Sumaye kupasua bomu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye kupasua bomu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Oct 2, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kutafakari kubwagwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, katika kinyang'anyiro cha ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), yeye (Sumaye), ameibuka na kueleza kuwa siku tatu zijazo ataeleza kilichojitokeza katika uchaguzi huo.

  Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka 10 cha awamu ya tatu ya uongozi wa Rais Benjamin Mkapa, aliangushwa juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu, katika kinyang'anyiro cha Mjumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hanang' Mkoa wa Manyara.

  Akizungumza na NIPASHE jana kwa simu, Sumaye alisema atakapokutana na waandishi ataeleza kwa kina kilichojitokeza kwenye uchaguzi huo siku tatu zijazo atakapowasili jijini Dar es Salaam.

  "Nimepigiwa simu na waandishi wengi wakinitaka nizungumze suala la kuangushwa kwangu kwenye nafasi ya NEC, lakini nimewaeleza kuwa nitaeleza suala hilo siku tatu zijazo nitakapokuwa Dar es Salaam," alisema Sumaye.

  Dk. Nagu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang, aliibuka kidedea kwa kupata kura 648 dhidi ya kura 481 alizopata Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005.

  Kuangushwa kwa Sumaye katika kinyang'anyiro hicho kumezua maswali mengi nchini ambayo baadhi ya watu wanaeleza kuwa hiyo ni ishara mbaya kwa mwanasiasa huyo mkongwe ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kugombea urais mwaka 2015 kupitia chama hicho kikongwe.

  Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa zamani wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mbunge wa zamani Jimbo la Makete, Dk. Hassy Kitine, alisema kuangushwa kwa Sumaye katika nafasi ya NEC hakuwezi kumuathiri kisiasa kama atachukua uamuzi wa kuwania urais mwaka 2015 kupitia CCM.

  "Katiba ya CCM haisemi kuwa kama unataka kuwania urais ni lazima uwe mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kwa hiyo nasema kama Sumaye kweli anatafuta urais, bado ana nafasi ya kuwania," alisema Dk. Kitine ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

  Kwa upande wake, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema uchaguzi wa NEC ni wa ngazi ya wilaya tu kwa hiyo Sumaye anaweza akawa anakubalika kitaifa kuliko katika wilaya anayotoka.

  "Kimsingi siwezi kumkadiria, sababu suala la urais ni kitu kingine, ni uamuzi wake binafsi sababu alipochukua fomu kugombea u-Nec alijua kuna kushinda na kushindwa, pia upo usemi kwamba nabii hakubaliki kwao," alisema Sitta.

  Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahimu Lipumba, alisema kuangushwa kwa Sumaye ni dalili mbaya kwake kama ataamua kuwania urais mwaka 2015.

  Prof. Lipumba alimpongeza Dk. Nagu kwa ushindi alioupata dhidi ya Sumaye. Hata hivyo, Lipumba alisema kushindwa kwa Sumaye hakumaanishi kwamba hakubaliki ndani ya chama chake.

  "Hizi ni dalili mbaya kwa Sumaye na inaonyesha kwamba kila nafasi atakayogombea atashughulikiwa, pia mwanamke kumbwaga mwanaume ni changamoto kwa vyama vingine kwamba wanawake wapewe nafasi, wana nguvu za kuongoza," alisema Prof. Lipumba.


  Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Philip Mangula, ameibuka na kujitetea kwa wanachama wa wilaya mpya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwamba jina lake liliondolewa ili asiwanie nafasi ya Nec kupitia wilaya hiyo kwa sababu alikuwa nchini Msumbiji.

  Mangula aliomba kuwania nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Wanging'ombe pamoja na wanachama wengine ambao ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Njombe Magharibi, Yono Kevela, Julieth Kadodo na Mechard Msigwa, lakini jina lake lilifyekwa na vikao vya juu vya CCM.

  Kuondolewa kwa jina la Mangula kulizua madai kwamba huenda kunatokana na madai kwamba haelewani na baadhi ya viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa.

  "Wakati vikao vya juu vya chama vikiendelea Dodoma, nilitumwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenda Msumbiji kuwakilisha nchi katika maadhimisho ya chama cha Frelimo," alisema Mangula.

  Mangula akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Wanging'ombe juzi, alisema madai kwamba hatakiwi na viongozi wa juu wa chama ni uzushi.

