Unaweza kuitambua sauti ya Ibilisi katika uchaguzi wa Tanzania wa 2015?
Nani anaweza kuwa juu ya mwenye chama! Unaanzaje kumpinga mwenye chama?
Chacha Wangwe alijaribu kumpinga mwenye Chama akashindwa, Walid Aman Kabourou alijaribu kumpinga mwenye chama akashindwa, Brown Ngwilulupi alijaribu kumpinga mwenye chama akashinwa, Mahimbo Kaoneka alijaribu kumpinga mwenye chama akashindwa, Zitto Zuberi Kabwe na Kitila Mkumbo walijaribu kumpinga mwenye chama wakashindwa, Sasa amekuja Dr. Wilibrod Slaa anajaribu kumpinga mwenye chama. Pengine atashindwa kama wenzake waliojaribu kumpinga mwenye chama huko nyuma.
Kwenye hiki chama kila mwenye mawazo tofauti hutafsiri ama anatumika na CCM, ama anataka kuwa JUU YA CHAMA. Kumbe tatizo ni kwamba ukiwa na mawazo yanayotofautiana na mwenye chama, huko ndo kujaribu kuwa Juu ya Chama. Funzo hapa ni kwamba ILI KUWA CHINI YA CHAMA, NA SIYO JUU YA CHAMA, ni lazima ukubaliane na mwenye chama.
Kujua mantiki ya hoja hii watafute hawa waliojaribu kutofautiana na mwenye chama wakaja kujifunza kwa kuchelewa sana kwamba kupinga mawazo ya mwenye chama ni kuwa juu ya chama. Hawa watakuhakikishia kuwa kumbe hiki chama ni MTU; ni mtu ambaye atakaa tu na wale wanaokubali kuwa chini ya Chama kifikra na kimatendo. Yaani atakaa tu na wale wanaokubali fikara za kwake tu.
Orodha ya watu waliojifunza somo hili kwa kuchelewa sana ni ndefu; ila hii hapa ni orodha ndogo nakutangulizia uwatafute kupata undani: Walid Aman Kabourou, Brown Ngwilulupi, Mahimbo Kaoneka, Chacha Wangwe, Zitto Zuberi Kabwe, Kitila Mkumbo, na orodha ni ndefu. Sasa kaja na huyu mpya Dr. Slaa.
Hivi hili tatizo la kuwa juu ya chama manaake nini? Mbona mi naona kama vile ni tatizo la kuwa juu ya mtu?
Kuna sauti mbili katika uchaguzi wa mwaka 2015 Tanzania. Kuna Sauti ya Ibilisi na sauti ya Roho Mtakatifu. Na mara kwa mara sauti ya Ibilisi huwa kubwa zaidi kuliko sauti ya Roho Mtakatifu. Sililiza vizuri sauti hizi kuhusu watu kuwa juu ya chama utaitambua haraka sana sauti ya ibilisi inatoka wapi.
Tunaye ibilisi na roho mtakatifu miongoni mwetu kwenye uchaguzi huu wa Tanzania wa 2015. Mimi nimeshamtambua ni nani huyu mwenye sauti kuu, mwakilishi wa Ibilisi; na ni nani huyu mwenye sauti iliyofifia sana, huyu ambaye kaleta mbele yako sauti ya roho mtakatifu.... Mkatae Ibilisi na hila zake; hata pale anapokuja na Biblia mkononi mwake.
Hebu isome hii picha uniambie wewe unaionaje. Je hii ni sauti ya Roho Mtakatifu?
