Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 348
- 847
Kijana mwenye asili ya India Rish Sunak hatimae amefanikiwa kuwa kiongozi wa Chama cha Conservative (Torry party) nafasi itakayo mfanya kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya kuidhinishwa na kuteuliwa na mfalme Charles lll.
Sunak mwenye Miaka 42 ambaye ni mbunge wa Richmond (York) ni Waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza asie na asili ya Uingereza ya moja kwa moja, wazazi wake waliwahi kuishi Kenya na Tanzania kabla ya kuhamia Uingereza.
Sunak alifunga ndoa mwaka 2009 na mwanadada Akshata Murty ambae ni Mwanamama tajiri ambae amerithi utajiri kutoka kwa wazazi wake, kwasababu hiyo imemfanya Rushi Sunak kuwa mbunge tajiri zaidi Uingereza.
Utajiri huo unatokana na mkewe ambae ni mtoto wa billionaire N. R. Narayana Murthy, Sunak and Murty ni matajiri wa 222 katika nchi ya Uingereza, utajiri wao wa jumla ni paund milioni £730.
Sunak alizaliwa huko Southampton, huku wazazi wake wakitokea Punjabi India na kuhamia Uingereza wakitokea Afrika mashariki miaka ya 1960s.
Sunak alisoma Oxford na Stanford ambavyo ni vyuo vikuu bora duniani, ni Mara ya Kwanza Uingereza inapata Waziri mkuu asiye Mkristu.
Tarehe 23 Oktoba Sunak alitangaza nia yake ya kugombea Uongozi wa chama, mapema leo baada ya Boris Johnson kujiondoa kwenye kinyang'anyiro baada ya kupata waugwaji mkono wachache na Mordaunt kujiondoa, Sunak alitangazwa kuwa Kiongozi mpya wa Chama cha Conservative nafasi inayomfanya kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
Anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza mwenye asili ya Asia, na anakuwa Waziri mkuu wa 79 wa Uingereza.
Ndimi Comred Mbwana Allyamtu CMCA