Sudan nao washtukia ushenga wa Marekani baina ya waarabu na Israel

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,162
10,890
Yule msomi wa kimarekani aliyepewa sifa kubwa Sudan na kukabidhiwa serikali ya mpito baada ya kuanguka kwa Omar Albashiri na ambaye wiki kadhaa zilizopita aliponea chupuchupu kufa kwa bomu barabarani,jina lake Abdalllah Hamdouk, sasa naye ameishtukia diplomasia ya Marekani.

Wiki iliyopita waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Pompeo aliingia nchini humo kufanya mazungumzo na watawala wa Sudan,hata hivyo undani wa mazungumzo hayo haukujulikana mpaka jana wakati Abdallah Hamdouk akihutubia wananchi wake alipofichua siri ya mazungumzo hayo.

Abdallah Hamdouk akasema pamoja na haja ya nchi yake kutolewa kwenye orodha za nchi zinazofadhili ugaidi iliyonayo Marekani lakini hawataki kutolewa huko iwe kwa thamani ya kurudisha uhusiano na Israel.Akaongeza kwamba kurudisha uhusiano na taifa hilo rafiki na ndugu wa Marekani kunahitaji mjadala zaidi na vigezo kuzingatiwa.

1601205954532.png
 
Back
Top Bottom