Subira

wimbo mmbaya,sababu kwenye outro umeninyima korabo hata yakunirusha kama zile nyimbo za kikongo haujafanya
Hahhahahaaaa ningekurusha ukaanguka ukaumia kiuno ningenunua kesi
 
Zuwena zuwenaaaaa kweli nakupendaaaaaa.
Hiyo Surrender bridge si waiongeze tuache kugongana? Kweli na kupendaaaaa. Zuwena alipo sijui ila mtoa mada katangulia kwa mola tena mjidai mseme hakuna kama yeye wala Maneti wala king kiki wala zembwera nikitaja wote nitawehuka we acha tu.
 
subira yangu ndo iliyonipoonza,
ngoja ngoja naonekana mjinga,
kwa sababu nilimpenda kweeli,
kwa sababu nilimpenda kweeli?

sasa ndugu endelea kusubiri!.....
Yule mdada aloact kwenye hiyo video ni nani na yupo wapi sababu mhu sisi ndo wale wa kuita watoto watuwekee tunachotaka kuangalia.
 
ngoja ngoja naonekana zobaaaaaaa? Kwa sababu nilimpenda Zoba mbona akina mwampemba wanawin yeye mh.
 
Nyimbo nzuri mkuu, ila nna mashaka walioitambua ni wachache sana, maana wenyewe wameshazoea miziki yao ya sikuhizi yenye adhabu katikaki ya burudani utasikia mikono juu, mikono juu, piga keleeeee
Kuna Binti Mmoja Akanilazimisha Twende Kwa Hizo Ngoma, Nikaona Aaah Isiwe Shide Ngoja Twende.
Kufika Pale Mi Nikakaa Kaunta Nikaanza Kunyonya dawasco pale Ye Huku Anapigishwa Adhabu Huku Ananishangaa We Mbona Hupati Steam, Nikamwambia Mi Nawasubiri Twanga Wapande Ndo Niwe Na Raaaaha.
It Was At Moshi Ushirika Stadium
Eti Adhabu
 
wachache sana watakusoma hapa
 
Stahmil na upoe zidisha uvumilivu
Uvumilie muumba ndo mwenye nguvu
Dua ninawaombea wale walotaharuki
Wazidi kuendelea kwani chuki makhuluki
Ipo siku watajua ukweli haufichI.
 
Stahmil na upoe zidisha uvumilivu
Uvumilie muumba ndo mwenye nguvu
Dua ninawaombea wale walotaharuki
Wazidi kuendelea kwani chuki makhuluki
Ipo siku watajua ukweli haufichI.
Dah nilikatisha kwa kusahau huu mwendelezo asante sana komredi
 
Ha ha haaaa. Mshana hapo mwisho inakuwa:

'Maovu si sifa yangu na kugombana sitakiiii'.
 
Asante mamito....huu wimbo ulikuwa dedication yako na ule mwingine wa Njia peleka salamu...
Lols,

Tena njiwa peleka salamu nnaupendaje.

Njiwa peleka salamu?, ah kwa yule wangu muhibu.
Umueleze afahamu, kama ninapata tabuuuu.
Hali yangu mahamumu, aahh maradhi yamenisibu.
'Ewe njiwa, ewe njiwa, peleka salamuu.
Kwa yule kwa yulee, wangu muhibuuu.
 
Shukran pamoja sana komredi wacha tukumbuke vizuri vya kale.
Hebu tujaribu na huu nikikwama tia neno
Njiwa peleka salamu uu ooh kwa yule wangu muhibuuu
Ukifika aaa muelezee kwamba ninapata tabu uu
Pendo langu halijaishaaa..........


cc: Angel Nylon
 
nimejaribu hapo chini kumbe nimechapia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…