Hiyo Mamlaka kuna chalii yangu aliamua kuacha na kwenda kufungua kampuni yake,na sasa maisha yanasonga.
Imejaa kujuana sana,watu wanapeana vyeo na kupandishana madaraja kwa kujuana,kama huna mtu ndani ya mfumo wa Mamlaka andika umeumia,walimuweka dogo bench,wanakuja watu wasio ajiliwa ila ni ajira za mkataba,wanapewa safari za nje na masemina kibao...pamejaa watoto wa vigogo wa mamlaka walio na kazi za mkataba.
Wanabaniana mpaka posho na kupandishiana mishahara,wakubwa wanashinda nje ya nchi kutwa kucha,wengine hakuna.
Niliumia sana dogo kipaji chake kudhalauliwa,wapo watu humo na degree za Kampala University ya Gongo la Mboto kisa wanajuana na wakubwa ndani ya mamlaka basi ni tabu,wakamnyima dogo kujiendeleza,Huyo Suleiman kama amepewa meno kamili na Mwakyembe,basi aisafishe TAA,iwe ya kiuweledi,athamini wafanyakazi kwa weledi,malipo na mazingira mazuri ya kazi....iwe yenye sura ya kimataifa...wasiogope vijana....iliniuma sana.bwana mdogo kuacha kisa fitna,na kutokuwa na Godfather