Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 579
- Thread starter
- #81
Mtiririko wa post zako hauna tofauti na mtiririko wa post zilizokuwa zikiletwa hapa jamvini na TUNTEMEKE dhidi ya viongozi wa CDM. Inaelekea wewe ni mwathirika wa mfumo wa huu mpya wa Mwakyembe unaowaweka nje wezi wa mali za watumiaji wa bandari ya Salama. Kama sio mwathirika wa moja kwa moja basi wewe umetumwa kufanya kazi hii,ila jambo ambalo hujafanikiwa ni kutokujua kwamba waadhirika wa uchafu ule uliokuwa ukifanywa pale bandarini hawakuelewi na wanakuona wewe ni mpika majungu.
Haiwezekani usione zuri alilofanya Mwakyembe tokea ameanza kuchukua hatua dhidi ya dhuluma wizi uliokuwa ukifanywa pale bandarini .Wewe kila kukicha ni kuweka post za kumtuhumu Mwakyembe. Jipange uje na style mpya utafanikiwa na wanaokutuma watakuongezea posho ya unachokifanya kwenye media.
Kwa mambo ya msingi hata aliposema uongo Mwakyembe nilimuunga mkono na kumsaidia kama Richmond, Madawa airport etc. Na ushahidi ninao, sio hili la kuua uchumi bandarini