Sugu amvaa Nchimbi

WaTanganyika mnanishangaza sana tena sana . Hapa la Kusaga na Ruge kupewa studio mnalalamika mbona suala la MoU ya kanisa na Serikali hamlalami?

Au kwa kuwa nanyi mpo kwenye kunufa

Acheni unafiki .Poleni sana,

kwani we al zakhawi ni mtanzania?
 
WaTanganyika mnanishangaza sana tena sana . Hapa la Kusaga na Ruge kupewa studio mnalalamika mbona suala la MoU ya kanisa na Serikali hamlalami?

Au kwa kuwa nanyi mpo kwenye kunufaika.

Acheni unafiki .Poleni sana,

kwani wa kizazi hicho walikuwa wamelala? Hawa hii ni generation yao..
 
Huna hoja hapo kwenye red...unajuaje kama alishaandika na sasa anawajuza watanzania waujue ukweli wa mambo..usidharau facebook..hata Obama raisi wa taifa kubwa duniani anaitumia.
Hebu acha ushamba mkuu hivi wewe unadhani watanzania wangapi wana account za facebook au twitter? marekani na ulaya viongozi wanatumia facebook na twitter sababu asilimia kubwa ya raia wao wanaenda sawa na technology sasa Tanzania ni watu wachache sana wanasoma.
 
nilifuatilia mabishano yake na Nchimbi bungeni... Nchimbi alimweleza spika kuwa Sugu amekuwa akimjia ofisini mara kwa mara juu ya suala hilo.Majibu anayompa anayaelewa ila hayakubali. Kifupi alimaanisha BASATA ingeleta urasimu.Chombo kilichoundwa kusimamia studio kiko huru kwa kuhudumia wasanii wote.. Sugu akanyanyuka kwenye swali la nyongeza,tena kwa jazba,akamwaga sana povu,akataja Lady Jay Dee sijui kafanyaje... Nchimbi akajibu kifupi,serikali haina muda wa kujadili personal issues
 

Jamani tusiwe kama watoto tunasahau mapema kama hizi kelele za kulalamika tu online zinasaidia ufisadi usingekuwepo leo hii,Sugu inatakiwa aulize kwenye kipindi cha maswali na majibu cha bungeni (Ajue msimamo wa serikali katika hilo).
Kuna mahakama hapa Tanzania kwanini asiende kuwashtaki si anajua data zote la hilo sakata,mimi sikubali kwamba kuandika status facebook na kuwasilisha bungeni kwenye hotuba tu ni harakati, Je kipindi ameongea bungeni alipewa majibu gani na kuna muongozo upi wa sheria ?

Tusiwe washabiki tu hili suala la clouds,kuna wasambazaji,promoter na mambo mengi tu yanachangia hali mbaya ya wasanii na sugu kama mbunge na mwanaharakati wa medani ya burudani basi inatakiwa afanye zaidi ya haya, kufika kule tunapotaka.
 
Hiyo nimeshasoma kitambo tu labda ubandike majibu ya serikali kuhusiana na hilo ndio nijue pumba na mchele, maana tusiangalie upande mmoja tu.
 
WaTanganyika mnanishangaza sana tena sana . Hapa la Kusaga na Ruge kupewa studio mnalalamika mbona suala la MoU ya kanisa na Serikali hamlalami?

Au kwa kuwa nanyi mpo kwenye kunufaika.

Acheni unafiki .Poleni sana,
Hapo kwenye red tamko limeshatolewa sheikh wangu , kumbe tulivyokua tunapinga MOU tulikua tunachemka, Sheikh Salimu ametoa ujumbe kutoka bakwata na kuwataka wahadhiri wa kiisalmu kusitisha maandamano kupinga MOU na badala yake na sisi waislamu taundae proposal tupewe misaada ya kuendeleza huduma za jamii na sio kupinga maendeleo yanayofanywa na makanisa.
Tuchangamkeni Sheikh wangu, yani kuhusu hili swala la MOU waislam tunajidhihirisha kuwa ni weupe pee vichwani.
 
Hili la BASATA halimuhusu kama mbunge??

Unasahau kuwa Sugu ni waziri kivuli wa Utamaduni na michezo hivyo anavyofanya ni sehemu ya majukumu yake!! Sasa la msingi mjibu hoja anazoziibua. Kama Mkweree aliwapa hiyo studio hao waliomfanyia kampeni aseme hivyo badala ya kuwahadaa wanamuziki vijana wote kuwa angewatengenezea Studio!!
 
Matatizo ya kuongozwa na form four failure.
 
Kweli wewe mtanzania halisi.

Kama ni maswala ya umri Tanzania kusingekuwa na shida maana hatuma kiongozi mtoto (30+), kwahiyo mi naona ungejibu hoja tu umri mpaka sasa haujasaidia kutatua matatizo yetu.

Jitahidi sana watoto wako wasisome shule ulizosoma wewe ingawa ni rahisi sana kuridhi namna ya kufanya argument kutoka kwako kwa kupitia viasili mwili.
Kama ndani ya nusu saa unasema Sugu afate taratibu zinazopaswa juu ya swala hili badala ya kuandika fesibuku, nimekuwekea document inayoonyesha taratibu zilizofatwa na cha ajabu saa hivi unaniambia tena eti nikubandikie majibu ya serikali juu ya hili, jaribu kuwa na tabia ya kutokuogopa maandishi mengi,tafuta majibu na maamuzi ya serikali juu ya hili alafu ndo ufanye argument.
No research no right to speak.
 
Katika hili, Sugu alishasema bungeni kwa kumuuliza waziri husika, pia wakati wa bajeti ya wizara ya Sophia Simba, napo Sugu aliuliza. Lakini katika nyakati zote hizo, majibu yalikua ni blah blah. Pengine ndio maana Sugu ameamua kutafuta njia nyingine za kufikisha ujumbe. Lakini wazo na swali la Kiranga nalo ni muhimu kuzingatia. Inabidi Sugu na crew yake waanze kuangalia namna nao watajipanga katika kufanya mradi kama huo (studio). Kwa namna hiyo Sugu ataweza kua ametoa fursa ambazo anaona Clouds na genge lake wamewanyima wasanii wengi kwa kupora studio ambayo Kikwete alijenga kwajili ya wasanii wote!! Otherwise ni kweli kelele za Sugu bila mbadala wowote zitakua nuisance muda si mrefu!!
 
Aaaah mimi naomba mungu nikizeeka nisiwe kama wewe, toka mwanzo nimesema kwamba kupiga kelele tu facebook haisaidi kitu sasa sisi wananchi tufanye nini?
Sugu kama mbunge atafute njia mbadala ya kutatua tatizo na sio kuandika facebook halafu mbona hasemi majibu ya serikali unadai blah blah.
Hapo kwenye red ulisikia wapi unanitisha kuhusu shule yako au ndio darasa la nne la zamani, sasa unadhani wanaanzaje kufanya research
 
Kutegemea tegemea serikali saa zote mwanamme noma. Kulilia lilia serikali kila kitu "mpiganaji" noma.

Jenga chako na wako tuone, serikali ikikuingilia tutaitoa baru.

Ni lazima serikali itumie vizuri kodi zetu, kama inaanzisha mradi ni kwa ajili ya wadau husika ama watanzania wote.

Kutumia kodi zetu kuanzisha studio na kuikabidhi kwa kampuni binafsi haikubaliki hata siku moja. Na kama wewe unaona sawa, ni kwanini Kusaga na Ruge wasitumie fedha yao wenyewe kutengeneza studio yao hadi wanasubiri kufanya ujanja ujanja kwenye vitu vya umma?
Ulishawahi kumsikia mtu akilalamika kwanini wameanzisha clouds entertainment group?
 

Alipozungumza bungeni ulikuwa wapi kutazama tv, kusikiliza redio ama kusoma magazeti na mitandaoni? Nyie ndio mliokuja hapa kulalamika kwamba kwanini azungumzie bungeni ambapo mtuhumiwa ruge hawezi kujitetea. Kama amemuandikia barua na hataki kujibu ulitaka akae kimya? Na hiyo studio si kwa ajili yake bali anaipigania kwa niaba ya wasanii wasiokuwa na uwezo na nafasi ya kusema kama Sugu, na kwakuwa naye ni msanii basi ana kila sababu ya kuwasemea wenzake.
 

Raisi kikwete alivyokuwa anaandika kwenye facebook jana kuwapa pole wahanga wa mafuriko pamoja na kuwaomba watanzania washiriki kikamilifu katika kuwasaidia waathirika alikuwa anawaandikia wamarekani na ulaya , sio?

Kwahiyo unataka kusema wale waliokumbwa na mafuriko wana account facebook na twitter lakini wasanii wa muziki pamoja na wadau wengine wa muziki hawana? au ulitaka kusemaje hapo ili ueleweke.
 
Kwa haya majibu yako hasa hapo kwenye red, nakushauri usipende kukaa mda mrefu na watoto wako ili wajikomboe kifikra.
An empty head is devil's workshop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…