   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Hawa nao ni Mikwara tu, Kwenye Kikao na Wandishi wa Habari ataishia kuongea haya,

  1, Sijaridhishwa na Jinsi mchakato ulivyo kwenda wakati wa Uchaguzi, Kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa Kanuni

  2. Ila kwa sbabu ya Chama Changu nimeamua kusahau yote na naahidi kusaidiana na Mshindi katika Kujenga Chama Wilayani Hanang na Wilaya zingine za Jirani

  3. Naamuru Kundi langu Kusambaratika Rasimi na Kumuunga Mkono Mery Nagu kwa Hali na Mari katika kuikitumikia Chama Chetu wailayani Hanang

  WATU WASISUBIRIE NONDO ZA AJABU SANA KUTOKA KWA SUMAYE, CCM YOTE INAFAHAMIKA, KWANI TUMESAHAU DR WA KULE NZEGA ALIVYO TISHIA KUONGEA NA WANDISHI WA HABARI NA MWISHO WA SIKU AKANYWEA
   
 3. n

  nyanyonyi Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado tutasikia mengi sana
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  bagwell waliambiwa asiyeridhika aondoke ccm, hawakuambiwa kwenda kwenye vyombo vya habari.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tunakumbuka pia mahojiano ya Lowasa baada tu ya kuachia uwaziri mkuu, TvT yalivyokatizwa ghafla!
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,567
  Trophy Points: 280
  Mangula ni CCM kwelikweli!!!
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Huyu mu iraq kwa kukiuka maelekezo ya mweyekiti(SULTAN JK) afukuzwe kabisa kwenye chama.
   
 8. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Bomu tena? Kageuka Mpalestina? Ukionja madaraka halafu ukataliwe nooooomaaaaaaa!
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  bagwell Mh. Simaye ana mgao wake wa keki inayomtosha maisha yake yote - 80% ya mshahara wa waziri aliye madarakani; aangalie mambo mengine ya kimaendeleo kama kutumia akiba zake kuibua miradi itakayoongeza ajira kwetu sisi walala hoi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  JK kaishamaliza kila kitu njia nyeupe Sumaye ondoka CCM.
   
 11. m

  maswitule JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Alitakiwa aongee dakika tano au mara tu anapotoka kwenye chumba cha uchaguzi ndio angeongea ukweli lakini siku tatu hatakuwa na jipya lolote
   
 12. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ingawa FTS alishindwa kwa mizengwe, hatadiriki kusema ukweli kutokana na nidhamu ya CCM.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Hakuna jipya. Sumuye is finito, Waziri mkuu mstaafu analipwa pesa mpka anakufa, sijajuwa huyu amesahau nini ambacho alishindwa kukifanya akiwa Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali kwa miaka 10.

  Ninavyomshangaa Sumaye ndivyo ninamyomshangaa Mangula na mpaka leo bado sijajuwa ni nini kilichojificha nyuma ya kuwa mjumbe wa NEC.
   
 14. C

  Concrete JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hakuna jipya hapo, zaidi ya maneno ya faraja tu.
   
 15. m

  malaka JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kubwa hapo ni kuunga mkono mshindi hakuna jipya mtaniambia.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  I find this kind of funny........Why is JK sometimes acting like this?
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mzee mangula kaahidiwa na mwenyekiti ataingia nec kwa kuteuliwa,katiba inampa nafasi mwenyekiti,ndio mana hana wasiwasi,jk aliamua muda mrefu kurudisha uhusiano wake na mangula baada ya kugundua ni kina lowassa ndio walikua wanamchonganisha nae kwa kuwa walikua wanamuogopa kama ilivyokua kwa mwandosya,jk anamuhitaji sana mzee mangula kwa sasa
   
 18. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Hawa ndo aina ya viongozi nisopenda hata kuwasikia yaaani kawa waziri mkuu for ten good years bado anataka kuwa katika mashindano ya vitu kama hivi ili iwe nini sijui........alienda kusoma Havard sijui ........kwa nini wasianzishe miradi hata ya kuelimisha wananchi tuuu huko wilayani na kitaifa ili kusaidia jamii.......madawati hakuna na yeye ana links nyingi tu kutokana na wadhifa aliowahi kuubeba.......haoni Maajar's family atleast wanafanya kitu??????

  Hivi hawaoni kina Bill Gates?????

  Unapokuwa mtu mzima ni bora kurudi katika jamii utakozikwa kuliko kukomaa na era ambayo tayari haijali nani ulikuwa huko nyuma..........acha wajifunze in a hard way!!!!!!!
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Kwa nini hakumwambia asigombee?
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nimefurahi Mama Nagu kushinda teh teh teh
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...