Sumaye amgwaya Lowassa!

Hana jipya. WanaJF naomba kuuliza ivi ukiwa waziri mkuu mstaafu ina maana ukihama chama unakosa haki zako za uwaziri mkuu mstaafu au katika serikali hii ya Tanganyika inakuwaje. Mi nafikiri waziri mkuu unakuwa kiongozi wa wote bila kujali chama. Na stahiki zako unawezapata hata ukihama chama kama wewe ni waziri mkuu mstaafu. Naomba nielezeni
 
Hebu mtafute Pasco hapo atakuwa navyo hivyo vibahasha, kwenye ghafla kama hizo za vibahasha huwa hakosagi.
Mkuu Mzalendo80, si kweli kuwa hafla za vibahasha mimi huwa sikosi, bali nilipokuwa reporter, hivyo vi bahasha, nimevipokea sana!. Bahasha hizo za waandishi mimi nimezihalalisha rasmi hapa, Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...na kwa sasa mimi sio reporter tena, ni mwandishi wa kujitegemea, situmwi na mtu, siwajibiki kwa mtu, wala siitegemei media yoyote kutoa habari au program zangu!, ukiniona mahali, ujue mimi ndio nimelipa na sio mimi kulipwa na hizo media, kwenye press conferences zangu, mimi ndio huwa navigawa hivyo vibahasha halali.
P.
 
Mpaka hapa navilaumu vyombo vyetu vya habari, vilipata wapi ujasiri wa kutuandikia zile habari, SUMAYE KUPASUA JIPU, SUMAYE KUSEMA YA MOYONI, SUMAYE ATETA NA CHADEMA, NK......wametuweka matumbo joto kwa kudhani labda Sumaye ataongea lolote jipya juu ya Chama chake, analishwa,anapewa usafiri, anapewa mshahara, anapata ulinzi na mazagazaga mengine leo atapata wapi ujasiri wa kukivua nguo chama chake?
Mzee wa watu alisema ataongea na waandishi wa habari basi, hakusema uzushi magazeti yetu wanaotulisha ili wauze makaratasi yao.
 

Hawana jeuri ya kuhama hawa waswahili,si mnakumbuka yule mungine nae aliwahi kuitisha press conference kama hii kule kwake monduli nadhani mwaka huu mwanzoni,tukawekwa matumbo joto mwisho wa siku akaishia kutapatapa tu,mwisho wa siku hakuna mwanachama wa ccm aliye mkubwa kuliko chama,wote wanakiogopa chama.Jamaa wa monduli aliishia kulialia tu kama huyu ndugu yake,alilialia kama ifuatavyo:


 
kachanganyikiwa kushindwa na mwanamke, kama rusha ilitawala kwenye uchaguzi,utaratibu wa nini kifanyike anaujua. yaani kwa hii press aliyoitisha ameonesha udhaifu wake na kumpaisha juu mshindani wake
 
Reactions: Ame
Sumaye has been P our PM for 10 ten fuc king yrs! Anatutaka nini? Alianzisha takrima Leo analia lia nini like a hIgh school girl on the first day out?

Kaka punguza ukali wa maneno...otherwise utakula ban mda si mrefu.
 
Thanks for not being emotional. Kweli tunawahitaji viongozi shupavu na mahiri kama Sumaye am,baye anachukia rushwa na kuipiga vita kwa maneno
 
Reactions: Ame
Na hawa waandishi wetu vp huwa hawaulizi maaswali maana kuna mengi ya kumuuliza, kama alivyosema mchangiaji mmoja kwamba ikiwa hakati rufaa it means amekubaliana na rushwa ndani ya chama chake, hakika sijaona lolote la maana aliloongea zaidi ya MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Reactions: Ame
Kakutuma huku kuja kuwatoa watu kwenye mada?nimeonamlolongo wa mahoteli tuuu,hakuna chochote cha maana,kwenda zako gamba wewe.
mie sijamuelewa alieweka hiyo link,
1. hizo hoteli ni za sumaye
2. za mpinzani wake/ magamba mwenzie?
3. ndo huwa anafikia(sumaye)
4................
vinginevyo jamaa mpumbavu au atupe korilesheni ya uzi huu na hizo hoteli
 
Rushwa alifanya yeye 2005 kuwania Urais kwa kuwapa wajumbe wa NEC kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. enzi hizo (Mpare) wajumbe hao walikunja buku 300 kila mmoja South corridor na Hyanda a juu walimpa Mwandosya.

