Sumaye: Vyuma havijakaza, bali vimepinda

Sumaye: Vyuma havijakaza, bali vimepinda

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema wananchi kama wataendelea kuichagua CCM, watarajie hali ngumu ya maisha.
Sumaye akihutubia mkutano wa kampeni wa Chadema wa uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga leo, alisema: “Sasa hivi sio vyuma vimekaza tu bali vimepinda na hapo bado.”


“Kama tutaendelea na hicho Chama Cha Mapinduzi hii hali tunayoisema mbaya hii ni trela tu, sinema bado.”
mbaya.
“Tusipochagua chama cha upinzani tutazidi kuvumilia, mimi nilikuwa Waziri Mkuu lakini nilipoona tunakowapeleka Watanzania siko nilihamia upande wa pili ili kuwatumikia wananchi,” alisema.


Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani aliwataka wananchi wa jimbo hilo wamchague Asia Msangi kupitia chama hicho ili uwe mwanzo wa dalili ya 2020 upinzani kuchukua nchi.


Naye Mwenyekiti Baraza la Wazee Chadema, Hashim Juma alisema: “Imefika muda CCM ikae pembeni iwapishe waishike nchi.
“Wacha wao waende Dodoma, ila watuachie Ikulu yetu, Chadema tukichukua nchi tutarudi Dar es Salaam hapa ndiyo kwenye kila kitu,” alisema.
 
Huyo sumaye arudishe kwanza pesa zetu za tvt ( tbc)
 
Huyu mzee Sumaye yaani ! Hivi miaka yake kumi ya uwaziri mkuu ? Sijui hata nisemeje, halafu leo ndio anaponda chama tawala... I see !
 
Mwenyekiti wa baraza la wazee chadema ! Du ! Amejaa jazba na hasira hatari ! Anatamani muungano ufe hata leo hii...sijui hata walimpaje uenyekiti huo la! Anamlaumu mh. Rais kumuachilia Babu Seya wakati mgombea wake wa nafasi ile 2015 aliahidi kufanya hivyo pia ! Sijui huwa hawana kumbukumbu watu hawa jamani ?
 
Je Chadema inaamini kuwa kuhamia dodoma sio sahihi?
Mambo ya chadema nenda ufipa kaulize!,
Kwa mtizamo wangu kuhamia dodoma ni jambo jema sana ila lifanywe taratibu siyo kufanya haraka haraka kuna gharimu sana. Mfano m/rais alihamia dodoma kwa mbwembwe mbele ya makamera baada ya makamera kuzimwa katembelea rivasi kurudi dar na ofisi yake ipo dar for 98%
 
Mambo ya chadema nenda ufipa kaulize!,
Kwa mtizamo wangu kuhamia dodoma ni jambo jema sana ila lifanywe taratibu siyo kufanya haraka haraka kuna gharimu sana. Mfano m/rais alihamia dodoma kwa mbwembwe mbele ya makamera baada ya makamera kuzimwa katembelea rivasi kurudi dar na ofisi yake ipo dar for 98%
Hoja ya kuhamia dodoma ilianza lini?kwa nini useme ina uharaka?
 
yaani kwa akili yangu timamu nipange foleni kupigia kura yangu mgombea anayenadiwa na Sumaye? ama lowassa? walioitia madoa ccm ndo hawahawa leo wanaiharibu chadema, Ufipa endeleeni kuwakumbatia chama kinakufa kibudu.
 
Ilianza tokea awamu ya kwanza ilitakiwa itekelezwe kwa awamu na ndo lilikuwa azimio la nyerere lakin awm zilizofuata hazikuliendeleza jambo hilo,Sasa Magufuli kafanya vyema sana ila liende kwa awamu awamu si kulazimisha kwani hata kwenye bajeti haikutengwa pesa kwa ajili hiyo sasa yeye anachota pesa za kununua dawa anaitumia kwenye kuhamia dodoma.Tuhamie dodoma ila isituathiri sana.
una ushahidi wa fedha ya dawa iliyochotwa kwa ajili ya kuhamia dodoma?
 
Back
Top Bottom