Supana mkononi halafu kila mtu fundi..

Supana mkononi halafu kila mtu fundi..

Tatizo si gari mkuu sie wenye karakana ni tatizo namba moja amini tunakubali kuendeshwa na dereva kichwa maji
 
Tilipu shamba, tilipu kwa fundi
Fundi mchundo
Fundi breki
Fundi umeme
Fundi injini
Fundi bodi(kuchomea)
Na kila fundi ana saidia wake... Maarufu kama nyoka
Gari limechakazwa na mafundi hawa... Limegeuzwa kichwa cha mwendawazimu... Kila likionekana karakana kila fundi na supana yake mkononi hulivamia, wanasema kupiga mande
Si fundi mchundo wala fundi kuchomea, si saidia fundi ama mwanafunzi wa ufundi... Wote hulizingira kila mtu akitaka kutengeneza chake... Hata vile vizima hulazimishwa uharibifu ili vitengenezwe.. Watu waingize siku.... Shida iliyopo ni mpangilio wa kazi
Nani atengeneze nini
Nani amsaidie nani
Nani afungue nini
Nani afunge nini...
Mwisho wa siku boriti moja inafunguliwa na huyu kisha inafungwa na yule halafu anakuja mwingine anaifungua tena....
Kukichwa mafundi wanatawanyika hoi bila kutengeneza gari kikamilifu....
Kukipambazuka dereva analipeleka gari shamba likaingize siku.. Likifanikiwa kurudi litafikia karakana... Mapato yote ya siku yataishia kwa mafundi
Dereva kakosa mpangilio
Mafundi wote wamekosa mpangilio
Saidia fundi wote mulemule
Hata wanafunzi pia....
Kilichobaki ni kila mtu na supana lake... Na ujuzi wake, na ufundi wake na ujuaji wake....
Hatuendi mbele tunarudi nyuma... Dereva anataka kuwa saidia fundi... Mwanafunzi anataka kuwa fundi mkuu.... Fundi mchundo anasema anajua makanika ya makinikia...
niliwahi kumuona mtu akijaribu kuivuta semitrela kwa guta
Niliwahi kumuona mtu akijaribu kujitishwa jabali
Ngoja nikawahi sinema ya kesho.. Gari halijarudi shamba na dereva hajasema lolote mpaka sasa...... Labda anaendesha... Halafu njia ina makolongo.. Leo ilikuwa ni kwenda kubeba choroko za koloshoView attachment 926148
Kichekesho zaidi Dereva na hao mafundi wake wote NgagariPoa.... Full mikwala

Yaani gari likiwa gereji utacheka ufe....mara Konda analalama..kwa dereva "oh tulipakia magasho ndio mana gari halina spidi"

Mara, mzigo wa Korosho hauna faida ushushwe.. Mara Tumekusanya nauli ya kutosha... Mara Tajiri mwenye mzigo sijiu kapotea, yaaani full Komedi.

Wacha tufungulie tu Koki Koki Koki la Maji taka mana mafundi wamechafuka, Dereva kachafuka, hakuna tena wa kuwachafuaa....

Nataja ktk list ya kwanza, wa kwanza kuchafuka ni Konda, tena kamchfua mpaka Dereva na kama Konda akibisha basi niko radhi kutembea kwa miguu na nisipande gari....
 
eti ni ngangaripoa.... Ila konda bwana... Ngoja niishie hapa
 
Tilipu shamba, tilipu kwa fundi
Fundi mchundo
Fundi breki
Fundi umeme
Fundi injini
Fundi bodi(kuchomea)
Na kila fundi ana saidia wake... Maarufu kama nyoka
Gari limechakazwa na mafundi hawa... Limegeuzwa kichwa cha mwendawazimu... Kila likionekana karakana kila fundi na supana yake mkononi hulivamia, wanasema kupiga mande
Si fundi mchundo wala fundi kuchomea, si saidia fundi ama mwanafunzi wa ufundi... Wote hulizingira kila mtu akitaka kutengeneza chake... Hata vile vizima hulazimishwa uharibifu ili vitengenezwe.. Watu waingize siku.... Shida iliyopo ni mpangilio wa kazi
Nani atengeneze nini
Nani amsaidie nani
Nani afungue nini
Nani afunge nini...
Mwisho wa siku boriti moja inafunguliwa na huyu kisha inafungwa na yule halafu anakuja mwingine anaifungua tena....
Kukichwa mafundi wanatawanyika hoi bila kutengeneza gari kikamilifu....
Kukipambazuka dereva analipeleka gari shamba likaingize siku.. Likifanikiwa kurudi litafikia karakana... Mapato yote ya siku yataishia kwa mafundi
Dereva kakosa mpangilio
Mafundi wote wamekosa mpangilio
Saidia fundi wote mulemule
Hata wanafunzi pia....
Kilichobaki ni kila mtu na supana lake... Na ujuzi wake, na ufundi wake na ujuaji wake....
Hatuendi mbele tunarudi nyuma... Dereva anataka kuwa saidia fundi... Mwanafunzi anataka kuwa fundi mkuu.... Fundi mchundo anasema anajua makanika ya makinikia...
niliwahi kumuona mtu akijaribu kuivuta semitrela kwa guta
Niliwahi kumuona mtu akijaribu kujitishwa jabali
Ngoja nikawahi sinema ya kesho.. Gari halijarudi shamba na dereva hajasema lolote mpaka sasa...... Labda anaendesha... Halafu njia ina makolongo.. Leo ilikuwa ni kwenda kubeba choroko za koloshoView attachment 926148
 
Halitamfia dereva peke yake,bali pia linaumiza mafundi,abiria na hata wafanyakazi wenyewe wa hilo gari wanaumizwa. Likifa,litawafia wote,hakuna atakayepona.
Hahahaha sasa hili gari kama lina mafundi wengi hivi mwisho wa siku si litaja mfia dereva mazima.
 
Kuwa na Dira kwenye swala lolote maishani mwako ni swala muhimu sana, hata kwenye boma lako...Si swala la mchezo mchezo, yetu macho, na ndio kwanza 3yrs, bado 7yrs zingine! Inatisha...
 
.
IMG-20181108-WA0064.jpeg
 
Uko vizuri Sana
Mshana Jr
Hakika Dreva huyu
Analiendesha gari vibaya
Trip moja na kupelekwa kwa fundi.
 
Mkuu Mshana Jr hii gari huwa haisubiri kufika karakana! Huku ikitembea huku Mafundi nao wanaendelea na kazi,kuna mmoja anapiga Fill pump,mwingine anagongea terminal ya betri,halafu kuna mwingine namuona ameweka sikio kwenye engine!anasikilizia mlio wake,ngoja tuone anataka kufanyaje
240624_0c5ac241927e945569bed885d028501e.png
 
Back
Top Bottom