Historia ni mwalimu mzuri, na kuna wakati ni vigumu kuikana.
Baada ya kusomwa taarifa mbili za Kamati za Makinikia pameibuka manabii na mashujaa wa nchi wakidai "..Rais Magufuli alikuwa wapi kipindi hicho chote" amekuwa Mbunge na Waziri kwa kipindi cha takribani miongo miwili na sasa Ndiye Rais. Kwanini hakuchukua hatua? Baadhi ya mashujaa hao walionukuliwa kirefu na vyombo vyetu vya habari ni Luwasa na Sumaye.
Najiuliza, kipindi hicho chote Sumaye na Lowasa walikuwa wapi? Je, hawakuwa Mawaziri na Je, hawakuwa wabunge? Bahati njema wote wawili wamepata kuwa Mawaziri wakuu huku Sumaye akihudumu kwa kipindi chote cha mpito huo na kuvunja rekodi ya kuwa Waziri Mkuu pekee tangu nchi hii ipate uhuru kuhudumu kwa miaka 10. Aliongoza kipindi cha mageuzi ya kiuchumi na ubinafsishaji wa migodi hii yote (1995-2005). Lowasa yeye amekuwapo kama Waziri Mkuu (2006-2008) lakini kabla ya hapo amekuwa Waziri kamili kwa zaidi ya miaka 20. Na amekuwa mbunge.
Wawili hawa mpaka kufikia Julai 2015 walikuwa wanachama watiifu wa CCM. Walikuwa sehemu ya yale majibu ya "Ndiooooooooo" kwa muda wote huo. Leo ushujaa wao ni upi?
Shukrani kwa Luwasa kung'amua kuwa mchakato mzima wa kufikia maamuzi ya kiserikali hauwezi kumwacha salama aliyekuwa Waziri mwenyedhamana (mtetezi mkuu wa hoja). Lakini pili, kwa dhana ya collective responsibility, hakuna namna yeyote aliyewahi kuwa Waziri au Mbunge kwa kipindi chote hicho (ukiondoa wale wa upinzani waliowahi kupinga) kukwepa wajibu.
Sumaye na Lowasa hawakuwepo?