Suluhu la bei kubwa ya bando kwa mitandao ya hapa nyumbani

creedfx

Member
Jun 24, 2022
86
37
salam salam,

Ni wazi hali ni ngumu halafu kila siku bei za vifurushi zimekuwa zinapanda bei mfano, Halotel kwangu mimi ndiyo nikiwa naona ni mtandao wenye gharama nafuu.

Kwa miezi fulani hapo nyuma nilikuwa najiunga kifurushi cha 10,000 unapewa GB 4.4 kwa mwezi, hii kidogo inapunguza gharama kwa matumizi ya kawaida ila sasa unaenda kwenye kile kifurushi cha Royal kujiunga kwa mwezi unakutana na GB 3.8 kitu ambacho ni dhahiri itakulazimu kuongeza pesa ili upate GB za ziada.

Binafsi lengo la kuja huku ni kutaka msaada na ushauri kuhusu mtandao gani unakifurushi kizuri ambacho ukipiga wastani wa pesa unayolipia kifurushi na kiasi cha data utakazopewa basi inakuwa ni msaada mkubwa kwa kiasi fulani.

Kwa sababu nafahamu kuna ma 'great thinkers' na kuna watu ambao wanauzoefu na ufahamu mkubwa kuhusu mitandao ya simu na gharama zake kiujumla, natumai nitapata msaada mzuri na kwa wakati na kama basi umefanikiwa kupata uzi huu na siyo mtaalam basi naomba umtag yeyote mwenye unafahamu anaweza tusaidia.

Mpaka kuandika uzi huu na kuomba msaada nimeshapitia nyuzi kadhaa zilizowekwa humu kuanzia 2020 mkapa 2022 kwa ku 'search ROUTER' na nyingi nimeona kipengele cha Tigo kile kifurushi cha kutumia bando ndiyo ulipe kinapigiwa debe mno.

Kama kuna kingine basi naombeni msaada.
 
Tafuta Mi-Fi ya TTCL
Sahani kaka naomba unipe mchanganuo kidogo kama initially cost na continuous running cost pia sababu why W
Mi-Fi YA ttcl and pia changamoto zake kama hutojali
 
suluhu hapo mtafute samia labda kwa majaliwa utapata mpango wa hyo bundle ila kwa serikali hii ya ccm usitarajie kuna kiongozi atakayesimama kutetea maswala kama hayo.
Tafuta namna ambayo utaweza kupata unafuu wa bundle. Ukiwa unajua kuongea na watu vizur mbona kupata gb10 ni jambo lisilohitaji hata pesa ila narudia ujue kuongea na watu vizur.
mtumiaji wa mitandao alaf ukose hata dem au mshkaji kwenye makampuni ya simu basi utakua haupo serious na maisha.

kuna ule msemo unasema unapoish jitahidi ujuane na
Askari
Hakimu
Doctor
Mwalimu
Bank manager
Watu wa halmashauri na manispaa
Mateja
Wahuni wa mtaa
Wauza bar
na Malaya wa kujiuza.
kwenye mizunguko yako watakusaidia kwa namna moja au nyingine
 
Shukran sana ndugu yangu Ila me natafuta tu haueni ya bundle maana mimi shughuli zangu zinanitaka nitumie desktop computer kadhaa so matumizi ya bundle huwa makubwa kiasi
 
Hii huduma ya satellite internet ipoje mkuu
Kampuni zinakuungia internet
Unlimited data, ila speed ndo hupimwa ie 10,20,30,40-200mbps

Bei zaanzia 70K kwa mwezi

Au
Voda Supakasi

Bei yao ni 115000-120000 kw mwezi
 
Back
Top Bottom