Sukari guru inatengenezwaje?

kufanakupona

JF-Expert Member
Jun 18, 2015
522
417
Za saa hizi,

Hamna ubuge ninaoupenda kama sukari guru,ulaini laini wake kama keki na sukari tu,taaaaamu! Kibaya huku kwetu zinapatikana kwa nadra sana kwa msimu.

Napenda kuzipika mwenyewe kila mara niwe nazibunya tu,am am am am am.Kuzitengeneza kwake ndiyo shughuli,ishu.

Nielekezeni wakuu jinsi ya kutengeneza sukari guru
 
we upo mkoa gan? tafta mkagulu wenyeji wa gairo ndio mabingwa wa kupka sukari gulu
 
Last edited by a moderator:
weka picha...maana haya majina hutofautiana kulingana na sehemu ulipo
 
Ukitaka jinsi ya kutengeneza keki nambie.Vijitu hivyo vya uswahilini sjui jinsi ya kutengeneza
 
hivi nyie binaadamu wengine mnaishu dunia gani? we tangu lini umesikia sukari guru inapikwa?? ,, ngoja nkusaidie kwa nnavyo jua mie sukari guru hulimwa ndo maana huwa ipo kwa misimu na pia inapatikana baadhi ya sehemu tu ambapo ardhi yake ina support kilimo cha sukari guru. i hope utakua umenielewa.
 
Hivi sukari guru c ni yale mabaki{uchafu} yanayobaki baada ya sukari kutengenezwa kule viwandani au unazungumzia sukari guru gani mkuu?
 
we upo mkoa gan? tafta mkagulu wenyeji wa gairo ndio mabingwa wa kupka sukari gulu

Ina maana Tanzania nzima wanaojua kupika sukari guru ni waluguru peke yake?
Ina maana makabila mengine hayawezi kutengeneza sukari guru?
Naamini watu wengine wanaweza.
Hata wewe kama unaweza nielekeze tu.
 
Last edited by a moderator:
weka picha...maana haya majina hutofautiana kulingana na sehemu ulipo

Yanatofautiana majina tu,lakini sukari guru ni ile ile na ladha ni ile ile.
Hamna asiyeijua sukari guru,si' ile tamu kama sukari iliyokatwa katwa vipande vidogo vidogo na wewe?
 
hivi nyie binaadamu wengine mnaishu dunia gani? we tangu lini umesikia sukari guru inapikwa?? ,, ngoja nkusaidie kwa nnavyo jua mie sukari guru hulimwa ndo maana huwa ipo kwa misimu na pia inapatikana baadhi ya sehemu tu ambapo ardhi yake ina support kilimo cha sukari guru. i hope utakua umenielewa.

Nashukuru kwa kunifahamisha kwamba sukari haipikwi bali inalimwa.Nilikuwa sijui.
Tupe mwanga hata kidogo kama unajua jinsi inavyolimwa.
 
Hivi sukari guru c ni yale mabaki{uchafu} yanayobaki baada ya sukari kutengenezwa kule viwandani au unazungumzia sukari guru gani mkuu?

Mi' najua basi kama ni mabaki au inatokana na nini!
Mimi nazionaga tu.
Inaonekana unafahamu mengi zaidi mkuu kuhusu matengenezo ya sukari guru.
Tupe mchango(mwanga) wako mkuu unaojua wewe.
 
Nasikia sukari gulu ni mabaki ya sukari yenyewe inayozalishwa kiwandani, ni kama mauchafu ya sabuni yanayofanana na magimbi yaliyokuwa yanauzwa maeneo fulani.
 
jinsi sukari nguru inavyopikwa, chukua miwa kamua maji yake baada ya hapo weka kwenye pipa halafu pika mpaka ichemke haswa halafu tafuta chombo kisafi kama kikombe then mimina yale maji bado ya moto acha ipoe itaganda ndo inaitwa sukari nguru. uikitaka kujua zaid nenda jukwa ya kenya watakuelekeza inavyopikwa, hasa hasa ujaluoni.
 
Yanatofautiana majina tu,lakini sukari guru ni ile ile na ladha ni ile ile.
Hamna asiyeijua sukari guru,si' ile tamu kama sukari iliyokatwa katwa vipande vidogo vidogo na wewe?

sasa inatofautiana nini na hii sukari inayotumika majumbani mfano kwenye chai
 
jinsi sukari nguru inavyopikwa, chukua miwa kamua maji yake baada ya hapo weka kwenye pipa halafu pika mpaka ichemke haswa halafu tafuta chombo kisafi kama kikombe then mimina yale maji bado ya moto acha ipoe itaganda ndo inaitwa sukari nguru. uikitaka kujua zaid nenda jukwa ya kenya watakuelekeza inavyopikwa, hasa hasa ujaluoni.

Ubarikiwe sana mkuu.
Umeeleweka sana.
Ngoja nianze kuitengeneza sasa hivi kwa fujo full shendele.
 
sasa inatofautiana nini na hii sukari inayotumika majumbani mfano kwenye chai

Japokuwa zote source ni moja,yaani miwa.Tofauti ipo kubwa sana kati ya sukari guru na sukari ya kawaida ya majumbani,Kwanza kimuonekano(kiumbo),pili sukari ya majumbani inakinaisha haraka sana.
 
Inavyoelekea unaijua sukari guru kwa mapana zaidi.
Tiririka unachofahamu kuhusu aina mbalimbali ya sukari guru.

hamna wala sijui hiyo guru..mi hutofautisha sukari kwa chemical formula yake, hata hiyo aliyoeleza mkuu hapo juu nilikuwa siijui kama ndio guru.
ila jua kuwa hata hii sukari ya kawaida ukiiweka kwenye chombo ukaipika inayeyuka na baada ya hapo unaweza ukaiweka sasa kwa umbo lolote unalolitaka, hata ladha inabadilika kidogo.
 
Umetuongezea maarifa ya namna ya kuitengeneza sukari guru kwa njia nyingine mpya.
Unadhani ladha ya hii sukari guru uliyosema inaweza kuwa sawa na ile iliyozoeleka mitaani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom