POTOSHI Sugu asema Lissu ni Mhaini, wana CHADEMA kanda ya Nyasa wanaikataa na hawaitaki 'No reforms, No election'

POTOSHI Sugu asema Lissu ni Mhaini, wana CHADEMA kanda ya Nyasa wanaikataa na hawaitaki 'No reforms, No election'

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

1755951957461.png

1755951972129.png
 
Tunachokijua
Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ni mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa lakini pia amewahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi tofauti kupitia jimbo la Mbeya Mjini.

Mnamo tarehe 20 Agosti, 2025 Sugu alifanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine alibainisha kuwa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa licha ya watu kupotea akiwemo Deus Soka na wenzake. Aidha alieleza kuwa dola imeendelea kuonesha ubabe kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kufungia makanisa na kuwanyima raia haki yao ya kuabudu, na baadaye akasisitiza kuzunguzma yale yanayoendelea ni jukumu la watu wote, si jukumu la wanasiasa wala wanachadema peke yake.

Aidha aliongeza kuwa, mwenyekiti wa CHADEMA nchini Tundu Lissu, aachiwe bila masharti yoyote kwani yeye siyo Mhaini bali ni kesi ya kisiasa.

Madai ya Video

Kutokana na mkutano huo kumekuwepo kipande cha video kinachomuonesha kuwa Sugu alisema Lissu ni Mhaini, wana CHADEMA kanda ya Nyasa wanaikataa na hawaitaki 'No reforms, No election'


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video, umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande visivyohusiana kutoka kwenye Video ya mmkutano wa Sugu na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari Joseph Mbilinyi (Sugu) alisema wana CHADEMA kanda ya nyasa wanasimama na msimamo wa 'No reforms, No election' pamoja na kukataa sheria za hovyo za uchaguzi zinazoleta kadhia kwa wagombea na wapiga kura na kudai mabadiliko ya sheria hizo.

Aidha aliongeza kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA nchini, Tundu Lissu aachiwe mara moja bila masharti yoyote, yeye siyo mhaini, kwani kesi hiyo ni ya kisiasa.

Rejea hapa kuanzia dakika ya 12:11


View: https://www.youtube.com/live/uKYw8JinUVc?si=l-_jh5PlNprohw_c&t=731
Back
Top Bottom