Tilipu shamba, tilipu kwa fundi
Fundi mchundo
Fundi breki
Fundi umeme
Fundi injini
Fundi bodi(kuchomea)
Na kila fundi ana saidia wake... Maarufu kama nyoka
Gari limechakazwa na mafundi hawa... Limegeuzwa kichwa cha mwendawazimu... Kila likionekana karakana kila fundi na supana yake mkononi hulivamia, wanasema kupiga mande
Si fundi mchundo wala fundi kuchomea, si saidia fundi ama mwanafunzi wa ufundi... Wote hulizingira kila mtu akitaka kutengeneza chake... Hata vile vizima hulazimishwa uharibifu ili vitengenezwe.. Watu waingize siku.... Shida iliyopo ni mpangilio wa kazi
Nani atengeneze nini
Nani amsaidie nani
Nani afungue nini
Nani afunge nini...
Mwisho wa siku boriti moja inafunguliwa na huyu kisha inafungwa na yule halafu anakuja mwingine anaifungua tena....
Kukichwa mafundi wanatawanyika hoi bila kutengeneza gari kikamilifu....
Kukipambazuka dereva analipeleka gari shamba likaingize siku.. Likifanikiwa kurudi litafikia karakana... Mapato yote ya siku yataishia kwa mafundi
Dereva kakosa mpangilio
Mafundi wote wamekosa mpangilio
Saidia fundi wote mulemule
Hata wanafunzi pia....
Kilichobaki ni kila mtu na supana lake... Na ujuzi wake, na ufundi wake na ujuaji wake....
Hatuendi mbele tunarudi nyuma... Dereva anataka kuwa saidia fundi... Mwanafunzi anataka kuwa fundi mkuu.... Fundi mchundo anasema anajua makanika ya makinikia...
niliwahi kumuona mtu akijaribu kuivuta semitrela kwa guta
Niliwahi kumuona mtu akijaribu kujitishwa jabali
Ngoja nikawahi sinema ya kesho.. Gari halijarudi shamba na dereva hajasema lolote mpaka sasa...... Labda anaendesha... Halafu njia ina makolongo.. Leo ilikuwa ni kwenda kubeba choroko za kolosho





View attachment 926148