Suluhisho la mgogoro na Malawi ni hili; sio suala la ziwa wala mpaka

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Watanzania tujiulize, miaka yote hii, kutia ndani kipindi ambapo Tanzania na Malawi tulikuwa na uhusano mbaya enzi za Kamuzu Banda, kipindi ambacho wala SADC haikuwapo, hatukuwa na mgogoro na Malawi kuhusu ziwa wa kiasi hiki. Kwa nini leo?

Kama kupigana na Malawi juu ya ziwa basi ingetokea kipindi cha Kamuzu Banda.

Angalia kwamba siku zote Tanzania tumetumia nusu ya ziwa kama letu, na hata miaka ya sabini tukaweka meli za Takoshiri kuhudumia wakazi wa mwambao wa ziwa - Mbamba Bay, Ludewa, Manda nk; kwa nini Malawi hawakulalamika juu ya nchi yao kuingiliwa siku zote hizo na wakasubiri hadi leo hii?

Sababu ni kwamba mgogoro si juu ya ziwa au mpaka, na ndio maana mazungumzo ya kusuluhisha yanakwama. Mgogoro ni mafuta mengi yanayosemekana yako katika ndani na kwenye eneo la ziwa.

Angalia kwamba hata Zanzibar wameanza suala la kujitenga baada ya kuambiwa kuna mafuta eneo la Zanzibar!

Mafuta siku zote ndio tatizo katika Afrika.

Ikiwa hivyo ndivyo, kwa nini basi mazungumzo kati yetu na Malawi juu ya suluhu ya huu mgogoro isiwe jinsi ya kugawana hii rasilimali ya mafuta itakapochimbwa popote katika ziwa? Mie nadhani tukubaliane kugawana 50:50 na kufanya juhudi za pamoja za utafutaji mafuta katika ziwa, na mambo haya ya ziwa ni la nani tuachane nayo kabisa. Ikiwa visima vya mafuta vitakuwa nchi kavu, basi Malawi au Tanzania inakuwa na haki ya kuvimiliki 100%, lakini kisima chochote cha mafuta ndani ya maji (offshore oil development) kiwe ni joint venture ya 50:50

Tukiendelea kutafuta suluhu kwa ku-focus kwenye ziwa na mpaka tutapoteza muda na fedha nyingi. Tutatajirisha wanasheria. Tuache ubinafsi, tukubali kuendelea na status quo kwamba hili ziwa ni no mans land, na hivyo tujadiliane production sharing agreement (PSA) ya mafuta yatakayotoka ndani ya ziwa.

Naomba tusaidiane kufikisha ujumbe huu kwa viongozi wetu.

Update 1

Inafurahisha sana kuona hatimaye viongozi wetu wanafanya kilekile ambacho sisi wananchi wa kawaida, bila hata kutumia gharama yeyote, tofauti na mabilioni waliyotumia kutaaua mgogoro huu, wanafanya kile engine tulichokiona siku nyingi!

Update 2

upload_2017-5-30_9-50-23.png

upload_2017-5-30_9-49-32.png

Tusubir kwanza tuone diplomasia ichukue mkondo wake.

.
Wakati tunasubiria hiyo dipplomasia hebu pia tujadili yaliyokamata anga la nchi husika. Tanzania wamewapiga marufuku watu wake kumhubiri Mungu hadharani.
Malawi nao wamewapiga marufuku polisi wake kuwakamata kwa nia ya kuwafungulia mashitaka wa-se-nnge/wasagaji wa nchi hiyo.
50/50!!
.
 
Suluhisho la kweli na la uhakika ni kuingia vitani tu! Malawi hawawezi kutupangia jinsi ya kutumia maeneo ndani ya mipaka ya nchi yetu!!!!!!!!!!!!
 
kuna mtafiti mmoja alisema kama malawi watashikilia kuwa mpaka ni ukingo wa ziwa na wakashinda kwenye vyombo vya kimataifa basi sisi watz tuchukue hatua ambazo serikali ya kikoloni sikumbuki vizuri kama ni ya kiingereza au wajeremani waliichukua miaka ya mwanzoni ya 1900. walichofanya niku divert maji ya mto unaopeleka maji nyasa ambao chanzo chake kiko njombe,ambayo itapelekea kina cha ziwa kupungua na mpaka wa tanzania kusogea kuelekea upande wa malawi,na umiliki wa hazina iliopo,ila kwa wavuvi itakuwa sorry tena, sound strange!!!
 
