Sukuma Gang sio watu wa kupuuzwa, itafutwe namna ya kuifuta hii itikadi ili kuleta Umoja wa Kitaifa

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari JF,

Kwa wasio fahamu hii itikadi ya Kundi la Sukuma Gang inaundwa na watu wa aina 3 na ilikuwepo hata kabla ya 2015 kipindi hicho wakiwa ni wafuasi wa Lowassa ndani ya CCM hivyo baada ya kukatwa 2015 wengi wao wakaungana na Kundi la pili wanao support falsafa ya Hayati Magufuli.

Aina ya 3 inayounda Kundi Hilo ni wazalendo. Hawa wanaamini nchi inaongozwa na Kundi la watu Msoga Gang ambao hawapo Kwa maslahi ya Taifa.

Hivyo unazungumzia hili Kundi unagusa watu wengi na wenye Nguvu sana na wapo kila sehemu ya nchi mpaka kwenye vyombo usalama. Kwa kifupi ni Dubwana kubwa. Hawa kina Musiba ni mifano tu ambao hata wao kuwagusa ni vigumu sana Zaidi ya kuwatingisha tu.

Hivyo basi kama ni watu ambao wanajulikana na itikadi zao zinajulikana na ni Kundi kubwa basi ili kuweka Umoja kuna haja ya kuangalia namna ya kulivunja Hasa Kwa kuwashirikisha kwenye Mambo muhimu ya kitaifa kama Teuzi NK, kikubwa kuwepo na Umoja wa kitaifa.​
 
Habari JF ,Kwa wasio fahamu hii itikadi ya Kundi la Sukuma Gang inaundwa na watu wa aina 3 na ilikuwepo hata kabla ya 2015 kipindi hicho wakiwa ....
Kwanza hiyo kitu haipo. Kilichopo ni sera. Sisi tunataka uwajibikaji na kukomesha wizi na uzalendo. Hivyo mliokuwa mnawatukania na kumdhihaki aliyewafia mikononi mwao ndiyo hao hao watawalambisha udogo.

Uzuri mfumo wao jamaa ni ukuta kwa ukuta huwezi jua nani ni nani na waliwaachia mkajiachia hahahaha kila mtu akajulikana na uhusika wake hahahahaha poleni sana.

Kuweni wazalendo ombeni msamaha ingawa mmechelewa kinawahusu kifo tu ili nchi iendelee. Ni kama Yesu aliposulubiwa wanafunzi wake waliteswa na wengine kuuliwa ila mwisho wa siku watesi wote walikufa na injiri ya Yesu ikahubiriwa mataifa yote.

Ndiyo ninyi wezi na wauza madawa mtakufa wote na injili ya uzalendo na uwajibikaji itahubiriwa Tanzania yote na nchi yetu itakuwa tajiri sana na kila mtu atafurahia maisha.
 
Duh mbona ghafla sana

20230516_230630.jpg
 
.... kitabu ulichojiandalia mwenyewe wakati wa uhai wako ndicho kitakachoamua nini kisomwe utakapokufa. Ukijiandalia kitabu chema, watasoma maandishi mema kwenye kitabu chako; lau ukijiandalia kitabu kibovu watasoma upuuzi kutoka katika kitabu chako mwenyewe!

Usilaumu wasoma kitabu; laumu aliyeandaa kitabu!
 
Habari JF ,Kwa wasio fahamu hii itikadi ya Kundi la Sukuma Gang inaundwa na watu wa aina 3 na ilikuwepo hata kabla ya 2015 kipindi hicho wakiwa ni wafuasi wa Lowassa ndani ya CCM hivyo baada ya kukatwa 2015 wengi wao wakaungana na Kundi la pili wanao support falsafa ya Hayati Maguful...


Acheni kuwaonea hao watu.....hakuna kitu kinachoitwa SUKUMA GANG .....wala hakuna kitu kinachoitwa MSOGA GANG.....

Ni uzushi tu wa kuwashambulia wengine na kuwapaka matope kwa sababu za kisiasa.....

CCM ni moja.....hizo rabsha za makundi ya kisiasa zimekuwepo siku zote ila hazijafikia kiwango cha UKABILA NA UKANDA kama hivi inavyotengenezewa PICHA......

Taifa letu ni moja....
Sisi ni wamoja......

UKABILA+UKANDA+UDINI=USHETANI ULIOPITILIZA
 
Sukuma gang ni dubwana kubwa lisilo na chochote cha kuifanya msoga gang, sukuma gang wamefiwa na mganga sie msoga tumepoteza hirizi tu so tutaenda kuchonga ingine si mganga wetu yupo, nawaambieni asali tutalamba na hakuna chochote mtatufanya zaidi ya kelele za Nye Nye Nye Nye Nye asali asali!! Asali ni tamu kama mvinyo na tutaendelea kulamba huu ni wakati wetu tuacheni Bana.
 
Kwanza hiyo kitu haipo. Kilichopo ni sera. Sisi tunataka uwajibikaji na kukomesha wizi na uzalendo. Hivyo mliokuwa mnawatukania na kumdhihaki aliyewafia mikononi mwao ndiyo hao hao watawalambisha udogo. Uzuri mfumo wao jamaa ni ukuta kwa ukuta huwezi jua nani ni nani na waliwaachia mkajiachia hahahaha kila mtu akajulikana na uhusika wake hahahahaha poleni sana. Kuweni wazalendo ombeni msamaha ingawa mmechelewa kinawahusu kifo tu ili nchi iendelee. Ni kama Yesu aliposulubiwa wanafunzi wake waliteswa na wengine kuuliwa ila mwisho wa siku watesi wote walikufa na injiri ya Yesu ikahubiriwa mataifa yote. Ndiyo ninyi wezi na wauza madawa mtakufa wote na injili ya uzalendo na uwajibikaji itahubiriwa Tanzania yote na nchi yetu itakuwa tajiri sana na kila mtu atafurahia maisha.
Mkuu una uhakika hao Sukuma Gang wako?!!!

Msoga gang je?!!

Ni akina nani mkuu wangu?
 
Sukuma gang ni watu wabinafsi na wanaoamini kwenye siasa za fujo na kuteka na kuua wanaowakosoa. Mwenendo wao huu wakibanwa zaidi mwisho wataingia msituni. Waasi wa kwanza katika Taifa letu hili watakuwa sukuma gang.
 
Back
Top Bottom