- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Huu ni ujumbe wa Sugu kweli?
Huu ni ujumbe wa Sugu kweli?
- Tunachokijua
- Joseph Mbilinyi (Sugu) ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Nyasa. Sugu ni msanii pia ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini.
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook kumekuwa na grafiki inayosambaa ikiwa na utambulisho wa Jambo TV ikiwa na ujumbe kuwa;
"Sugu aibua mjadala: CHADEMA inakimbia kupiga kura, inashambulia upinzani"
Grafiki hiyo imeambatanishwa pia na inayoonekana kuwa ni screenshot ya kile kinachoonekana ni kutoka kwa Joseph Mbilinyi (Sugu) kupitia ukurasa wake wa X.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Utafutaji kupitia maneno muhimu umebaini kuw ahakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo kumuhusu mwenyekiti wa kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu).
Kupitia ufuatiliaji kwa njia ya mtandao imebainika kuwa ujumbe huo unaonekana kuw aumechapishwa katika ukurasa wa X wa Sugu ni wa kughushi na haujachapishwa naye.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X hadi kufiki Oktoba 9, 2025 ulikuwa ukionesha taarifa ya mwisho kuchapishwa ilikuwa ya Oktoba 4, 2025 ambapo kiongozi huyo alichapisha ujumbe pamoja na video akiwa kwenye ufunguzi wa GO GLOBAL huko Atlanta Marekani.
Aidha grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ikiwa na utambulisho wa jambo TV ni ya kughushi kwani ina mapungufu kadhaa ikiwemo kutumia aina tofauti ya mwandiko na inayotumiwa na chanzo hicho, hata hivyo ufuatiliaji umejirirdhisha kuwa haikuchapiswa na Jambo TV.