Sugu moto chiniii!!!

Hayo ni makosa na si hilo tu kuna maneno kama maalumu, maskani, wataalamu, maskini magazeti na watu wasiolewa msingi wa lugha ya Kiswahili huyaandika: maalum, maskan, wataalam, maskin, na kadhalika. Kukosoa na kuwekana sawa ndiyo njia ya kuelimishana.

Mkuu huyo Ritz kasomeshwa zile shule za "DAD AM GOING".. Siunajua kule English ndo kila kitu! Wakishajua kuandika na kuongea hiyo lugha basi ndo wanajiona ma'greatthinker.. Usipoteze muda kumfundisha elimu yetu ya "St. Abdalah"..
 
Wana JF hivi mmeona kwenye taarifa ya habari itv jinsi mbunge wa mbeya mjini alivyojaza mtu kwenye mkutano na wapiga kura wake.?
Wabaya wa sugu mtachonga sana lakini Sugu ni level nyingine. Hata kama watu hawampendi ama wanaona hafai, but anapendwa sana na kuaminiwa sana na wapiga kura wake thats enough. Sugu moto chiniii..
wewe utakuwa ni yule mpambe wake Balozi
 
Hivi alipata nafasi ya kuipondea Clouds? Maana huyu kamaa akipewa mic lazima azungumzie Clouds FM.
 
Ndio maana katika katiba mpya, cheo cha u RC kiondolewe kabisa, hawana kazi hawa MRC. Kuna Demokrasia gani wakati hawa ma RC wanachaguliwa na mtu mmoja (raisi) wakati mbunge anachaguliwa na na mamilioni ya watu halafuanakuwa chini ya mkuu wa mkoa
 
Hivi unajua ni kwa nini hii mikoa ina vurugu? ni kwa sababu wabunge wake nao ni vurugu, hawana busara na zaidi ni VILAZA kwa hiyo bila kufanya hivyo CDM itawatema mwaka 2015. Hujiulizi kwa nini ROMBO, DAR, KIGOMA na kwingine ambako kuna wabunge wa CDMA hakuna vurugu? Hawa ni watu ambao wamekotwa mitaani kwenda kuwa wabunge, so itachukua muda wananchi wa mikoa hiyo kupata maendeleo kwa vile VILAZA wao wanatafuta umaarufu ilil waweze kurudi tena mwaka 2015. Waulize wananchi wa maeneo hayo mpaka sasa LEMA, WENJE NA SUGU wamefanya nini katika majimbo yao mbali na migomo na maandamano.

SUGU kupitia mfuko wa jimbo aliwapa mikopo midogomidogo wafanyabiashara wote wadogo waliopoteza kila kitu masoko yalipoungua,wale ambao wanapanga bidhaa chini kwa kukosa pa kwenda then serikali inawafukuza bila kuwaonyesha waende wapi..ndio maana umwelewi Sugu,ila unashangaa kwa nini hawa watu wanamwelewa sana
 
Nini kushangiliwa, MREMA alisukumwa mwaka 1995 sembuse kushangiliwa. Walimshangilia kama Msanii wa Kizazi kipya siyo kama Mbunge. Wana Mbeya walishamsoma SUGU kuwa ni mpenda sifa , hivyo ni lazima wampe haki yake. Wanajua wazi kwamba pale hawana Mbunge bali msanii

kaka kama umekosa la kuandika nibora ukampumzika j2 hii.hv huo usanii wa sugu unakukera sana kweli nyani haoni masabuli yako mbona lidudu mtu lenu komba ni msanii na amefanya nini la maana.
 
Kimsingi hii ndo sababu wamemkataa asiwasikilize kwani wao hawakumtuma aongoze MBY bali JK.Kiongozi wanayeona ana uhalali wa kisiasa kujibu na kushughulikia kero zao ni SUGU kwani ndo wana mkataba naye juu ya mustakabali wa maisha na maendeleo yao.KANDORO HANA CHAKE AKAMSIKILIZE JK ALIMTUMA KUFANYA NINI MBY?Kwa kitendo hicho wamechangia dai mojawapo ktk katiba mpya ambalo ni wakuu wa mikoa au majimbo wachaguliwe ili wawajibike kwao.
upo akili
 
Nyerere aliwahi kusema tatzo linalo tusumbua wa afrika ni umaskini wa fikra na mgando wa mawazo! Hongera kwa kulidhibitisha hili baada ya miaka 50 ya uhuru wa so called Tanzania!
Mbona unajikanyaga hivyo? mara mmeona alivyokusanya watu, mara wabaya wa SUGU mtachonga, mara hawampendi wanaona hafai. Kumbe hata wewe unajua hafai unawatupia watu mpira. SUGU anajua nini , kukusanya watu siyo kigezo cha kuweza, tulishaona ona wanasiasa wengi wakikusanya watu wakiwemo akina SLAA , lakini ndo kama hivyo wanaweza nini? siasa za hasira, majungu, kashfa majukwaani na kelele za njaa ndiyo kuweza. Halafu ukumbuke kuwa SUGU ni msanii , Watu wengi wanaweza kuwa na Shauku ya kwenda kumuona Msanii na siyo Mbunge.
 
