Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Watanzania tujiulize, miaka yote hii, kutia ndani kipindi ambapo Tanzania na Malawi tulikuwa na uhusano mbaya enzi za Kamuzu Banda, kipindi ambacho wala SADC haikuwapo, hatukuwa na mgogoro na Malawi kuhusu ziwa wa kiasi hiki. Kwa nini leo?
Kama kupigana na Malawi juu ya ziwa basi ingetokea kipindi cha Kamuzu Banda.
Angalia kwamba siku zote Tanzania tumetumia nusu ya ziwa kama letu, na hata miaka ya sabini tukaweka meli za Takoshiri kuhudumia wakazi wa mwambao wa ziwa - Mbamba Bay, Ludewa, Manda nk; kwa nini Malawi hawakulalamika juu ya nchi yao kuingiliwa siku zote hizo na wakasubiri hadi leo hii?
Sababu ni kwamba mgogoro si juu ya ziwa au mpaka, na ndio maana mazungumzo ya kusuluhisha yanakwama. Mgogoro ni mafuta mengi yanayosemekana yako katika ndani na kwenye eneo la ziwa.
Angalia kwamba hata Zanzibar wameanza suala la kujitenga baada ya kuambiwa kuna mafuta eneo la Zanzibar!
Mafuta siku zote ndio tatizo katika Afrika.
Ikiwa hivyo ndivyo, kwa nini basi mazungumzo kati yetu na Malawi juu ya suluhu ya huu mgogoro isiwe jinsi ya kugawana hii rasilimali ya mafuta itakapochimbwa popote katika ziwa? Mie nadhani tukubaliane kugawana 50:50 na kufanya juhudi za pamoja za utafutaji mafuta katika ziwa, na mambo haya ya ziwa ni la nani tuachane nayo kabisa. Ikiwa visima vya mafuta vitakuwa nchi kavu, basi Malawi au Tanzania inakuwa na haki ya kuvimiliki 100%, lakini kisima chochote cha mafuta ndani ya maji (offshore oil development) kiwe ni joint venture ya 50:50
Tukiendelea kutafuta suluhu kwa ku-focus kwenye ziwa na mpaka tutapoteza muda na fedha nyingi. Tutatajirisha wanasheria. Tuache ubinafsi, tukubali kuendelea na status quo kwamba hili ziwa ni no mans land, na hivyo tujadiliane production sharing agreement (PSA) ya mafuta yatakayotoka ndani ya ziwa.
Naomba tusaidiane kufikisha ujumbe huu kwa viongozi wetu.
Update 1
Inafurahisha sana kuona hatimaye viongozi wetu wanafanya kilekile ambacho sisi wananchi wa kawaida, bila hata kutumia gharama yeyote, tofauti na mabilioni waliyotumia kutaaua mgogoro huu, wanafanya kile engine tulichokiona siku nyingi!
Update 2