu kwa sana kwa kupata mume.

Kiukweli nilistuka niliona labda ni utani ile kumpandia hewani si akaniambia ndio yuko fungate na bwana yake so nisimsumbue tena nimuache na ndoa yake.

Nimeumia sana na siyo kwamba sikuwa na malengo nae ila usawa ndio ulikuwa unakaba ningekuwa na pesa basi ningemuoa kipenzi changu ameniacha na maumivu ya moyo.

Ni bora angesema kuliko kunifanyia suprise kama hiyo, suprise ya kuniumizia moyo wangu, suprise iliyoijaza machozi machoni pangu hakika ni maumivu yasiyovumilika.

Lakini mwisho wa yote namtakia ndoa njema yenye amani lakini akae akijua kwamba kila tone la chozi langu limejaa maumivu makali sana yanayotoka moyoni.

....... itanichukua muda kusahau.
Kamteke
 
Alikuwa hakupendi mkuu....
Kimsingi haupaswi kujuta, zaidi ya kushukuru Mungu kwa kufanya hili mapema.
 
Haukua wako huyo...huwezi jua Mola aliokuepushia.

Ndoa sio rehearsal ujue kwa hiyo usijitie kiherehere cha kuikimbilia kisa binti anafosi
 
The same situation napitia sasa ,nina manzi wa ananielewa sana na mimi namuelewa sana,anataka nimuoe ata kesho ila yeye bado ajamaliza chuo mi nimeshamaliza ka degree kangu sema vyuma bado vimekaza sana kwa upande wangu
 
pambana !tatizo magraduate wengi wanang'ang'ania kuishi dar !hebu nenda hata mikoani nenda hata njombe huko mamufindi huko katafte maisha !toka mjini !
 
Sijawahi kutegemea kama ipo siku ningefanyiwa suprise kama hii inshort is hurt inauma sana.

Asee kuna msichana fulani nilikuwa na mahusiano naye nilimpenda sana ila ndo hivyo kigeto geto si mnajua maisha yalivyo.

Alafu msichana ndio kwanza alikuwa kidato cha sita basi mipango kibao akimaliza pepa tu mwenyewe anataka nichukue jiko nimuweke ndani ila kikwazo ilikuwa mimi bhana ukicheki nilikuwa sijaseti mipango yangu fresh.

Basi mzee mwenyewe msichana alivyomaliza pepa alikuwa anasimamia msimamo wake eti nimuoe basi mtoto wa kiume nilikuwa nampa sound tu atulie tulie niweke mambo sawa maana usawa wenyewe wa magu uuh isije siku tukalala njaa na ukicheki ata hela ya posa yenyewe sina.

Basi dogo alionyesha kama kukubali flani hivi zile sound zangu kumbe moyoni ana yake .

Da ile Juzi kati sasa kidume nimeingia facebook niperuzi kidogo nikakuta mtoto kapost picha akiwa na shela juu alafu stutus za kumshukuru Mungu kwa sana kwa kupata mume.

Kiukweli nilistuka niliona labda ni utani ile kumpandia hewani si akaniambia ndio yuko fungate na bwana yake so nisimsumbue tena nimuache na ndoa yake.

Nimeumia sana na siyo kwamba sikuwa na malengo nae ila usawa ndio ulikuwa unakaba ningekuwa na pesa basi ningemuoa kipenzi changu ameniacha na maumivu ya moyo.

Ni bora angesema kuliko kunifanyia suprise kama hiyo, suprise ya kuniumizia moyo wangu, suprise iliyoijaza machozi machoni pangu hakika ni maumivu yasiyovumilika.

Lakini mwisho wa yote namtakia ndoa njema yenye amani lakini akae akijua kwamba kila tone la chozi langu limejaa maumivu makali sana yanayotoka moyoni.

....... itanichukua muda kusahau.
Vyuma vimekaza hadi waoaji wanaogopa! Ila pole,kafurahia shela atakutafuta siku akwambie amekumic
 
Pole mnoo
Waswahili walisema mwenye kisu kikali ndie mla nyama!!!

Amini hakuwa wako huyo, alikuwa anapita tuu, tulia anza upya!!
 
Back
Top Bottom