Sina tatizo na Sugu anapenda maisha ya ki-hiphop (uwana-harakati) lakini nadhani alitakiwa ayafanye haya mapema ili kuzuia uharibifu uliotokea. Pia ana direct influence kwa mkuu wa mkoa kwa hiyo alikuwa na uwezo(ambao najua anao) wa kupambana na mkuu wa mkoa kuhusu kitu sahihi kilichotakiwa kufanywa kwa ajili ya wamachinga. Hii ingesaidia wamachinga wasiingizwe kwenye fujo na ndio maana ya UWAKILISHI BORA kuliko kusubiri mpaka wamachinga waingie barabarani. Tuchukue mfano wa Dr Slaa na viongozi wengine wa kariba yake ambao hubaini matatizo mapema na kupambana nayo kabla ya kuutarifu umma inapoonekana kuna ukakasi kwenye utekelezaji.
 
Nimegundua wengi wanaomponda sugu wanawivu wa kimama, mbona hawakutumwa wengine kama nao walikuwa wanaweza kuwatuliza wananchi
 
Nimegundua wengi wanaomponda sugu wanawivu wa kimama, mbona hawakutumwa wengine kama nao walikuwa wanaweza kuwatuliza wananchi

Umesahau waliandika kwenye bango kuwa Rais wao ni Sugu. Kulikuwa hakuna wa kutuliza ile hali zaidi yake asee.
 
avatar ya kichwa ngumu nimeipenda sana yaani ccm ni pot la mtoto wa cdm kujisaidia hongera sana
 
Hapa nipite tu. Naona wengi mna chuki binafsi na Sugu. Kuleta amani ni jambo la kushangilia na sio la kubeza!.

Acheni uMasaburi nyie kueni. Amani ni muhimu sana.
 
[h=3]KUTOKANA NA VURUGU ZA MBEYA MDAU EDWIN RICHARD MWAKYEMBE AIPONGEZA MBEYA YETU BLOG NA AZUNGUMZIA KWA KINA JUU YA MKOA WA MBEYA[/h]




MBEYA YETU,
Napenda kuchukua fursa hii kwanza kuwapa pole Wananchi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwa hari iliyotokea, pili napenda kutoa shukrani zangu na pongezi kwa wamiliki wa hii blog 'MBY YETU' kwa kazi kubwa ya kuifanya dunia ione nini kinaendelea jijini MBEYA, natambua kuwa haikuwa kazi rahisi kupata picha za matukio katika uwanja wa mapambano kwa kuwa rungu na risasi za POLISI, mawe yaliorushwa na vijana katika harakati zao hayakuchagua nani zimlenge, binafsi nawapongeza sana.
Binafsi nimekuwa nikifuatilia toka Campinas, Sao Pual- Brasil kwa karibu sana, na nimeona jinsi dunia ilivyokuwa ikifuatilia kwa kuangalia reports on map kwenye hii blog, ukweli inasikitisha sana sana, hakuna atayebisha ukweli MBEYA ni jiji la aina yake sio kama Arusha kuwa utalii unajenga jiji, sio Dar kwamba maofisi, viwanda, Airport na bandari vinamchango mkubwa katika uchumi wake, MBEYA ni biashara ya maduka tena yenye mitaji midogo, na juzi tumetoka kuunguliwa kwa Soko ambalo kwa namna moja au nyingine mitaji iliyotokana na mikopo imepotea na watu kubaki na madeni.
Sasa hizi vurugu katika ukweli wa dhati mimi binafsi nimeteseka sana sana na kuona huruma ya dhati, hata kama napata fursa ya kuandika waraka huu nikiwa nje ya nchi, bado kama mkazi wa ISYESYE Block HH ni lazima tutafute suluhu ya haya. Hakuna biashara inaweza kufanyika kwenye vurugu, na hakuna atakaye faidika na vurugu kati ya VIJANA wala Serikali balini kuwa na mahusiano mabaya na kujenga historia mbaya. Serikali lazima ichukue hatua kwa kuangalia na kuandaa mbadala katika mipango yake hasa inapodili na VIJANA, ukweli usio shaka kabisa kuna tatizo la Ajira kwa Vijana Tanzania.
Bado nina imani na uongozi uliopo katika kutatua tatizo hili, lakini napata mashaka nikitafakari zaidi naona picha ya jazba ilitawala busara katika utekelezaji wa zoezi zima kwani nguvu imetumika na watu wameumia sana kwa pande zote mbili. Mhe Abas Kandoro nategemea utaonyesha uwezo wako na ubobevu wa kuongoza majiji, historia inaonesha wazi umekuwa mkuu Arusha, Dar es Salaam kama kisima cha Wamachinga walikuwepo na waligoma vile vile suluhu ikapatikana na Machinga ComplexIkajengwa, Mwanza alkadhalika machinga waligoma wakati upo pale na sasa hatua za kumaliza hili zinaendelea na Mwanza shwari sasa, sasa hata Mbeya pia nina imani utafanya vizuri kwa kutumia busara na hekima zaidi, ili siku za usoni mkionana na Wamachinga badala ya kuogopana muanze Kutaniana. Ila nakupa pole sana katika hili yangu kwako ni busara na hekima ndio pekee itakuwa tija kwa JIJI la MBEYA.
Hari ya maisha duni, choyo, Upendeleo, ubinafsi, mishahara midogo isiyokizi mahitaji ya maisha[ purchasing power] ndio madhara ya yote haya, kunusuru hali hii serikali jijini Mbeya lazima itafakari kwa kina swala hili bila ya kujali itikadi za kisiasa, ni vema mipango iwe ya wazi na yenye tija kwa maslahi ya jamii ya jiji la MBEYA kwa kuwa 'JIJI LA MBEYA LENYE NEEMA, MSHIKAMANO, KUHESHIMIANA, KUTHAMINIANA, UCHUMI THABITI BILA VURUGU INAWEZEKANA ' Kila mmoja atimize wajibu wake kwa kuzingatia sheria na taratibu.
Imeandikwa na,
Ndugu: Edwin Richard Mwakyembe

[h=3]AMANI NA UTULIVU WAREJEA GHAFLA MKOANI MBEYA NA SHUGHULI KUENDELEA KAMA KAWAIDA KUANZIA LEO, MMTU MMOJA AFARIKI KATIKA VURUGU ZA SIKU MBILI[/h]

[h=3]
[/h]


Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama katika jengo la kitega uchumi la OTTU lililopo stendi ya magari madogo ya abiria(daladala), mara baada ya Mbunge Mbilinyi kuhutubia wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama mwenye shati la miraba ya samawati(Katikati) katika picha ya pamoja kabla ya Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi Kuhutubia.


Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila kupora bidhaa madukani.

Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.

Maelfu ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.

Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), likiwasaidia Jeshi la Polisi kuweka hali ya amani na utulivu mara baada ya kuisha kwa mkutano uliofanyika katika kituo cha mabasi madogo ya abiria(daladala) eneo la Kabwe Mwanjelwa jijini Mbeya

Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi.

NB:- Mtu mmoja afariki, watano wajeruhiwa kwa risasi na 235 wakamatwa, Mbunge ataka waachiwe bila Masharti yoyote.

[h=3]BAADA YA KUPIGWA BOMU LA MACHOZI WAGONJWA WAKIMBIA, MADAKTARI WAWILI NA WAUGUZI WATANO WAZIRAI.[/h]

[h=3]
[/h]


Vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na wangonjwa katika Zahanati ya Ipinda, iliyopo Mwanjelwa jijini Mbeya vikiwa wazi baada ya wagonjwa kukimbia mara baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.

Mgonjwa aliyekuwa akitibiwa Zahanati hapo akiwa amezirai baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi.

Wauguzi waliozirai wakiwa nje ya Zahanati mara baada ya kutibiwa

Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akionesha Bomu la machozi lililopigwa na Jeshi la polisi na kuingia ndani ya Wadi.

Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akielezea jinsi bomu la machozi lilivyopingwa.

Muuguzi akionesha eneo ambalo bomu la machozi lilipotua katika Zahanati ya Ipinda, eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya.

Mtaalamu wa masuala ya maabara katika Hospitali ya UHAI BAPTIST Dk Ngangele Lisukile akionesha bomu la machozi lililopingwa hospitalini hapo majira ya saa 5:30 asubuhi.

Mtaalamu wa masuala ya maabara katika Hospitali ya UHAI BAPTIST Dk Ngangele Lisukile akiwa ameshika kigae kilichodondoka mara baada ya bomu la machozi lililopingwa hospitalini hapo majira ya saa 5:30 asubuhi.



[h=3]LIVE! Kikao kinaendelea kati ya Serikali na wamachinga Mbeya[/h]


Kikao Kimeisha

Ulinzi waimalishwa zaidi Wakati wa Mkutano



Mkuu wa wilaya akiwa amekaa baada ya wananchi kukataa kumsikiliza

Muheshimiwa Joseph Mbilinyi akihutubia

Mkuu wa Wilaya Kushoto wakiwa na Muheshimiwa Joseph Mbilinyi

Kikao Kimeanza sasa watu ni wengi sana Mh. Joseph Mbilinyi anahutubia sasa..

Wanainchi wakiwapokea viongozi kwa Shangwe
Picha na Stanslaus yupo kwa tukio sasa endelea kufuatilia
Mbeya Yetu






 
Back
Top Bottom