ni miaka kama miwili imepita. Nakumbuka nilianza naye uhusiano nikiwa mwaka wa nne na yeye mwaka wa mwisho chuoni kwao. Kabla ya hapo nilikuwa karibu naye kwa miaka kama miwili nyuma. Akamaliza chuo akaniacha nikiwa mwaka wa tano ili niweze kuhitimu masomo yangu. Kwa muda ambao alikuwa anasubiri ajira alikaa nyumbani kwao kwani hakupata sehemu ya kujishikiza. January ajira zikatoka kapangiwa kigoma mi niko dar. Nilimwambia hamna noma kwani mawasiliano na usafiri si upo, we nenda. Akaenda kuripoti na kuanza kazi(ni mwalimu). Tuliendelea na mawasiliano huku mi nikiendelea kupiga shule ili nimalize nikafanye internship nioe kabisa. Niliwahi kumwambia nyuma kwamba kuoa kwangu ni mpaka niwe na uhakika wa kwamba tutakula na kulala kwa amani. Nikiwa naendelea na shule bahati mbaya nikaangukia mikononi mwa walaji wa vichwa(muhas wanajua hili) nikaliwa kozi moja. Loh! Sikuwahi kupata sup hivyo nilichanganyikiwa lakini nilijipa moyo kwani sikuwa wa kwanza. Na kurudia ni until when next offered meani ntarudia kozi na madogo. Nikajipanga nikamwambia mwenzangu akaniuliza, ko unagraduate lini? Nikamwambia, mwakani.. Akanambia, ko kuna mwaka mmoja mbele? Nikajua hapa mwenzangu anapiga mahesabu ya kuolewa, nikamjibu ndiyo. Kozi ilikuwa kama wiki 12, semister ilivyoanza nami nikaanza, loh.! Matatizo yakaanza, mawasiliano hovyo, akiongea mkato mkato yaani ikawa ni balaa. Alipata likizo akagoma kuja dar bila sababu. Katika kufuatilia kuna jamaa yangu wa karibu akanambia kuna jamaa mwingine anabambia. Nikaona hamna shida nikapiga chini na kuendelea na maisha yangu na nashukuru Mungu ile kozi niliipunch. Mpaka leo wanawake nawaona kama watu wanaotaka mafanikio tu bila kujua kwamba kuna visiki humo njiani.