William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
wewe uliyeanzisha thread ya vakesheni ya issa michuzi ulikuwa unamuonea wivu,husuda,majungu,gere au kijicho?
Hukujua kama michuzi analipa kodi na kutoa zawadi kwa watanzania?
Katizame comments kwenye michuzi blog juu ya topic yako ya kijicho kwa michuzi.
Kama sumaye alikuwa hana ugonjwa wa kiasi hicho kwanini alipelekwa ulaya na kutumia kodi zetu kwenye mahubiri ya kidini? Lazima kuna walinzi wanaolipwa kwa kodi zetu wameongozana nae.
Au baada ya kumaliza check up arudi nyumbani kwani lazima awe anaishi hotelini akiwa uingereza na chumba chake pekee yake hakipungui pounds elfu mbili kwa siku,bado wapishi na walinzi.huu ni utapeli wa kodi za wananchi.
Kah! Wewe mwenyewe umesema amekwenda kwa medical check up, na siyo kwamba amekwenda kulazwa hosp kutibiwa, kuna sababu gani ya yeye kutokwenda kwenye nyumba ya ibada kumshukuru Mungu wake kwa yote aliyomjalia? Na je, kama angeonekana kwenye Nght Clubs ingekuwa vipi? Jamani huyu ni Waziri mkuu mstaafu ambaye pension pamoja ma mafao yake mengine yamewekwa kisheria. Dr. Mwakyembe Kutibiwa Muhimbili hakumaanishi kwamba anabaniwa. Tumeshuhudia watu wengi tu wakiwemo wabunge wakipelekwa nje pale umuhimu wa kufanya hivyo unakuwepo, kwanini kwa Sumaye iwe issue! Au ni kwa kuonekania Kanisani?
Unafiki unao wewe kumbe ulijua kuwa Sumaye anatumbua pesa zetu za kodi hukusema,ukaona michuzi ambaye ni mtoto wa kimasikini.pia ujue kuwa Sumaye ni katika mawaziri mafisadi hahitaji kutuibia tena na per de em za ujanja ujanja kama hizi.swali amekwenda kutibiwa au kuhubiri?Huu ni unafiki, Sumaye si mtu bali Michuzi ndio mtu, Sumaye ndio anatumia pesa za walipa kodi Michuzi hatumii sio.
Acheni double standards.
Unafiki unao wewe kumbe ulijua kuwa Sumaye anatumbua pesa zetu za kodi hukusema,ukaona michuzi ambaye ni mtoto wa kimasikini.pia ujue kuwa Sumaye ni katika mawaziri mafisadi hahitaji kutuibia tena na per de em za ujanja ujanja kama hizi.swali amekwenda kutibiwa au kuhubiri?
sumaye alikuja kuangalia afya yake .na hayo maubiri aliombwa kuuuzuria na watanzania waishio UK.Na wala hakupanda gari .alipanda train ambayo ni £20 tu kwenda Reading na kurudi London.Tena sio first class bali third class.Sasa kosa lake liko wapi.Mnaacha kuangaika na Michuzi anayetumia hela zenu vikesheni mnamfuata Sumaye alikwenda kutibiwa akaenda na kwenye mahubiri hata hayo maubiri ni tiba pia.Badala mshukuru anamuomba mungu na huenda akamjalia akawa na afya njema ,hivyo hatatumia hela za wadau kwa matibabu tena.mnalamika.fungueni macho.
Mwanajamii wenu,
Susu
London,UK.
Acha wivu na majungu, unamuonea gere Sumaye, hiyo ni husuda, msione mwenzenu akifaidi, acha roho ya korosho, mwache atumie. Hata yeye analipa kodi, alaaaaa.
Mod thread ya majungu hii, mmeiona au hadi kuireport?
check up yaweza kuwa pamoja na colonoscopy (kama aliyofanyiwa bush wakati fulani); yahitaji kum-sedate mtu na kwa TZ inafanywa na surgeon; sasa kwa kuwa hakuna hospitali maalumu ya viongozi utakuwa umemuanika mukulu kwa at least watu 6 (nesi 2, wa-usingizi 2, surgeon 1 na assistant 1), hiyo ni noma kwa mukulu kama huyo!Hivi medical check up inajumuisha nini? Yaani hiyo check up haiwezi kufanyika Tanzania? Na kama haiwezi kufanyika Tanzania, tatizo ni nini - wataalamu(sijui hata unahitaji utaalamu gani) au vifaa au vyote viwili? Just curious..it doesn't hurt anything to ask.
Kama unakuwa huna utii na adabu kwa viongozi wako wakuu wa nchi, basi utakuwa huna utii hata kwa baba yako na mama yako iwapo unao (samahani lakini), Kama unayo dini ungetambua umuhimu wa mtu yeyote kwenda kusali, sasa iwapo wewe husali na hukuwahi na pengine hutapata hata uongozi wa Kijiji kama 'Mjumbe wa shina', ungefika level ya Mhe: Sumaye si ungesema HAKUNA MUNGU? Nikudokeze?.....Maandiko Matakatifu yaani Biblia yanasema hivi 'YEYOTE ANAYEASI MAMLAKA ILIYO KUU DUNIANI AMEMWASI MUNGU, KWA KUWA HAKUNA MAMLAKA ILIYOJIWEKA DUNIANI' ningekupatia Chapter na Verse number usome ila ukifunuliwa jinsi ya kuisoma then come back nikupe references ufike kwa urahisi. UPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO?
Hatumii kodi kwenda mji hadi mji kuhubiri mambo ya dini.afanya lililompeleka.au SUMAYE amekwenda reading kuandaa kundi la wana CCM kwa ajili ya uchaguzi?kwenye picha amejazana na wanaccm london sio mapasta au wachungaji.Hata Al haj Hassan Mwinyi anapokwenda nje for medical check up huwa hasahau ibada!