SUMATRA yafungia daladala Dar

SUMATRA yafungia daladala Dar

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imeifungia daladala inayofanya safari zake Kimara hadi Kariakoo kwa siku 30 kutokana na kuwatoza abiria nauli ya Sh. 800 tofauti na iliyopangwa na mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Michael Kisaka, daladala hilo lenye namba za usajili T 276 AYT linalofanya safari zake Kimara-Kariakoo lilikamatwa kwa kosa la kutoza nauli zaidi ya kiwango kilichoridhiwa na mamlaka hiyo. Taarifa hiyo ilieleza kuwa abiria walitozwa nauli ya Sh. 800 badala ya Sh. 500 kwa safari ya ruti hiyo.

"Huo ni ukiukwaji wa Kanuni namba 34 na 35 ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji kwa Magari ya Abiria ya mwaka 2007," alieleza. Mamlaka inatoa adhabu ya kufungia basi hilo T 276 AYT lenye leseni namba A2A044023 kwa muda wa siku 30 kwa njia zote za Tanzania Bara na kwamba adhabu hii itaanza leo.

Aidha, mmiliki alitakiwa kuwasilisha barua yenye maelezo na vielelezo kuhusu hatua zilizochukua dhidi ya dereva na kondakta wa gari lako kwa kosa hilo.

CHANZO: NIPASHE

Hili suala la makondakta kujipangia nauli lipo muda mrefu sana, na abiria wamelalamika mpaka wakaona ni jambo la kawaida. naishauri sumatra iweke maofisa wao kwenye vituo vikuu vya dalala, kama askari wa jiji, ili kudhibiti daladala zinazokiuka sheria za uendeshaji.
 
Route nyingi usiku na asubuhi nauli zinapaishwa watu wa gongo la mboto mpaka chanika wameshazoea hii hali
 
Tena SUMATRA inabidi waangalie uwezekano wa kushusha nauli zote za mabasi kwani mafuta yameshuka bei.

Unakosea Dada faiza nauli ya daladala haipandi kwasababu ya mafuta tu, jaribu kuulizia spea uone zilivyo panda biashara ya daladala nishiida tu hakuna faida ya kutisha.
 
Kma unaona nauli kubwa ww subiriy nauli alali uone kma ujafika kwako saa sita ucku hayo ndio maisha yetu ya watu wa dar
 
Nchi yetu suala la usimamizi, uwajibikaji ni masuala sugu yaliyokosa dawa stahiki...
 
Nchi yetu suala la usimamizi, uwajibikaji ni masuala sugu yaliyokosa dawa stahiki...

Na kwakweli kufungia daladala moja tu kati ya nyingi mno zinazofanya hilo kosa ni maskhara yaliyopitiliza
 
kuna dala dala huwa inafanya route zake toka kariakoo mpaka kimara hutoza 1000, na abiria wengi wanaifahamu kwani huwawahisha na kuwaepusha na adha za foleni, dereva wake huwa ni mjanja mjanja kukwepa foleni, wengi wa abiria wazoefu huwa na mawasiliano na dereva mhusika kabla ya kufika kituoni, nadhani itakua ndio hilo basi kama sijakosea
 
Kwani mafuta yameshuka kiasi gani kituoni?
 
kuna dala dala huwa inafanya route zake toka kariakoo mpaka kimara hutoza 1000, na abiria wengi wanaifahamu kwani huwawahisha na kuwaepusha na adha za foleni, dereva wake huwa ni mjanja mjanja kukwepa foleni, wengi wa abiria wazoefu huwa na mawasiliano na dereva mhusika kabla ya kufika kituoni, nadhani itakua ndio hilo basi kama sijakosea
hahaha!!! itakuwa ni yule wanamuita 'osama'.
 
.... kwa taarifa tu, kama wewe unatabia ya kupakia abiria kwenye kigari chako wakati wa kwenda na kurudi kazi, summatra wakikushika adhabu yao ni shilingi 1,100,000/= mchanganua kama ifuatavyo

Kubeba abiria bila kibali cha kutoka summatra 3500,000/=
kutoza naluli kubwa kuliko kiwango 250,000/=
kuto kuwa na tiketi 150,000/=
kuto kuwa na sare 250,000/=
kukatisha ruti 100,000/=

Tahadhari kwa wenye HOHA mitaa ya mbagala yasikukute !!!
 
3500,000 + 250,000 + 150,000 + 250,000 + 100,000 = 4,250,000
 
Unakosea Dada faiza nauli ya daladala haipandi kwasababu ya mafuta tu, jaribu kuulizia spea uone zilivyo panda biashara ya daladala nishiida tu hakuna faida ya kutisha.

Bei za mafuta ndiyo chanzo kikuu cha mfumuko wa bei, fanya kautafiti japo kiduchu.
 
Back
Top Bottom