Sugu & vinega watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sugu & vinega watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mwanagandila, Dec 26, 2011.

 1. Mwanagandila

  Mwanagandila Senior Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sugu a.k.a Joseph Mbilinyi pamoja na kundi la vinega wametoa msaa wa gunia 42 za mahindi kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea siku chache mkoani mbeya!
  Msaada huo wa gunia 42 una thamani ya mil 1.2 fedha ambazo zilipatikana katika asilimia ya kiingilio cha tamasha lao mjini mbeya mkesha wa kuamkia x mass.
  Vinega walipanga kutoa tshs 1000/= kwa kila tiketi ya tshs 3000/= ya kiingilio cha tamasha hilo!
  Swali vp Clouds fm wazee wa promo mbona hatujaona mchango wao wowote katika maafa haya ya mafuriko?au hata msaada ili watoe inabid wapewe udhamini na airtel?
  Faida wanazopata kwa matamasha yao kila mwezi wanashindwa kutoa hata 1% kwa waathirika wa mafuriko?
  Ama kweli wafu fm & na baba yao rugay ni wanyonyaji wa sanaa ya bongo
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Msaada wa vinega wameupeleka kwenye jimbo la nani?
   
 3. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hii wafu fm(Clouds),nimewasikia leo wakijisifu kwamba wametoa Hema kubwa jeupe,tena mtangazaji alienda mbali kwa kusema "Tent lipo tayari pale linasubiri wagonjwa waumwe ili watibiwe"
  Huyu mtangazaji atakuwa alibip kiswahili!!!
   
 4. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  kwa hii roho kama yako,Tanzania maendeleo yatachelewa sana..
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  1. Big up to Sugu and Co. for this effort. Tunataka kuona Watanzania wana ji organize wenyewe kutatua matatizo yao zaidi, bila kungojea/ kutegemea serikali.

  2. Wabongo wenye moyo wa kutoa (including the likes of Sugu) wanahitaji kuji-organize zaid, 1.2 mil Tsh (tunashukuru) ni mediocre kwa kiwango cha maafa haya. Mie si mambo fresh kihivyo lakini nimetuma mnyamwezi buku nyumbani Krismasi hii machiz/ family wajisikie.Not into flashing, but I felt this needs to be told just to give the correct perpective on this matter. Hiyo tu ni zaidi ya concert nzima ilivyotoa kwa charity hii.Sasa kama hii issue ingepata proper publicity na coordination mengi zaidi yangewezekana.

  3. Sugu is far from perfect. Lakini watu wenye mawazo ya "umimi" hawataisha kuuliza visivyoulizika. Mtu akifanikisha a benefit concert anatakiwa kukutia deni wewe ambaye hujafanya kitu. Sio kuanza kuamsha maswali ya "concert imechangia wapi?". Sugu mbunge wa Mbeya, ulitegemea aanze kuonyesha mfano wapi kama si jimboni kwake? Mshasikia "Charity begins at home?"
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,504
  Likes Received: 5,620
  Trophy Points: 280
  Yes bro,Charity begin at home.huu ndio mwanzo mzuri kwa wasanii sio kujifanya wanatoa kwa mgongo wa wafadhili kama Clouds na Airtel! Toa mfukoni mwako(give back to society).Safi vinega!
   
 7. Mwanagandila

  Mwanagandila Senior Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Unaweza kuta hata hilo tent waliolitoa wamepewa msaada na mtu au kampuni halafu wanajifanya wao ndio wametoa!
  Airtel last week walikuwa mbeya na wafu fm wiki hiyo hiyo mafuriko yametokea mbeya, cha ajabu hatujasikia kuchangia chochote kwa jamii iliyokumbwa na maafa
   
 8. Mwanagandila

  Mwanagandila Senior Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wamechangia waathirika wa mkoa wa mbeya eneo la iyunga! Wamefanya hivyo kwa sababu tamasha hili limefanyika mbeya na wikii hiyo hiyo ndo jiji la mbeya lilikumbwa na mafuriko!
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Watu kama Ruge wanasababisha nisitembee na gun yangu.
   
 10. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Msaada sio lazima utangaze wewe subiri utangazwe na wahusika Wengine Wanapenda Media tu. Sema sabau Siku hizi hakuna uadilifu ukitoa msaada kwa kujitangaza unapata mibaraka pia.. Toeni Kutoa ni Moyo na Usambe ni Utajili
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hongera zake na mungu awazidishoe moyo wa upendo watz wot na atuondolee rohop ya kwanini inayotusumbua..
   
 12. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ulianza vizuri ila hapo mwisho umeanza uchonganishi, any way big up sugu na vinega wote kwa kusaidia watanzania wenzetu.
   
 13. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Safi sana vinega
   
 14. gwino

  gwino JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Big up Sugu na Vinega wote
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kumbe VINEGA nyumbani kwao ni Mbeya!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwani aliyetoa charity ni SUGU au VINEGA. Kama ni VINEGA je home gani mnayozungumzia? Mbeya ndio home kwa VINEGA?
   
 17. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wivu wa kike na chuki za kijinga hazitowasaidia magamba nyie.. Sugu anawauma sana siyo???? Na bado mtaumia milele...halafu utakuwa siyo wewe ila ni bangi hizo. Mtu mzima mwenye akili zake timamu hawezi kuongea upupu hivi..ninamashaka sana na kiwango chako cha elimu.
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Charity begins at home as in Sugu kwao Mbeya, kaandaa kitu na wenzake kusaidia kwao. Huwezi kutegemea Sugu aanzie charity sehemu ambayo si kwao. Huwezi kumlaumu Sugu kwa nini kafanya benefit concert Mbeya, ndio kwao.

  Vinega wa Mpwapwa nao wakipata maafa washajenga mtandao wa kuitana na wenzao kupiga benefit concert, kwa style hii Sugu nae kama ratiba inamruhusu sioni kwa nini akatae.

  Mtu yeyote atakaye shoot down attempt ya Watanzania kusaidiana wenyewe kwa wenyewe bila kuomba msaada wa serikali mi namshangaa.
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  In the name of charity, so much mischief has already been witnessed in this world.
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Don't generalize, kama kuna mischief imetokea katika this particular charity itaje.

  Ama sivyo utakataza watu kutoa kwa sababu tu "in the name of giving so much mischief has already been witnessed in this world"

  Kama wewe huna roho ya kujitolea waache wenzako.
   
Loading...