Hiyo Mikoa ya Lindi & Mtwara Mama wa Mgombea aliwaonya hizo hela kuleni na kura mpeni Shemeji yenu ndio maana 3 bora NEC hawakumpitisha licha ya kutoa rushwa ndani ya CCM.

Miradi ya Kilimo ya IFAD ilijaa rushwa na ukabila Shinyanga Dodoma na Manyara ktk Mashamba ya Manyata na Basuto huingii hata kwa Rushwa leo kasahau.

Nimefurahi alivyosema atatulia huo ndio uungwana kuliko kuhama CCM.

Huyo aliyemzidi kete hataupata Urais kwani rushwa ipo juu tu huku chini kwa mpiga kura haipo
 
tatizo la ccm ni kuwahi kuzibana midomo, tena kwa vitisho. Alianza lowassa kipindi kile akiwaita waandishi hadi monduli. Akabwabwaja pumba. Akaja mwakyembe akasema ataanika kila kitu. Mara kimya, mara yuko kanisani. Akaja ulimboka. Mara kimya. Sasa huyu sumaye, mara naye anabwabwaja.
 
Sumaye hata angeenda CDM, aende CUF, aanzishe chama chake hakuna legacy aliyoiacha itakayokuwa mvuto kwa uzalendo. Ni mmoj kati ya waziri mkuu aliyeboronga kabisa. Walitoka madarakani na sifa mbaya sana yeye na mkuu wake Ben. Nakuambia hata Pinda akistaafu atakuwa na heshima kuliko huyu mla rushwa anayelialia kuzidiwa kete na wala rushwa wenzake. To hell Sumaye. To hell Lowasa. To hell Sitta. To hell Mwakyembe. To hell Benard Membe. To hell Asha R Migiro. To hell all CCM Hyenas.
 
Reactions: Ame
Pamoja nimechelewa kuuona uzi huu ila nimeishia page ya kwanza tu kuusoma, sina muda wakuwasikiliza wapuuzi, Sumaye is Dead snake. That's it.
 
Takrima si ilianza kwa Sumaye!! S yeye aliua agenda ya Uzawa! Si yeye alidhoofisha kabisa upinzani nchini akiwa na boss wake BM. Hili ni fundisho kuwa "kiongozi lazima uwe visionary" na ukiona "manyoya, ujue kaliwa". Habari ndio hiyo!!
 
hili jamaa punga sasa kapoteza muda wa nini kwa waandishi? na waandishi wetu hovyo kabisa kesho utaona wanaandika huu upuuzi
 
• Akana kuwa na uhasama naye, adai hamwogopi mtu

na Edson Kamukara

WAZIRI Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, ametoa dukuduku lake la moyoni akisema hana uhasama na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa na kubainisha kuwa rushwa ya kimtandao iliyokighubika Chama cha Mapinduzi (CCM), ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang'.

Sumaye ambaye amepigwa mweleka kwenye uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kupitia wilayani Hanang' na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu, alikutana na wanahabari kuelezea mwendo mzima wa uchaguzi huo na hatima ya CCM.

Akizungumza kwa kujiamini huku akinukuu kauli zake za nyuma kuhusu mwenendo wa rushwa ndani ya chama chake, alisema uchaguzi wa Hanang' ulighubikwa na matumizi makubwa ya rushwa, vitisho vingi, uharamia wa kuhamisha wapiga kura usiku na maovu mengineyo mengi.

"La msingi ni kuwa mimi sijakata na wala sitakata rufaa ya kupinga matokeo wala kupeleka malalamiko katika chama changu kwa sababu yaliyokuwa yakitendeka yalikuwa yanafahamika," alisema.

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama kuondoa uvumi uliokuwepo kuwa Sumaye na Lowassa wana ugomvi wa kisiasa hasa wakati huu wa kujipanga kuelekea mbio za urais 2015, kiongozi huyo alisema hajazungumza na mtu kuhusiana na mambo hayo.

Sumaye alisema taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na kunukuliwa kuwa zimetoka kwenye chanzo kilicho karibu naye, lakini akafafanua kuwa hawezi kupambana na Lowassa kwa sababu hana uhasama naye.

