Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Waziri mkuu mstaafu wa Serikali ya Tanzania, Frederick Sumaye, amelishangaa Bunge la Tanzania kukataa kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akizungumza na Mwanahabari Huru Sumaye ambaye ndiye Waziri Mkuu aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu kuliko Waziri Mkuu yeyote nchini Tanzania, amesema angependa kuona Bunge linatengua maamuzi hayo na kurejea kufanya kazi na CAG.
“CAG hukagua hesabu za Bunge, kwa maamuzi haya ya leo ya Bunge ina maana Bunge litakosa haki ya kukaguliwa hesabu zake. Hii itapelekea kama kuna ufujaji wa pesa kwenye Bunge, basi nchi haitafahamu kwa sababu hakuna atakayeibua taarifa hizo.
“Lakini pia CAG akiikagua Serikali na akaona kuna mahesabu hayajakaa sawa, Bunge halitaweza kuisimamia vizuri Serikali kwa kuihoji mahala zilipokwenda pesa,” amesema Sumaye.
Waziri Mkuu huyo wa zamani amesema maamuzi haya ni maamuzi mabaya sana kwa maendeleo ya Taifa na ni udhalilishaji wa ofisi ya CAG.
Naye Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, amewalaumu wabunge wa chama tawala cha CCM ambao kwa wingi wao wamepitisha maamuzi ya kutotaka kufanya kazi na CAG.
“Wananchi ndio waone namna sisi wawakilishi wao tunavyojali matumbo yetu na kusahau maslahi ya nchi. Hapa kuna kitu kinafichwa na wameona CAG ataanika uozo.
“Na sisi Wabunge wa upinzani tunawalaumu na kuwashangaa sana hawa wenzetu wa CCM. Hivi hawaoni hatari ya kukataa kufanya kazi na CAG?” amehoji Ester Matiko.
Bunge la Tanzania
Spika wa Bunge la Tanzania alikasirika baada ya CAG kukituhumu chombo hicho cha kutunga sheria kuwa ni dhaifu.
Baada ya kauli hiyo, ambayo CAG aliitoa kwebye chombo kimoja cha habari nchini Marekani, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimuita CAG kwenye kikao cha Kamadi ya Maadili na Mamlaka ya Bunge ili ahojiwe.
Leo Jumanne, Aprili 2, Kamati ya Maadili ilipeleka ripoti yake bungeni ili ijadiliwe. Na wabunge wengi walipiga kura za ndio wakiunga mkono azimio la Bunge kutofanya kazi na ofisi ya mkaguzi huyo.
Maamuzi hayo yamekuja siku chache baada ya CAG kuwasilisha kwa Rais ripoti mpya ya hesabu za Serikali ya mwaka 2018/19