Sugu Awaka, Amwaga Cheche Bungeni!

Usidanganyike kijana kuwa kuna mwana siasa yuko pale kukutetea wewe, ile ni kazi yao ya kuwaingizia vipato vya ziada na kuwaongezea umaarufu. Wapi kwingine watapata coverage ya TV na kujiongezea umaarufu huku wanalipwa zaidi ya pale? fikiri.

Nnakuhakikishia hakuna hata mmoja anaegombea ubunge akawa yuko kwa nia ya kusaidia wengine, kwanza ni kujisaidia yeye mwenyewe. Wanafik tu, hawana lolote. Pale ni njia ya mkato.

JF Comedy
 
Kijana usiyekuwa na huruma kwa vijana wenzako,huyu Mh(MB) Mwanaharakati Mtetezi wa wanyonge a.k.a Sugu anawatetea wanyonge wewe unaona ka vile anapiga kelele,kuna siku utakuja kumkubali kwa haya mazuri anayoyafanya


Mkuu usijiangaishe na FF kwani anajulikana yuko mlengo gani. Yeye ni mtetea mafisadi na pia mtetezi mzuri wa serikali dhaifu ya Kikwete. Hakuna chochote kinachoweza kufanywa na wapinzani yeye akakifagilia. In short FF ninahisi ni UWT/TISS au yuko kwenye payroll ya Nape. Ni kosa kumwita kijana. Huyu ni mtu mzima mwenye akili zake lakini anajifanya hamnazo. Kwa udini ni namba moja. Yuko kwenye ignore list yangu kwani uwa sina muda wa kujibizana na watu wa kariba yake!!!!

Tiba
 
Huyo jamaa nilimsikiliza kama dakika moja hivi nikaona anapiga kelele tu, hata kuongea hajui.

FF unanitafutia ban humu, una roho mbaya mwenamke wewe, kuna tetesi kuwa Magamba wamekuwa wakikutumia kuwa-Mwakyembenize watu wanaopingana na ufisadi. Unachekesha lol !!
 
pia amesema nchimbi kaweka " washkaji" zake kwenye kamati ya vazi la taifa,hawana utaalam wowote

namuunga mkono kabisa
huyu jamaa ni mpuuzi ukinywa nae ukamsifia tu kuhusu wanawake ama kumpelekea mademu anakuingiza kwenye kamati...imeshangaza kajaza wahuni watupu kwenye kamati ya vazi la taifa

hilo mwanzo
umeona ile kamati ya sijui wanaita nini ya bmt
ni aibu kaweka wahuni wenzake anakunywaga nae pale breakpoint bila aibu sikuhiyo naona majina kadhaa nikacheka sana nikaona kumbe nikiona waziiri anakunywa na mie ntakuwa pembeni yake labda ntachaguliwa vazi la wapenzi bora 2012
 
Wakati wa majumuisho, Nchimbi kaipangua hii hoja na kumopaka sana Sugu kuwa hawezi kuwateua watu makini eti tuu kwa sababu anajua fulani ana bifu na fulani. Pia akapaka hauwezekani ugomvi udumu zaidi ya miaka 10, ukishakuwa mbunge ni kiuongozi wa umma, hivyo sasa wewe ni kioo cha jamii, sahau yaliyopita songa mbele, haya ma bifu mpaka kuimbana na kutukanana matusi mpaka ya nguoni sio mambo!.

Mh jamani Nchimbi kasahau kuwa kuna watu wanaozea segerea kwa kuwa na bifu na Mkuu??
Amesahau kilichomfanya Waitara kutolewa u CDF soon after JK kuingia Ikulu? ugomvi huu umetoka enzi zile JK yuko chu cha jeshi akiwa kapelekwa na CCM.
Visasi vya wakuu vinakaa hata miaka 30.
Ila kiukweli wasanii wananyonywa sana. zamani ilikuwa wahindi wanaosambaza kazi zao, bt now haya matamasha yanawaumiza sanan na hawana jinsi maana soko lao limeporwa na wizara ya kuwasaidia ya Nchimbi ndo imetiwa mfukoni na Clouds. Kuna tabu sana hapa na Sugu hataweza kupumzika mpaka kieleweke.
Nisichopenda ni jinsi anavyowasilisha ujumbe wake. Lugha inayotumika si ya kimaadili. Ila mapambano yake ni mazuri hasa kwa wasanii wasio na pa kutokea au wasio na mtetezi.
 
namuunga mkono kabisa
huyu jamaa ni mpuuzi ukinywa nae ukamsifia tu kuhusu wanawake ama kumpelekea mademu anakuingiza kwenye kamati...imeshangaza kajaza wahuni watupu kwenye kamati ya vazi la taifa

hilo mwanzo
umeona ile kamati ya sijui wanaita nini ya bmt
ni aibu kaweka wahuni wenzake anakunywaga nae pale breakpoint bila aibu sikuhiyo naona majina kadhaa nikacheka sana nikaona kumbe nikiona waziiri anakunywa na mie ntakuwa pembeni yake labda ntachaguliwa vazi la wapenzi bora 2012
mkuu ndo tatizo la kuwekana,yeyealiwekwa na mshikaji wake naye kawatia washikaji zake.
 
Pia amesema Nchimbi kaweka " washkaji" zake kwenye kamati ya vazi la taifa,hawana utaalam wowote
Mazingaombwe haya! Vazi la taifa kwa wavaa mitumba wapi na wapi?
Vazi la taifa tenda ya kushona atapewa fisadi Fulani na tenda ya kusambaza fisadi mwingine, Halafu itatolewa amri Kila siku ofisi za serikali kuvaa vazi la taifa. Ni ufisadi tu sintovaaa Hilo vazi
 
Hahahah...alikuwa anasoma, mbaya zaidi hata kusoma hajui!
Wewe unaejua kusoma uko wapi,Bora yeye ambaye hajui kusoma yuko pale Mjengoni na tena ni waziri kivuli bila kusahau ni kati ya waanzilishi wa Bongo flava, na ule mradi aliodhurumiwa na vibaka wa Maendeleo ya
vijana.
Kong'wa nzoka utabaki vile vile na kujipendekeza kwako kwa yule mshikaji aliyekuweka mjini.
 
Mazingaombwe haya! Vazi la taifa kwa wavaa mitumba wapi na wapi?
Vazi la taifa tenda ya kushona atapewa fisadi Fulani na tenda ya kusambaza fisadi mwingine, Halafu itatolewa amri Kila siku ofisi za serikali kuvaa vazi la taifa. Ni ufisadi tu sintovaaa Hilo vazi

kwanza vazi la taifa si ni rubega na kaniki kwa kina mama,sasa kamti ya nini kama si ufisadi tu.ni kweli watalazimiswa( ofisi za serikali) kulinunua kama gazeti la uhuru
 
Back
Top Bottom