"Nikiamua kugombea urais sitagombea kwa sababu ya mtu fulani bali nitagombea kwa sababu ya nchi na wananchi wa Tanzania," alisema.

Akifafanua kuhusu vitendo vya rushwa ndani ya CCM, alisema kuwa nchi nyingi hasa zenye demokrasia changa kama Tanzania zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi.

Sumaye alisema madaraka yatakuja tu kama wananchi wapiga kura wanaona wewe ndiye utayewafaa na wala wasirubuniwe kwa fedha au jambo lolote kwa kutumia vibaya nafasi ya umaskini wao.

"Hivi leo tunavyoongea hali ya rushwa wakati wa uchaguzi imekuwa mbaya zaidi. Katika uchaguzi wa kidemokrasia wapiga kura humchagua mwakilishi wanayemtaka kwa sababu ya uwezo wake yaani humchagua mwakilishi wao kwa ajili yao.

"Katika demokrasia iliyopondeka kwa rushwa, fedha huwachagulia watu mwakilishi kwa ajili ya waliotoa fedha. Wapiga kura ni wapiga mihuri tu," alisema.

Sumaye bila kutaja majina ya wahusika, alisema hali imetoka kwenye kuhonga ili achaguliwe katika eneo lake na badala yake kuna rushwa za kimtandao ambapo mtu hutoa fedha katika maeneo mbalimbali nchini ili watakaochaguliwa wawe wafuasi wake mbele ya safari atakapowahitaji.

"Uchaguzi huu umeghubikwa sana na matumizi makubwa ya fedha za rushwa. Suala la rushwa katika nchi yetu na katika CCM siyo mgeni lakini sasa tatizo hilo limeota mizizi na linazidi kuwa kubwa," alisema.

Kuhusu kwenda CHADEMA
Sumaye alikanusha vikali akisema hajawahi kukutana na kiongozi yeyote wa CHADEMA wala chama chochote cha upinzani.
Lakini akabainisha kuwa hawapaswi kufikia kudai kuwa vyama vya upinzani au viongozi wake ni maadui wa CCM.

"Mimi ningekuwa nimekutana nao ningesema tu mbona hata hao wengine wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba huwa wanakutana nao? Alihoji.

Alisema yeye ni mwanachama mwaminifu wa CCM na kwamba alishawahi kusema kuwa hayuko kwa ajili ya cheo na wala kukosa ujumbe wa NEC na hasa kwa njia iliyotumika hakumnyimi usingizi wala hahuzuniki kugombea urais kwa tiketi ya CCM endapo ataamua kufanya hivyo.

Sumaye alisema kama ni matatizo, vyama vyote vina kasoro zake, hivyo haoni kama kuhama chama ni suluhu na kutamba kuwa kushindwa kwake kumempa nguvu zaidi na hivyo akiamua kugombea urais lazima apitie CCM.

Kuhusu TAKUKURU
Alipoulizwa kuhusu utendaji wa Taaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kama imetimiza wajibu wake kushughulikia tuhuma za rushwa kwenye uchaguzi wilayani Hanang', Sumaye alitafakari kidogo kisha akajibu kwa kutumia mfano.

"Hivi kama nyie wanahabari mmekuja hapa mkanisikiliza haya ninayowaeleza, halafu kesho watu wanasoma kwenye magazeti yenu hawakuti kitu au kwenye televisheni hawaoni, wanaweza kusema mmetimiza jukumu lenu? Alihoji Sumaye.

Kada huyo aliwaachia wanahabari watafsiri wenyewe kama kweli TAKUKURU inatimiza wajibu wake katika kushughulikia madai ya rushwa kwenye chaguzi.

"Napenda nitambue kuwa haya ninayoyasema si matamu masikioni mwa baadhi yetu lakini ni vema tukayasikiliza kwa makini na kuchukua hatua chanya ili yasilete madhara zaidi katika jamii na wala tusidiriki kuwanyamazisha wanaoyazungumzia
 
Sumaye hana ubavu wa kupambana na Lowasa hata kwa dakika moja tu,ila ni kweli chaguzi za ccm zimetekwa na wanamtandao,kumbuka uchaguzi 2010 Selelii,mh sitta (uspika) na wengine wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…