Ha, ha ha! Na ikitokea ziwa linaongezeka ndivyo mpaka utakavyokuwa ukisogea kuingia Tanzania! Ila naona siku hizi Kyela hakuna mafuriko.
 
kuna mtafiti mmoja alisema kama malawi watashikilia kuwa mpaka ni ukingo wa ziwa na wakashinda kwenye vyombo vya kimataifa basi sisi watz tuchukue hatua ambazo serikali ya kikoloni sikumbuki vizuri kama ni ya kiingereza au wajeremani waliichukua miaka ya mwanzoni ya 1900. walichofanya niku divert maji ya mto unaopeleka maji nyasa ambao chanzo chake kiko njombe,ambayo itapelekea kina cha ziwa kupungua na mpaka wa tanzania kusogea kuelekea upande wa malawi,na umiliki wa hazina iliopo,ila kwa wavuvi itakuwa sorry tena, sound strange!!!

Sounds good.huh!
I like this!
 
Tatizo kubwa ni kuwa Tanzania inaongozwa na watu wapagani wasiomjua Mungu.

Punguza jazba. Wako viongozi usiowajua wanamtanguliza MUNGU katika kila wanalofanya.
Ni vizuri utoe ushauri tu ili ijulikane wafanye nini, ili waongoze nchi kwa uzuri na ufanisi.
 
Watanzania tujiulize, miaka yote hii, kutia ndani kipindi ambapo Tanzania na Malawi tulikuwa na uhusano mbaya enzi za Kamuzu Banda, kipindi ambacho wala SADC haikuwapo, hatukuwa na mgogoro na Malawi kuhusu ziwa wa kiasi hiki. Kwa nini leo?

Kama kupigana na Malawi juu ya ziwa basi ingetokea kipindi cha Kamuzu Banda.

Angalia kwamba siku zote Tanzania tumetumia nusu ya ziwa kama letu, na hata miaka ya sabini tukaweka meli za Takoshiri kuhudumia wakazi wa mwambao wa ziwa - Mbamba Bay, Ludewa, Manda nk; kwa nini Malawi hawakulalamika juu ya nchi yao kuingiliwa siku zote hizo na wakasubiri hadi leo hii?

Sababu ni kwamba mgogoro si juu ya ziwa au mpaka, na ndio maana mazungumzo ya kusuluhisha yanakwama. Mgogoro ni mafuta mengi yanayosemekana yako katika ndani na kwenye eneo la ziwa.

Angalia kwamba hata Zanzibar wameanza suala la kujitenga baada ya kuambiwa kuna mafuta eneo la Zanzibar!

Mafuta siku zote ndio tatizo katika Afrika.

Ikiwa hivyo ndivyo, kwa nini basi mazungumzo kati yetu na Malawi juu ya suluhu ya huu mgogoro isiwe jinsi ya kugawana hii rasilimali ya mafuta itakapochimbwa popote katika ziwa? Mie nadhani tukubaliane kugawana 50:50 na kufanya juhudi za pamoja za utafutaji mafuta katika ziwa, na mambo haya ya ziwa ni la nani tuachane nayo kabisa. Ikiwa visima vya mafuta vitakuwa nchi kavu, basi Malawi au Tanzania inakuwa na haki ya kuvimiliki 100%, lakini kisima chochote cha mafuta ndani ya maji (offshore oil development) kiwe ni joint venture ya 50:50

Tukiendelea kutafuta suluhu kwa ku-focus kwenye ziwa na mpaka tutapoteza muda na fedha nyingi. Tutatajirisha wanasheria. Tuache ubinafsi, tukubali kuendelea na status quo kwamba hili ziwa ni no mans land, na hivyo tujadiliane production sharing agreement (PSA) ya mafuta yatakayotoka ndani ya ziwa.

Naomba tusaidiane kufikisha ujumbe huu kwa viongozi wetu.

Update

Inafurahisha sana kuona hatimaye viongozi wetu wanafanya kilekile ambacho sisi wananchi wa kawaida, bila hata kutumia gharama yeyote, tofauti na mabilioni waliyotumia kutaaua mgogoro huu, wanafanya kile engine tulichokiona siku nyingi!

Nimefurahi sana kuona kumbe kile nilichoweka humu JF hayakuwa mawazo potofu. Labda voingozi wetu wanapaswa kusoma JF mara nyingi zaidi
 
Suluhisho ni kugawana kati kwa kati kama sheria za kimataifa zinavyosema kuhusu mipaka ya maji
 
Hili ni swala la kidiplomasia.. Na mipaka ipo wazi Malawi where it stands. Kuleta choko choko hizi ni kama wanajaribu kutikisa kibiriti. Hopefully yatakwisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom