Sumaye: Upinzani kugumu kuliko CCM

Sumaye: Upinzani kugumu kuliko CCM

Msemajiukweli habari hii umeileta kama faraja ya jinsi mtu akijiunga upi zani atataabika. Ila ukweli ni huu, viongozi walio wengi huwa wanabweteka sana wanapokuwa madarakani, huwa wanaishi maisha ya upendeleo uliopitiliza. Wakipanda majukwaani utawasikia watu wafanye kazi na sio kutegemea serekali!!! Huyo mtu anayezungumza hayo unakuta anapata mshahara tena mzuri, ila kila kitu anapata bure. Ngoja sasa atoke madarakani akutane na yale maisha aliyokuwa anawahubiria wenzake, mbona utamuonea huruma.

Kwa mfano hii sheria ya kuendelea kuwalipa marais na mawaziri wakuu wastaafu maisha yao yote ni upendeleo wa wazi kabisa. Iweje mtu aliyekuwa anahimiza wenzake wafanye kazi aendelee kulipwa muda wote baada ya kustaafu wakati mwingine alipokuwa madarakani wala hakuhakikisha wastaafu wengine wanalipwa stahiki zao kwa wakati? Anacholalamikia Sumaye leo ndio kile alikiona sawa wapinzani kukutana nacho alipokuwa ccm/madarakani. Na kilio hicho ndio kitakuja kusikika kwa wanaccm wengi pindi wakitoka madarakani na wengine wakafanya kwa mtindo huuhuu wanaofanyia wanaccm wapinzani wao.
Umeeleza vizuri sana. Upinzani sio kabila kuwa ukizaliwa Mgogo huwezi kujibadili na kuwa Mhehe.
Sumaye ametoa neno la kutafakarisha kwa wote, maana Mtawala wa leo ndio mpinzani wa kesho. Jee ccm wako radhi kujikuta wanakumbana na adha wapatazo wapinzani wao watakapo kuwa wapinzani 2020?
 
Sumaye rudi ccm ,biashara na DJ huiwezi. Bavicha watakuita msaliti soon.

Stay tuned
 
Nilijua tu ile ishu ya kusukumiwa Kibaha imemtachi...Baba wa watu ameisubiri fursa ametoa la moyoni.
 
tupe tafsi yako mkuu!
maana unapingana na tafsiri zenye reference kabisa
Ninashukuru kwa kumuuliza swali kama langu.

Kuna baadhi ya watu wanafahamu kusema hapana lakini ukimuuliza kwa nini hapana, wanakuwa hawana jibu/majibu ya kuibeba hapana yao.
 
Sad story kuona MBA ya Harvard going to west, kweli kuishi ni kujifinza
 
Kwa taarifa yenu Mh Sumaye si mwanasiasa.

Ila ashukuru Mungu tu kuwa amewahi kuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10.
Mkuu una maana gani?

Naomba unifafanulie vizuri kwa sababu pamoja na kustaafu Uwaziri Mkuu lakini bado anataka awe Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa.
 
Mkuu una maana gani?

Naomba unifafanulie vizuri kwa sababu pamoja na kustaafu Uwaziri Mkuu lakini bado anataka awe Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa.
Mwanasiasa halazimishi siasa Bali utamjua kwa falsa zake,imani yake,msimamo wako,itikadi zake na mwisho ni maono. Yake kwa Taifa.
 
Mwanasiasa halazishi siasa Bali utamjua kwa falsa zake,imani yake,msimamo wako,itikadi zake na mwisho ni maono. Yake kwa Taifa.
Ninashukuru kwa kunipa ufafanuzi zaidi.
 
When you rewind the tape up to Saturday, 22nd August 2015 utamsikia Sumaye akisema amejiunga upinzani ili kuwafundisha wapinzani jinsi ya kuendesha siasa na serikali huku akiwasifu Dk. Slaa na Prof. Lipumba kuwa ni moja kati ya waliousimamisha upinzani vyema.

Dk Slaa has gone and Prof. Lipumba political future has been hanging by a thread since the day Sumaye and Lowassa left CCM to join CHADEMA.

Fastforward mpaka Sunday 9th October 2016 tunamsikia akitoa maneno ambayo ukiyachunguza yanaonyesha aliokuwa anadhani atawafundisha kazi kwa sasa ndio wanaomfundisha kazi ya uvumilivu.

Maelezo ya Mzee wangu Sumaye yanaonyesha yuko katika deep regret and remorse. The journey and new political adventure has cost him something emotionally or financially and led to a punishment or undesirable result.

Haishangazi kwa sasa tunasikia anataka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Mkoa.

From Tanzania Prime Minister to CHADEMA Regional Chairman. Hii ni ishara kamili ya frustration for unfinished political business.

Tusije kushangaa kusikia amerudi CCM!

Siasa za Tanzania ni majanga!
Tatazo la Watanzania ni hilo uñalowaza wewe. Tunaamini kwamba mtu akifikia ngazi ya juu serikalini hana hadhi ya kutumikia tenà uma kwa ngazi zingine. Huu ni upofu na udumavu wa mawazo. Kule Urusi, Putin ametumikia Urais na Uwaziri Mkuu kwa nyakati tofauti. Hata Israel pia. Sumaye hakuwa kuongoza kwenye Ccm{ na hata kama angewahi), na hakuna kitu chochote kinachomzuia kushika wadhifa wa ngazi yoyote ile. Wewe kwani unaona kama ameisha au anajidhalilisha. Huu ni upofu wa kupindukia. Kama wewe unawaza negatively, usitake watu wengine wakawaza kama wewe, wapo watakaowaza positively.
 
Ataiota sana CCM,kutoka ligi kuu ya Vodacom,hadi kombe la Mbuzi uwanja wa Kinesi.
Inabidi avumilie tu kwa sababu maji aliyafulia nguo na sasa hana budi kuyaoga.

Hata hivyo kila mwezi analipwa zaidi ya asilimia 80 ya mshahara wake wa Uwaziri Mkuu.
 
Kwa nini anasema haya maneno kwa sasa?

Ina maana yeye alitegemea mteremko ndio maana akajiunga CHADEMA?

Hadhani kama kuongea maneno hayo ni kujaribu kuwatisha wale ambao wanapenda kuingia upinzani?

Kuna kina Mzee Mtei, Ndesamburo, Bob Makani etc ambao walikuwa serikalini na kwenye biashara hawakuwahi kutoa maneno yanayoonyesha kama kujuta au kutoa onyo kwa watu wanaofikiria kujiunga Upinzani.

Tukubali tu kuwa maneno ya Mzee Sumaye yana chembechembe ya regrets and remorse.

Mimi ningependa kuuchukulia huu kama mtazamo wako...binafsi......inawezekana isiwe vile anavyowaza yeye mwenyewe....
 
Kuwa na akili japo kidogo! Kwa Vyama gani vya upinzani tulivyonavyo vyenye uwezo wa kwenda Ikulu? Wagombea wenyewe wa kuokoteza toka CCM tena waliochujwa na kuonekana hawafai? Fair ground! Ilitokea wapi MTU anayetaka kukupindua ukampa silaha akumalize??? Wapi hiyo??? Acha ujinga wewe!
Unaonaje kama tutafuta mfumo wa vyama vingi?
Hilo halitasaidia CCM kuwatawala na kuwagawia umasikini wadanganyika kwa mwendo kasi zaidi?
Nimefurahi umekiri kwamba hakuna "fair playing ground" kwa vyama vya siasa Tanzania. CCM inapingwa mbeleko.
 
80% ya Watanzania walitaka Chama kimoja. Siyo kukiri kwangu!
 
Back
Top Bottom