sugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sugu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 27, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAKATI mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), akianza kazi katika mazingira magumu, baada ya kukabidhiwa ofisi isiyo na samani, juzi aligeuka kivutio kutokana na uamuzi wake wa kwenda kunywa chai eneo ambalo hutumiwa na watu wa kipato cha chini maarufu ‘Mwiboma’.
  Akiwa ameambatana na madiwani wa chama hicho, Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, alifika katika eneo hilo ambalo ni sehemu ya Soko la Uhindi lililoteketea kwa moto na kuagiza chai ya rangi na maandazi, jambo ambalo lilifanya mama na baba ntilie, pamoja na wateja waliokuwepo eneo hilo kugeuza ujio wa mbunge huyo kuwa mkutano.

  Tukio hilo lililoelezewa na wafanyabiashara kuwa ni ujasiri na lenye kulenga kuwa karibu zaidi na wananchi kwa lengo la kubaini kero na matatizo yao kwa ukaribu lilitokea muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina ya madiwani iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya.

  Akiwa na kundi la madiwani wa CHADEMA, walifika sokoni hapo na kwenda moja kwa moja katika meza za wateja na kuanza kuagiza chai na maandazi, hali iliyowafanya baadhi ya mama ntilie kusita kutoa huduma.

  Baadhi ya wafanyabiashara waliomtambua mbunge huyo, walianza kusambaza ujumbe kwa wenzao waliokuwa jirani na kusababisha mkusanyiko mkubwa eneo hilo, hali iliyogeuza ujio huo wa kifungua kinywa kwa mbunge na madiwani kuwa kama mkutano ambapo wafanyabiashara hao walianza kueleza matatizo na kero.

  “Hii ni kali yaani mheshimiwa leo kaamua kuja kunywa chai benchini, sijawahi kuona viongozi kama hawa ndo wanatakiwa, badala ya kujichimbia mbali hali inayofanya kushindwa kutambua matatizo ya wananchi,” alisikika mmoja wa wafanyabiashara hao.

  Waliongeza kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo kimeweka rekodi kwa kuwa hakuna mtangulizi wake hata mmoja wa nafasi hiyo aliyethubutu kwenda kunywa chai eneo hilo na kwamba hata mbunge mstaafu wa jimbo hilo, Benson Mpesya, hakuwahi kufanya hivyo licha ya awali kufanya biashara hapo.

  “Mwiboma ndiko alikoanzia maisha Mpesya, lakini tangu alipopata ubunge miaka kumi hakuwahi kufika eneo hilo alilofanyia biashara kipindi cha nyuma,” alipasha mfanyabiasha mmoja.

  Kwa upande wake, Mbilinyi alisema lengo la kwenda kunywa chai Mwiboma halikuwa la kikazi bali waliamua kwenda kufungua kinywa eneo hilo kwa kuwa linakidhi haja na si kwa ajili ya watu fulani tu.

  “Ndugu yangu hili ni eneo safi sana, kila kitu kinapatikana si unaona, mimi sijaja kutania hapa nakunywa chai na maandazi,” alisema Mbilinyi.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Tatizo viongozi wetu wengi wamekuwa "Waheshimiwa Sana" hadi vitu vya kawaida kama kujichanganya na Wananchi vinaonekana mambo ya ajabu...... Well Done Sugu... Keep it Up.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Viongozi wengi hapa Tanzania wakisha pata madaraka basi utasikia unajua mi ni nani Big up sana Sugu
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh haka kakinga bahili
   
 5. L

  Leornado JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mbona raisi Obama huwa nakula Mc Donald na hajapungukiwa na chochote?? Ni ujinga wa viongozi wa TZ kujidai wako class ya juu wakipata madaraka hata kutembea kwa mguu au mazoezi kwa baiskeli hawataki na kunenepeana kama wadudu mwisho wanakufa kwa presha.
   
 6. semango

  semango JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  viongozi wa bongo tatizo lao wanakariri badala ya kuelewa.Sugu waoneshe mfano.najua wataiga tu siku sio nyingi
   
 7. C

  CheGuevarra Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana Sugu naamini, kuwa mbunge maana yake kuwa mtumishi wa wananchi wa jimbo lako, but.. I advise that you have to fulfil your promises so that CDM retains the Constituency in 2015... Peoples..... Power
   
 8. Avocado

  Avocado Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri kuedelea kujimix,big up.
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kwanza mie hawa waheshimiwa sana huwa nawashangaa na kujiuliza kwa nini walitoa heshima ya kuwaita "Ndugu" na kudai eti wao waitwe...eti mheshimiwa....fulani, heshima ambayo hukoma pale unapokuwa nje ya Bunge ya nini? si bora wangebaki na ndugu ambayo ingetumika hata ubunge unapokoma? sasa kichekesho hata watu wa hovyo hovyo, mafisadi eti nao tukikutana tuwaite Mheshimiwa? imagine umekutana na Profesa Maji Marefu eti...Mheshimiwa Habari!
   
 10. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,771
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  Kumbe?!
   
 11. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha nawasapoti watu kama wakina Sugu lakini wabongo aisee akifanya Sugu poa akifanya mtoto wa Mkulima anakuwa anaigiza tu, ni mtazamo tu
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Akiwa hivi hivi kwa muda wote atakaokuwa mbunge basi kweli nitakubali kuwa yeye ni mtu wa watu. Time will tell
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kuwa Pinda anayo madaraka ya kuweza kuwawajibisha na kukemea ufisadi kuonyesha tu kwamba anakwenda shambani na kutembelea gari la bei ndogo wakati kodi zetu zinazidi kufujwa haisaidii kitu
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  safi sana mbunge mda si mrefu wengine wataiga mfano wako
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nampa tano Sugu..akiendelea na wengine wataiga!Sio wengine majimboni tu wanaonekana wakati wa kampaini achilia mbali kujichanganya!
   
 16. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  wanamwita sugu ah. Wanamwita sugu ah, sugu sugu sugu. We waukweli. Halafu we mpiganaji sana. Nakutakia kila la heri fuata nyanyo za anord shwazniga toka kwenye film hadi ugavana. Na bado mafisadi wataumia sana. Endeleen ku shine wana mapinduzi wa kweli.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  napenda sana avokado
   
 18. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #18
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  imeka veda ira isiwenguvu ya soda
   
 19. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Keep it up, usije badilika
   
 20. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Angalizo kwa Sugu. Kula,kulala na kuendelea na marafiki wako wa kabla ya Ubunge hakutakuwa na maana kama utashindwa kutekeleza ahadi zako kwa wananchi wakati unaomba kura.
  Kaza buti safari ni ndefu kuelekea mafanikio ya kweli.
   
Loading...