Sumaye: Upinzani kugumu kuliko CCM

Sumaye: Upinzani kugumu kuliko CCM

Maelezo yake yanashangaza hasa kutokana na wakati ambao ameamua kutasema.

Msemajiukweli habari hii umeileta kama faraja ya jinsi mtu akijiunga upi zani atataabika. Ila ukweli ni huu, viongozi walio wengi huwa wanabweteka sana wanapokuwa madarakani, huwa wanaishi maisha ya upendeleo uliopitiliza. Wakipanda majukwaani utawasikia watu wafanye kazi na sio kutegemea serekali!!! Huyo mtu anayezungumza hayo unakuta anapata mshahara tena mzuri, ila kila kitu anapata bure. Ngoja sasa atoke madarakani akutane na yale maisha aliyokuwa anawahubiria wenzake, mbona utamuonea huruma.

Kwa mfano hii sheria ya kuendelea kuwalipa marais na mawaziri wakuu wastaafu maisha yao yote ni upendeleo wa wazi kabisa. Iweje mtu aliyekuwa anahimiza wenzake wafanye kazi aendelee kulipwa muda wote baada ya kustaafu wakati mwingine alipokuwa madarakani wala hakuhakikisha wastaafu wengine wanalipwa stahiki zao kwa wakati? Anacholalamikia Sumaye leo ndio kile alikiona sawa wapinzani kukutana nacho alipokuwa ccm/madarakani. Na kilio hicho ndio kitakuja kusikika kwa wanaccm wengi pindi wakitoka madarakani na wengine wakafanya kwa mtindo huuhuu wanaofanyia wanaccm wapinzani wao.
 
Huwa wanapewa kihalali kabisa na ana hati za miaka 99 issue ni kuwa wameacha pori tu hawajaendeleza hata! Mfano Sumaye ana heka 30 pale Mabwe Pande mjini pale! Alitaka kujenga UNIV kwa mwendo huu sio rahisi hata!! Wafadhili hana wana uwezo kujenga mwenyewe hana! Sasa atakuja kupata lini wafadhili?
Kama waliyapora kwa kutumia nafasi zao walipokuwa madarakani acha walipe sasa! Ila kama waliyapata kihalali na wanaporwa kiuonevu ntawaonea huruma!
 
Sumaye alikaaa miaka 10 mfululizo kama waziri mkuu,anajua mengi ndani ya chama na serikali,na baadae aliingia darasani kuongeza elimu.Tuseme hajapungukiwa fedha labda anataka siasa za ushindani,kitu ambacho ni kigumu kupatikana,lakini kajaribu.
 
tupe tafsi yako mkuu!
maana unapingana na tafsiri zenye reference kabisa
Mtu anapoelezea matatizo/changamoto anayokutana nayo ktk shughuli anayofanya haimaanishi kua haitaki/ kaichoka ama anawakatisha tamaa wengine, No lengo ni kuelezea kua unapokusudia kufanya jambo hili basi uvumilivu ni jambo muhimu, alichozungumza mheshimiwa Sumaye ni kweli na hasa upinzani ktk serikali za kiafrika ccm ikiwemo unahitaji uvumilivu Mkubwa maana humo wapo hawa jamaa waitwa PT (wazee wa intelejesia), wao wamekua wapangaji wa ratiba za shughuli za vyama vya upinzani, Wapo wengine wemejiongezea madaraka, wameona kusajili tu vyama haitoshi bora pia wawe washauri wa vyama basi ni shida kuendesha upinzani Africa ( Tz ) bila uwepo wa uvumilivu.
 
Kwani kuna mtu amewahi kuwahoji Sumaye na mwenzie Lowasa kuhusu kasi zao za CCM?

Je wamewahi kuzichana hadharani kuthibitisha kwamba wao hawako CCM milele?

Sumaye na Lowasa ni sehemu ya "establishment" ya nchi hii na watabakia kuwa hivyohivyo hadi wanajikongoja.

Waendelee kuwadanganya haohao na ndiyo maana mzee Mkapa akawaambia hao wanaodanganywa kuwa ni wapumbavu na malofa, alikuwa na maana yake.
 
Mtoa mada ameeleza Vema. Upinzani kwisha kazi mpaka waliokimbilia huko wanajutaaaaa kuuparamiaaa!
Fikiri upya upinzani hauwezi kufa bila mabadiliko ya sheria na katiba usjindanye kwa kuwaza negative, Mrema mguu mmoja TLP mwingine CCM haina maana kua TLP imekufa wapo wengine wataendeleza.
 
Kumbe una mawazo mgando pamoja na kuwa umekwenda Shule. Umeshindwa kumuelewa amesema nini Sumaye mpaka utoe tafsiri mbovu kiasi hicho?
Nami nimeshangaa sana, haya ni maneno ya kujengana na kutiana moyo ili kufikia lengo na sioni kukata tamaa hapa
 
We ndo unashangaza! Loh!! Unaubongo saizi ya njegere.

Tatizo lenu mnajifanya mnajua sana wakati hamjui kitu chochote Sasa ulitaka sumaye afanye kazi gani? Awe anakuja kukulimia kwako?
 
Mtoa mada ameeleza Vema. Upinzani kwisha kazi mpaka waliokimbilia huko wanajutaaaaa kuuparamiaaa!
Mimi nafikiri mada imeweka wazi tu unafiki wa CCM na serikali zilizoongozwa na CCM kukubali kuanzisha mfumo wa siasa wa vyama vingi na siasa za ushindani wakati katika uhalisia wanafanya kinyume, wanachukulia vyama vya upinzani ni "ukoma", ni uadui. Tena inatumia vyombo vya dola na taasisi za dola kupiga vita upinzani.

Kinachotakiwa ni "fair playing field" ili vyama vishindane kisera kwa faida ya wadanganyika.
 
Kuwa mpinzani ni lazim uwe mvumilivu,hekima,busara na kutumia akili nyingi.
Kwanini nasema hivi,sababu ni chama tawala hakifanyi kazi zozote. Chama tawala kinategemea serikali ili kiweze kujitangaza na kujipambanua.
Mfano kutumia polisi,wakuu wa wilaya ma mikoa,watendaji wa mashirika na wizara. Hapa Chama tawala ata wakilala hawana shida kwasababu wao wataenda kuchukua maelekezo ya vitu vilivyotendeka.
Kwa upande wa upinzani ni lazima uvuje jasho na utumie akili ili uweze kufanikisha jambo,mfano kukimbizana mahakamani,kupigwa virungu na mapolisi wakati viongozi wa chama tawala hawapati hayo maswaibu.
Kwahiyo mnavyosema Sumaye anajutia sio kweli ila anaeleza hali ya upinzani jinsi gani unavyotakiwa kupambana.
 
Mimi nafikiri mada imeweka wazi tu unafiki wa CCM na serikali zilizoongozwa na CCM kukubali kuanzisha mfumo wa siasa wa vyama vingi na siasa za ushindani wakati katika uhalisia wanafanya kinyume, wanachukulia vyama vya upinzani ni "ukoma", ni uadui. Tena inatumia vyombo vya dola na taasisi za dola kupiga vita upinzani.

Kinachotakiwa ni "fair playing field" ili vyama vishindane kisera kwa faida ya wadanganyika.
Kuwa na akili japo kidogo! Kwa Vyama gani vya upinzani tulivyonavyo vyenye uwezo wa kwenda Ikulu? Wagombea wenyewe wa kuokoteza toka CCM tena waliochujwa na kuonekana hawafai? Fair ground! Ilitokea wapi MTU anayetaka kukupindua ukampa silaha akumalize??? Wapi hiyo??? Acha ujinga wewe!
 
Msemajiukweli habari hii umeileta kama faraja ya jinsi mtu akijiunga upi zani atataabika. Ila ukweli ni huu, viongozi walio wengi huwa wanabweteka sana wanapokuwa madarakani, huwa wanaishi maisha ya upendeleo uliopitiliza. Wakipanda majukwaani utawasikia watu wafanye kazi na sio kutegemea serekali!!! Huyo mtu anayezungumza hayo unakuta anapata mshahara tena mzuri, ila kila kitu anapata bure. Ngoja sasa atoke madarakani akutane na yale maisha aliyokuwa anawahubiria wenzake, mbona utamuonea huruma.

Kwa mfano hii sheria ya kuendelea kuwalipa marais na mawaziri wakuu wastaafu maisha yao yote ni upendeleo wa wazi kabisa. Iweje mtu aliyekuwa anahimiza wenzake wafanye kazi aendelee kulipwa muda wote baada ya kustaafu wakati mwingine alipokuwa madarakani wala hakuhakikisha wastaafu wengine wanalipwa stahiki zao kwa wakati? Anacholalamikia Sumaye leo ndio kile alikiona sawa wapinzani kukutana nacho alipokuwa ccm/madarakani. Na kilio hicho ndio kitakuja kusikika kwa wanaccm wengi pindi wakitoka madarakani na wengine wakafanya kwa mtindo huuhuu wanaofanyia wanaccm wapinzani wao.
Mkuu tindo

Tukubaliane tu kuwa hii dunia haina usawa.

Mtazamo wako kama wangu lakini mitazamo yetu haiwezi kufanya kazi katika mazingira ya kidunia.

Kuna watu kama Sumaye ambao ni wastaafu bado wanapata zaidi asilimia 80 ya uliokuwa mshahara wao na hapo hapo wamepewa walinzi na usafiri.
 
Back
Top Bottom