Suluba za Chadema kwa CCM Mbeya sasa zaonekana....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
CHADEMA yaiponza CCM

na Christopher Nyenyembe, Mbeya

USHINDI mkubwa na wa kimbunga uliolikumba jimbo la Mbeya Mjini na kupoteza kiti cha ubunge na viti vingi vya udiwani vilivyokuwa vikikaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) umezua makubwa katika uteuzi wa viti maalumu kwa walioteuliwa kutoka kwenye kata zilizopoteza ushindi.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuna kasoro kubwa katika uteuzi wa majina ya madiwani wanne wa viti maalumu watakaoingia katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya huku wakiwa wametoka kwenye kata zilizoangushwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hali ambayo imezusha malalamiko makubwa kwa wale walioachwa wakati kata zao ziliibuka na ushindi.

Uchunguzi huo ulibainika kuwa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) kutoka wilaya ya Mbeya mjini iliteua majina ya madiwani wa viti maalum 14 kutoka tarafa za Sisimba na Iyunga kwa kuwa viti vipatavyo 14 vimechukuliwa na upinzani, CHADEMA wakiwa wamejizolea viti 12 na NCCR-Mageuzi viti viwili huku CCM ikijikuta inaambulia viti saba maalumu vya udiwani.

Hali hiyo katika kutafuta ukweli wa migongano hiyo ya kugombania viti hivyo, baadhi ya madiwani wa viti maalum walioteuliwa na majina yao kutupwa kapuni walidai wameumizwa na zoezi hilo kwa kuwa wenzao walioteuliwa wametoka kwenye kata ambazo CCM imekosa ushindi, lakini wanashangaa kata hizo kutoa viti maalumu na kuacha zile zenye ushindi.

Madiwani waliotemwa walipohojiwa na Tanzania Daima walisema uteuzi huo sio wa haki hasa wakizingatia kuwa safu ya madiwani wa viti maalum waliopitishwa ni wenye uwezo wa kifedha, wakitilia mashaka kuwa upendeleo huo unaweza kusukumwa kwa nguvu ya pesa.

Alisema kuwa kati ya madiwani saba wa viti maalum walioteuliwa waliotoka kata za Sisimba, Ilemi, Iganzo, Nsalaga, Tembela, Mwasanga na Mwakibete hawakustahili kupewa viti hivyo kwa kuwa kata hizo zilizokuwa zikikaliwa na CCM zimepoteza viti na hazina ugomvi na madiwani waliotoka kata za Itiji, Uyole na Manga kuwa hao wametoka kwenye kata ambazo CCM imeshinda viti vya udiwani wa jimbo.

Katibu wa UWT wilaya ya Mbeya Mjini, Shadya Mtoro alipohojiwa alisema kuwa jumuiya hiyo imefanya uteuzi huo kwa kuzingatia sifa za wanachama wake ambao ni wasomi, waadilifu na walioweza kuitumikia jumuiya hiyo kwa zaidi ya miaka mitano na kwamba katiba yao haisemi mwenye sifa ya kuwa diwani wa viti maalumu lazima atoke kwenye kata iliyoshinda udiwani.
 
MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
0
Wamefanya uteuzi strategically ili CCM waendelee kuonekana onekana ktk kata hizo walizoshindwa, vinginevyo CCM ndiyo inaaga hivyo! Muda si mrefu tutaanza kusema R.I.P CCM
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
2,000
nani ataongoza halmashauri kati ya chadema na ccm

naomba na mimi kujibiwa swali hilo, bahati mbaya sikuwa mbeya kwa miezi sita sasa, ningetaka kujua nitaongozwa na nani katika jiji hili, chadema au mvinyo wa kale uitwao ccm?

CCM ilipata madiwani wa kuchaguliwa 21, Chadema ilipata madiwani 14, na NCCR-Mageuzi ilipata madiwani 2, hivyo CCM ndio itakuwa na madiwani wengi katika Jiji la Mbeya.

Lakini endapo uteuzi wa mgombea umeya wa CCM utaacha makovu ya makundi ndani yao na baadhi ya madiwani wa CCM wakapiga kura za chuki dhidi ya mgombea wao lolote litaweza kutokea.
 
markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
195
Lkn kama chadema wana viti 14, ukijumlisha na 12 viti maalum jumla yao itakuwa 26. ccm viti 21+viti maalumu 7 jumla 28. nccr 2+2viti maalum. kwa hiyo mi nafikiri watakao amua nani awe meya ni nccr-mageuzi. naomba kurekebishwa kama nimekosea
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
2,000
CCM ilipata madiwani wa kuchaguliwa 21, Chadema ilipata madiwani 14, na NCCR-Mageuzi ilipata madiwani 2, hivyo CCM ndio itakuwa na madiwani wengi katika Jiji la Mbeya.

Lakini endapo uteuzi wa mgombea umeya wa CCM utaacha makovu ya makundi ndani yao na baadhi ya madiwani wa CCM wakapiga kura za chuki dhidi ya mgombea wao lolote litaweza kutokea.

Jumla ya watakaopiga kura ni 37. Hiyo ni odd number na hivyo wakisimamishwa wagombea wawili basi hakuna kura kufungana na mshindi lazima apate kura kuanzia 19 kwenda juu.

CHADEMA na NCCR wakiungana na kura zikapigwa hivihivi basi CCM watachukua umeya kwa kura 21 ambazo ni 56.76%.

Ushindi wa upinzani unaweza kuja kwa njia zifuatazo.

Utaona kwamba wakiungana hivyo basi mshindi anatakiwa apate kura 19 na kwa sababu CHADEMA na NCCR jumla yao ni 16 hivyo wanahitaji kura tatu tu kutoka CCM ili CCM iangushwe pale.

Kama kweli kuna mpasuko basi ndani ya CCM basi mpasuko ni kwamba kuna kundi kubwa linalikinzana kwa nguvu zinazokaribiana. Kwamba mpasuko ndani ya CCM umezaa kundi la wapinzani humohumo lenye karibu asilimia 30% au hata zaidi.

Je, wapinzani humo Mbeya wanahitaji kura nyingi hivyo kutoka kwa wana-CCM? Hapana. Hapa wapinzani wanahitaji kura tatu tu ndani ya CCM. Hizo kura tatu (3) yaani ni asilimia 12.5% tu ya wana-CCM inahitaji kukamilisha hasira zao kwa kuwapigia wapinzani walioungana.

Si tumeona hasira za mipasuko zinavyochukua miaka kutoweka. Hivyo uwezekano hapa wa CHADEMA kushinda kiti cha umeya wa jiji la Mbeya ni mkubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

Mbinu ni hii tu, wanahitaji kuungana na kutoa mgombe mmoja. Hiyo ni hatua ya kwanza. Pili wahakikishe hawaharibu kura hata moja. Haya mawili yako chini ya uwezo wao yaani CHADEMA na NCCR.

La tatu ambalo haliko ndani ya uwezo wao bali wanaweza kuitahidi ni kufanya kila juu kuhakikisha wanapata kura toka kwa wana-CCM. na kama nilivyoainisha, wanahitaj kura tatu tu!

Cha msingi wasisitize kura iwe ni siri. Sijui mnanishauri vipi haya maoni yangu.
 
Naomba kujirekebisha mwenyewe. Ni kwa sababu sikuzingatia suala la viti maalumu kama mwana-JF mwenzangu markach alivyolifafanua hapo juu. Si kwamba nilipotosha bali hadi leo huwa sijui ni jinsi gani hesabu hupigwa ili kupata idadi ya viti maalum kitaifa au halmashaurini.

Nimeingiza tena hizi hesabu kwenye calcolator yangu inaiambia kwamba ukichanganya na viti maalumu point zangu za mwanzo zinabaki vilevile sipokuwa sasa jumla ya kura inakuwa ni 58.

Kila chama kikiweka mgombea na kikajipigia basi CCM wanashinda kwania wana kura 28 na CHADEMA wana kura 26 na NCCR wana kura 4.

Hivyo nikirudi kwenye yale mawazo yangu hapa CHADEMA wakiungana na NCCR basi hakuna tena haja ya kuhitaji kura toka ndani ya CCM hata kama kusingekuwa na mgawanyiko. Na hapa CHADEMA wanahitaji kura tatu tu toka NCCR.

Je, haiwezekani kupata kura tatu toka NCCR? Je, haiwezekani kupata kura hata moja toka ndani ya CCM yenye mgawanyiko huko Mbeya?

Mimi naona uwezekano ni mdogo sana kwa CCM kukwepa shimo hili la anguko. Yaani ikitaka kushinda basi kazi ni kubwa kwelikweli.

Mengine yote yanabaki kama nilivyosema dakika tano zilizopita na samahani kwa usumbufu.
 
Vakwavwe

JF-Expert Member
May 16, 2009
504
225

mbona kama tunalabdisha hivi!
ni kweli chadema ina wabunge 26 mbeya? na nccr 4?
mtu atuthibitishie tafadhali.
 
Edo

JF-Expert Member
Jun 11, 2008
728
170
Mbunge (Chadema) naye si huwa anaingia kwenye vikao vya madiwani, je yeye hapigi kura?
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
2,000
Nimeingiza tena hizi hesabu kwenye calcolator yangu inaiambia kwamba ukichanganya na viti maalumu point zangu za mwanzo zinabaki vilevile sipokuwa sasa jumla ya kura inakuwa ni 58.

Kila chama kikiweka mgombea na kikajipigia basi CCM wanashinda kwania wana kura 28 na CHADEMA wana kura 26 na NCCR wana kura 4.

Hivyo nikirudi kwenye yale mawazo yangu hapa CHADEMA wakiungana na NCCR basi hakuna tena haja ya kuhitaji kura toka ndani ya CCM hata kama kusingekuwa na mgawanyiko. Na hapa CHADEMA wanahitaji kura tatu tu toka NCCR.

Mimi naona uwezekano ni mdogo sana kwa CCM kukwepa shimo hili la anguko. Yaani ikitaka kushinda basi kazi ni kubwa kwelikweli.
.

mbona kama tunalabdisha hivi!
ni kweli chadema ina wabunge 26 mbeya? na nccr 4?
mtu atuthibitishie tafadhali.

Nijuavyo mie, CCM ina madiwani 7 wa viti maalum na Chadema 4 ambapo inaleta jumla ya madiwani 28 wa CCM dhidi ya 18 wa Chadema, hivyo ushindi wowote wa Chadema utategemea tu mgawanyiko wa madiwani wa CCM.
 
markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
195
Nikupataje nimekuelewa vizuri sana kwa ufafanuzi. Kama nilivyosema awali ikiwa ni kweli viti maalumu viko hivyo kwa mjibu wa Tanzania daima la leo, basi NCCR ndio watahamua nani kuwa meya wa jiji la mbeya
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
Lakini endapo uteuzi wa mgombea umeya wa CCM utaacha makovu ya makundi ndani yao na baadhi ya madiwani wa CCM wakapiga kura za chuki dhidi ya mgombea wao lolote litaweza kutokea

Tatizo kwa CCM ni kuwa Kamati Kuu inapenda kuwachagulia viongozi wanachama wake viongozi ambao wengi wao hawakubaliki......na hii huamsha ghadhabu za wapigakura.........................na kwenye hili hebu tusubiri tuone itakavyokuwa..............
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom