SUMATRA kero hii hamuioni?

Things Fall Apart

Senior Member
Jun 26, 2012
178
146
Habari wana jamvi,
SUMATRA ni chombo kinachohusika kusimamia viwango katika huduma ya usafiri wa nchi kavu na majini. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa kila nikipanda daladala au mabasi ya mikoani mara unakuta nafasi kati ya siti moja hadi nyingine (mbele na nyuma) inakuwa imebanwa sana kiasi kwamba magoti yanakuwa yamekita kwenye siti ya mbele yako hivyo kusababisha kukaa kwa kujibana huku magoti yakikandamizwa na siti ya mbele yako. Kama hiyo haitoshi, ikitokea abiria wa siti ya mbele kalaza kiti kidogo basi ndio magoti yanazidi kubanwa hadi kupata maumivu. Kwenye daladala ndio usiseme kuhusu kero hii. Kwanza kabisa siti za daladala ni nyembamba ukikaa siti ya upande wa njiani unakaa na kalio moja lingine linaning'inia kwani kasiti ni kembamba. Kwenye magoti ndio usiseme hiyo shida abiria wanapata.

Sasa kimsingi SUMATRA ninyi ni chombo ambacho serikali imekupeni mamlaka kisheria ya kusimamia viwango na ubora wa huduma hizi kuhakikisha kwamba wananchi tunapata huduma bora yenye viwango. Sasa kwa hili nina uhakika kwa asilimia 99.9 kuwa hamjalisimamia. Haiwezekani mmiliki wa basi la abiria anajiamulia idadi ya siti kwenye gari. Ni lazima kuwe na viwango (standards) kulingana na aina/ukubwa wa gari. Lazima kuwe na vipimo vinavyokubalika ndivyo vitumike kung'amua idadi ya siti kwenye basi na ukubwa wa nafasi kati ya kiti na kiti. Kwa kweli msitake tulifikishe ikulu japo msipolishughulikia tutalifikisha. Badilikeni jamani sio kila kitu hadi Mhe. Rais aseme ndio muwajibike. Na ndio maana akawaajiri ninyi na kuwalipeni mishahara kwa kutumia kodi zetu ili mtusaidie sisi abiria kwa hili. Zama za wananchi kuzoea shida umepita Tanzania. Serikali ya Awamu ya Tano imekwisha jipambanua kwa hilo kitambo sana. Acheni kukaa maofisini ingieni kwenye daladala na mabasi ya mikoani mjionee abiria/wananchi wanavyopata tabu kwenye baadhi ya mabasi ya wamiliki wenye tamaa ya kupata faida nyingi bila kujali ubora wa huduma wanayotoa. Au kwa sababu ninyi hampandi haya mabasi ndio maana haiwapi kero hii? Mkumbuke kuwa hizo STK na STL zimenunuliwa kwa kodi zetu tunazolipa hivyo msijisahau.

Tafadhali sana SUMATRA toeni majibu ya kero hii.
 
Ndo warefu na makalio makubwa kiasi, kwenye usafiri kwa kweli wanapata shida,
 
Kwenye miji mikubwa nashauri uwepo usafiri wa laxary nauli iwe elfu moja na elfu mbili, watu waweke bus za kisasa, kwa hizi nauli huwezi kulifanya youtong likawa daladala
 
Kwenye miji mikubwa nashauri uwepo usafiri wa laxary nauli iwe elfu moja na elfu mbili, watu waweke bus za kisasa, kwa hizi nauli huwezi kulifanya youtong likawa daladala
Mi naona ni bora nauli ipande kidogo kuliko hii adha abiria wanayopata kwa sasa.
 
Back
Top Bottom